Maandamano: RPC wa Mtwara kaonyesha ukomavu lakini nina hofu na hatima ya kibarua chake

Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
43,080
2,000
Wakuu hatuna budi kumpongeza RPC wa mtwara kwa kuruhusu kufanyika kwa maandamano leo huko mkoani Mtwara.Ni hatua nzuri inayoonjesha uwajibikaji kwa mujibu wa sheri na kanuni za nchi.Ni ma-RPC wachache wenye moyo huu kwa sasa.Nisiwalaumu sana hawa makamanda wa polisi wa miko kwani inawezekana wanafanyva kazi kwa maelekezo ya wakuu wao wa kazi

Hata hivyo,sitashangaa kuona maandamano haya yakiathiri kibarua cha RPC huyu kwa namna moja au nyigine.Nasema hivi kwasababu wakubwa wetu kwa maana ya watawala hawapendi kuambiwa ukweli.Ukiangalia baadhi ya mabango mengi yalikuwa na ujumbe uliomlenga mkuu wa kaya na ukisoma ujumbe kwenye yale mabango na kwa tafsiri ya watawala wetu ni kuwa mh.mkuu wa kaya atakuwa amedhalilishwa na maneno yale.Ukweli ni kwamba ukisha ruhusu maandamano ni vigumu kudhibiti mabango hata kama yana ujumbe usiowafurahisha watawala.

Baada ya kusema hayo,ni wazi kabisa kuwa kama RPC huyu aliruhusu maandamano haya bila kuwashirikisha wakubwa si ajabu wakamtoa kafara.Hata hivyo,inawezekana serikali imeruhusu maandamano haya baada ya shutuma za kuzima na kuzuia maandamano kuzidi.Pia inawezekana hatua ya kuishitaka serikali katika mahakama ya kimataifa ya nchini uholanzi imechangia kuwaamsha watawala.Vile vile inawezekana pia wanataka kujisafisha mbele ya jumuiya ya kimataifa.Sikutarajia kabisa serikali hii kuruhusu maandamano na ndio maana nina wasiwasi na kibarua cha huyu RPC.
 

bato

JF-Expert Member
Dec 20, 2012
3,813
2,000
Ndugu Rais aliwaambia wana CCM wasitegemee polisi iwatetee wakikosolewa na wananchi.Viongozi wao wenyewe waende kwa wananchi kujieleza.Polisi na vyombo vingine vya dola ni kwa ajili ya umma si kulinda maovu ya serikali. Bravo RPC wa Mtwara.
 

TUKUTUKU

JF-Expert Member
Sep 14, 2010
11,775
2,000
Hata wale jamaa zetu wenye ndevu ndefu na sarawili furi walipoandamana bila kibali serikali iliwatii mara moja na ikatimiza matakwa yao,ingekuwa chadema hapo!!?,
Kwa kifupi uwa tunawaita mujahidina au answari sunny!!
 

Bilionea Asigwa

JF-Expert Member
Sep 21, 2011
16,374
2,000
Viongozi wa SERIKALI SIKIVU huwa wanaogopa maandamano ya CHADEMA tuu sio ya hawa wengine ....Ila kwa hilo la mabango naona kama MUKULU linamuhusu moja kwa moja.............
 

ligendayika

JF-Expert Member
Aug 31, 2012
1,183
1,250
Hawezi kupoteza kazi huku serikarini ukiwa muoga hufanyi kazi si mlimuona JWTZ live watafuata wengi wanajua sasa kuwa nchi hii si ya CCM wala CHADEMA ni ya watanzania wote na sheria zinatuhusu wote. Mtwara wana haki ya wanachokidai
 

mukizahp2

JF-Expert Member
Jul 28, 2012
669
500
mkuu angalia ule uzi unaosema maandamano yanapita mtwara utaona picha za mabango,ila mabango kibao yanapinga maendeleo kupelekwa bagamoyo tu,na mtwara kubaki nyuma
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom