Elections 2010 Maandamano- uchaguzi tanzania jumamosi nov 6washington dc 2010, 10:am (white house)

mlitegemea muibe na kuwakatili wapenda mabadiliko na watu wote waseme amen? Mmeliwa na huo ni mwanzo tu.

tupatieni vibali maana mmeziti kwa vibali, barua za kutunga kuibiwa wakati huna cha kuibiwa, wezi wakubwa tunasubiri ndoa ya rais wenu,, tutekeleze ilani ya ccm kwa maendeleo, kidumu ccm
 
Mlitegemea muibe na kuwakatili wapenda mabadiliko na watu wote waseme amen? Mmeliwa na huo ni mwanzo tu.
Tatizo mmechelewa sana, na sijui kwa nini mmeshindwa kujifunza kwa tokea 1992... wakati mkijiandaa na kuandamana sie tunashereheka na Ushindi!
 
tupatieni vibali maana mmeziti kwa vibali, barua za kutunga kuibiwa wakati huna cha kuibiwa, wezi wakubwa tunasubiri ndoa ya rais wenu,, tutekeleze ilani ya ccm kwa maendeleo, kidumu ccm

Nani akupatie kibali? kibali cha nini?

Kajifunze kwanza kutype ndio uje.
 
Mimi nakataa Kikwete siyo chaguo la Watanzania

1.Sikumpigia kura yangu. Ndugu zangu wa karibu na marafiki zangu wengi hawakuwa wakimtaka na walikiri kutompigia kura
Ni kiherehere chako!
 
Tatizo mmechelewa sana, na sijui kwa nini mmeshindwa kujifunza kwa tokea 1992... wakati mkijiandaa na kuandamana sie tunashereheka na Ushindi!

Of course mwizi siku zake 40..zenu bado hazijatimia...ila karibia zitafika 40..soon
 

uchaguzi umekwisha tugange yajayo
kikwete rais wetu wote..............................................
 

uchaguzi umekwisha tugange yajayo
kikwete rais wetu wote..............................................
akha! be raisi wako wewe baba yako na mama yako mi wala mi raisi wangu ni slaa Dr wa ukweli
 

uchaguzi umekwisha tugange yajayo
kikwete rais wetu wote..............................................

Huu ndio upuuzi wa watz wengi..wanadhani demokrasia ni election tu..kwendeni zenu motoni na dhana zenu mfu.
 
Hongereni! Najua utetezi wenu si kwa ajili ya nafsi zenu bali ni juu ya masikini, wajane, watoto, walemavu, walalahoi na wote wasiojiweza in Tanzania, ambao kwa miaka 50 hawana mwelekeo wala matumaini ya kutokana na hali zao.
 
Hongereni! Najua utetezi wenu si kwa ajili ya nafsi zenu bali ni juu ya masikini, wajane, watoto, walemavu, walalahoi na wote wasiojiweza in Tanzania, ambao kwa miaka 50 hawana mwelekeo wala matumaini ya kutokana na hali zao.
Bado tusisahau suala la Kujitegemea, ni vema kila mwananchi kujua hili kwani ndio njia sahihi ya kufikia malengo binafsi kwa kila mtanzania. Aidha kwa upande mwingine huu ni wakati mzuri kwa wananchi kushiriki moja kwa moja katika kutatua matatizo yao ya msingi.
 
