Maandamano Thailand: Democrasia inaelekea kubakwa

Mshombsy

JF-Expert Member
Mar 15, 2013
372
180
Wote mtakuwa mnafahamu maandamano yanayoendelea Thailand kumng'oa waZiri mkuu mwanamke Shinawatra yakiwa yamechochewa na mswada bungeni wa kutaka waziri mkuu wa zamani Thaksin Shinawatra apewe AMNESTY.

Madai ya waandamanaji ni kutaka kabisa kuondosha ushawishi wa kisiasa wa familia ya Shinawatra. Maandamano yanaungwa mkono na chama cha Upinzani cha Democratic Party.

Cha kushangaza waandamanaji na hicho chama hawataki kuitishwa uchaguzi bali liundwe baraza la watu waadilifu kuongoza taifa lao.

Madai haya yanapingwa na Waziri Mkuu mwanamama Shinawatra na chama chake Tawala. Jana Waziri mkuu huyo alisema ataitisha kura ya maoni watu waamue mwelekeo wa taifa lao lakini leo ameamua kulivunja bunge na kuitisha uchaguzi.

KUBAKWA KWA DEMOCRASIA

Wanaopinga serikali yani waandamanaji wanajua hawawezi kushinda uchaguzi kwani Waziri mkuu aliyeko uhamishoni T. Shinawatra alipoingia madarakani aliweka sera zilizowagusa watu wa chini kilichopelekea yeye chama chake na vile anavyoshirikiana navyo kushinda chaguzi zote toka mwaka 2001.

Wapinzani wanajua hilo ndio maana wanataka liundwe baraza kuu kuongoza serikali.

Kwangu mimi hii ni kubaka demokrasia, nilitegemea chama kinachojiita Democratic kidai uchaguzi mapema lakini hakitaki kwasababu demokrasia ya watu kuchagua serikali yao hawanufaiki nayo.
 
Kwanini viongozi wa Thailand wakikutana na Viongozi wa Tanzania, serikali yao inakuwa matatani? Mhe. EL alipoenda kule Thailand kununua mvua, hazikupita siku serikali ya wakati ule ilipinduliwa na dili la mvua likayeyuka! Hivi karibuni, Waziri Mkuu wa Thailand alitembelea Tanzania na baada ya kurudi, kasheshe za kumg'oa ndiyo hizo. Hapa pia, naona dili za watu zitayeyuka!
 
Back
Top Bottom