Maandamano nchi nzima, yanaweza kutatua kero zetu?

Jamani eee, tuendelee na mipango ya kuandamana. Tueneze ujumbe kwa kwenda mbele

Wanaokuja hapa kututisha na kutuogopesha wamechelewa. Watanzania wa leo sio wale wa mwaka 1990.

Maandamano yaja, makubwa sana. Tunaendelea kueneza habari hadi vijijiniiii huko mafisadi wanakodhani wananchi ni wajinga.

Mwaka huu imekula kwao, mafisadi mtaangamia tu. Maana Mungu yupo kati ya watanzania.

Hakuna amani bila haki..... Vigogo wa Chama Twawala wanajilimbikizia maekari ya mashamba wakati vijana wa taifa hili wanaangamia. Jamani angalia vijana wanakuwa wapiga debe,wanakuwa wamachinga, dada zetu wanakuwa machangu doa, ndoa zimevunjika kisa wanaume wametelekeza familia kwa sababu ya uchumi m mbaya.

Hawa watu wasio na kazi wangegaiwa hayo mashamba wangelima na kujipatia kipato, na kuwa na makazi ya maana.

Amani iko wapi???


Amani ilikuwapo wakati wa nyerere - elimu ilikuwa bure, afya bure na wananchi walilima bila bugudha.

Wakati wa nyerere kulikuwa na viwanda na ajira zilikuwepo. Uchumi ulikuwa unaonekana kwa kila mtu.

Mafisadi wametafuna viwanda na mashirika yote na wanadhulumu wananchi.

Wanafikiri kwa kutumia ma sa bu ri wanasahau kuwa kuna vizazi vijavyo.

Sasa nani anasema kwa nini tusiandamane.

Mipango ya maandamano iendelee, mimi niko Dar. Nitasambaza vile vipererushi kila kata.
 
jamani lakini inawezekana tukiwa serious. Tunaweza ku demand rais aondoke kama hawezi kuwafilisi mafisadi akiwemo mwanae. Leteni mawazo how do we start mobilizing.

Kwanza tupate orodha kamili ya mafisadi na kiasi cha pesa kwenye akaunti zao na hata na mali zao tuziweke wazi.

Then ukichanganya na matatizo yaliyopo nchini tunaweza kushawishi jumuiya za kimataifa wasitishe misaada tz hadi clean govt itapopatikana.
Wenye data za ukweli kuhusu hawa corrupt leaders aweke hapa tuanze kuzi compile.

'Let's go Tanzanians, we can'

HAYA WATANZANIA, SABABU TUNAZO, TUNASUBIRI TENA. TUMESHAUZWA KAMA WANYAMA LAKINI BADO TU TUNAENDELEA NA UOGA WETU

VASCO DA GAMA ANATUMIA UWOGA WETU KUJINUFAISHA.

SOMA CABLE WIKI LEAKS HAPA UONE UOZO

https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...tuhuma-za-rushwa-dhidi-ya-rais-kikwete-3.html
 
Back
Top Bottom