Mimi nakataa Kikwete siyo chaguo la Watanzania

1. Sikumpigia kura yangu. Ndugu zangu wa karibu na marafiki zangu wengi hawakuwa wakimtaka na walikiri kutompigia kura
2. Kachaguliwa na Watanzania 5,276,827 (Zikiwepo na kura za maluani - uchakachuaji) kati ya Watanzania zaidi ya Milioni 40
3 Wananchi waliojiandikisha zaidi ya 11,511,020 ambao ni asilimia 57.16% hawakupiga kupiga kura kutokana na either kuhofia kura zao kuchakachuliwa au mfumo mbovu uliowekwa ili kupunguza kura za wapinzani mfano, kuzuia raia kupiga kura ya raisi sehemu yoyote ya nchi wakati anachaguliwa raisi wa nchi nzima au kufunga vyuo vya elimu ya juu na mashule.
4. Kachaguliwa na wananchi wengi walio vijijini kutokana na uelewa mdogo.
5. Amesaidiwa sana na vyombo vya ulinzi na usalama na taasisi za serikali vikiwemo vyombo vya habari vya serikali kufanikisha matakwa yake na familia yake
6. Katumia gharama kubwa sana katika kampeni (Mabango kutoka Canada, magari ya kifahari nk. wakati Watanzania wanaishi maisha ya dhiki kubwa
7. Ahadi zake ni nyingi na amezitoa nje ya Ilani kama alivyothibitisha meneja wa kampeni zake na yeye mwenyewe alisema nyingine zilikuwa za papo hapo.
8. Miaka mingine mitano ya Wadanganyika kudharaulika na kunyanyaswa na mafisadi wakati president akijikomba kwa wale Nyerere aliosema - nanukuu "Mijitu hii lengo wao ni kututawala, kwa nini tunawaongezea uwezo wa kututawala?'' mwisho wa kunukuu

Waliopiga kura 8,626,283 = 42.84%

Kura zilizoharibika = 2.64%

Mgawanyo wa kura ni hivi:

APPT: 96,933 = 1.12%
CCM: 5,276,827 = 61.17%
CHADEMA: 2,271,941 = 26.34%
CUF: 695,667 = 8.06%
NCCR: 26,388 = 0.31%
TLP: 17,482 = 0.20%
UPDP: 13,176 = 0.15%

Ndio ameisha kuwa sasa, huna la kufanya na leo hii yupo anaapishwa kwa mujibu wa Katiba ambayo ndiyo sheria mama. Ww hukumchagua , ila wengi wamemchagua kwa uchaguzi huru na wa haki ndio maana amepata hizo 61.17% huo ni USHINDI WA SUNAMI AU KISHINDO WAWEZA KUUITA.
 
Watumwa wakubwa nyie, Oboma ndio baba yenu? Tz ni nchi huru aichaguliwi rais na Marekani. Mimi niko Washngton na si shiriki kwenye upuuzi wenu.
Mafisadi kama wewe hatuwahitaji washiriki. Tunataka MATAIFA yasikie, sio tu Obama kama ufinyu wa .....yako unavyodhani.
 
JK amesaidiwa na dola, serikali, na media. Bila shaka mhimili mwingine yaani Mahakama umejipanga pia kumsaidia. Nguvu ya Umma= Uhuru
 
Ndugu Watanzania ambao tunaoshi maeneo ya Washington DC, tunawatangazia wote kwamba tutafanya mandamano ya kupinga matokeo ya uchaguzi mkuu, 2010 na namna shughuli ya kuhesabu kura za uchaguzi zilivyofanywa na Tume ya Uchaguzi wa Tanzania ambao uligubikwa na wizi na udanganyifu wa hali ya juu katika sehemu na maeneo mbalimbali nchini Tanzania. Kwa kuwa State Department imetoa ridhaa ya maandamano haya ya amani, tunawaomba Watanzania, wanayoipenda Tanzania, sehemu yoyote walipo hapa Washington DC, Maryland, Virginia na Pennsylvania wajitokeze kwa wingi, wake kwa waume, watoto na kumbuka kuja na bendera, mabango, ngoma, zeze na vinubi, Tshirts ili message ifike kwa Presedent Obama.

Tunawaomba watanzania wote waishio Marekani mujitokeze kwa wingi katika kupinga matendo hayo ya ubadhilifu nchini kwetu. Kwa wale ambao wanataka kujitokeza wasiliana nasi kwa: #202 367 2761 # 301 655 6577 # 224 628 8279

Tunaomba kibali kopy yake hapa na pia hizo number za simu mbona kama ni mtu kaamua kuzitaja? what if i am calling while I am outside USA-then what is the code number? kama vile sizpati?? na useme ni mobile au residential kamanda? Acheni upigaji as those numbers does not exist guys. Msiwadanganye watu kwani huwa twataka ukweli wa haswa. Nashauri hii thread ifungwe kabisa na MD.
 
Back
Top Bottom