Maandamano ni stahili na staili ya sawia na thabiti ya kudhihirisha nguvu ya umma | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Maandamano ni stahili na staili ya sawia na thabiti ya kudhihirisha nguvu ya umma

Discussion in 'KATIBA Mpya' started by Vox Populi, Feb 27, 2011.

 1. Vox Populi

  Vox Populi Member

  #1
  Feb 27, 2011
  Joined: Oct 23, 2010
  Messages: 23
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  Mara nyingi hakuna mtawala anayependa watu waandamane dhidi ya serikakali yake au hata dhidi yake. Maandamano kwa nchi zisizothamini na kutambua misingi thabiti ya demokrasia ndio njia ya msingi ya watu au jamii fulani kuelezea na kufikisha maoni na ama kuelezea kero zao. Na kwakuwa mwisho wa hekima huwa ni ubabe, mamlaka husahau kwamba wake hapo walipo si kwasababu ya nguvu zao bali ni kwa sababu ya ile wanayoweza kuelezea kama ni dhamira ya watu hata kama si kweli. Maandamano ndio msingi pekee kwa wananchi kuonesha mamlaka yao. Maandamano hufikisha ujumbe mapema. Ni nyenzo ambayo wananchi wanaweza kuitumia vema katika kuona haki na mamlaka yao hayachezewi. Tudumishe maandamano kama sauti ya kimya lakini iliyo na nguvu. Naomba kuwasilishaa!!!!!!!!:A S 112:
   
Loading...