Maandamano makubwa ya Madaktari yaja (wiki ijayo)

Hamjawachoka bado mnawapenda sana...kama mmewachoka lesen zao za nn?wapen waende hata iran na wao
Waende Iran wakafanye nini? wanajualia wapi operations madr wabongo? Unadhani kwanini watu wanaenda kutibiwa india, watu wanaenda India baada ya kushauriwa na hao hao madr wabongo kwamba hawawezi kazi hivyo wanamwabia mgonjwa mwenye uwezo au sometimes serikali inawafund wagonjwa kadhaa au misaada inatolewa watu wanaenda kutibwa nje.
 
wanatoa dawa za maumivu tu kwa kila ugonjwa? hapo kweli bado unaona kosa ni la daktari? tuliyowachoka ni mipumbavu kama wewe ambayo haiwezi kujiuliza ni kwa nini viongozi wetu wakiugua kidogo ni kupelekwa india lakini mwananchi wa kawaida anakosa dawa na kuishia kupewa panadol tu...halafu eti unamlaumu daktari...
Kuna kitu wabongo wengi hamjui; viongozi wanaenda India coz bongo tunamadr uchwala hawajui vyema haya mambo kwa taarifa yako viongozi wanaenda nje baada ya kushauriwa na hao hao madr kwamba hii kazi au huu ugonjwa sisi madr uchwala hatuwezi hivyo ni vema kama unauwezo ukimbie nje. Hata wewe ungeenda nje ungepewa nafasi. Viongozi hawaumwi malaria wanaumwa magonjwa yao bana ambayo madr wenu hawajafundishwa kuyatibu wao wanafundishwa kuganga maumivu tu.
 
WTF! Madaktari bongo wandhani wao ni akina nani? mbona wanataka waiendeshe nchi hivyo? Huo muda wakugoma wanautoa wapi na huku wagonjwa wakiwa unattended mahospitalini, acheni kazi madr wote mkitaka acheni ndugu zetu waendelee kufa, bora kutoa hizo billions kwa dr from Iran kuliko hawa dr uchwala wa Tz, wanaotoa dawa za maumivu tu kwa kila ugonjwa. TUMEWACHOKA fyuuuuuuuuuuuuuuuuuuuu!!!!!

we kweli wa ajabu na matusi yako! kama unaweza nenda hospitali katibu sasa?si kila kazi unaona ni lelemama kama, halafu hadi leo hii unafikiria mambo ya iran, unaishi wapi? Iran doctors couldnt come because of the letter from US asking TZ president to stop reflaging Iranian for oil!! what am wondering ur G'ment said will recruit retired doctors , where are they? said it did set apart 200bil for "imported" doctors, where is the money? where are those doctors?...back to square one.
 
Waende Iran wakafanye nini? wanajualia wapi operations madr wabongo? Unadhani kwanini watu wanaenda kutibiwa india, watu wanaenda India baada ya kushauriwa na hao hao madr wabongo kwamba hawawezi kazi hivyo wanamwabia mgonjwa mwenye uwezo au sometimes serikali inawafund wagonjwa kadhaa au misaada inatolewa watu wanaenda kutibwa nje.

Wagonjwa wanapelekwa india kwakuwa hospital hazina vifaa mfano Muhimbil hakuna Ct scan..rudishen lesen zao ili muone mbona mnazing'ang'ania si mtafute za kwenu sasa
 
WTF! Madaktari bongo wandhani wao ni akina nani? mbona wanataka waiendeshe nchi hivyo? Huo muda wakugoma wanautoa wapi na huku wagonjwa wakiwa unattended mahospitalini, acheni kazi madr wote mkitaka acheni ndugu zetu waendelee kufa, bora kutoa hizo billions kwa dr from Iran kuliko hawa dr uchwala wa Tz, wanaotoa dawa za maumivu tu kwa kila ugonjwa. TUMEWACHOKA fyuuuuuuuuuuuuuuuuuuuu!!!!!

Sasa we ulitaka wagonjwa wapewe nini wakati hospitalini kuna panadol peke yake. Option iliyobaki kwa Dr ni bora wagonjwa wafe bila kusikia maumivu. Haina shida tumeshazoea hata kwa panadol tunaponaga malaria.
 
Good, saafi sana. I hope those Police people will be fair to let people express their points, sabab hii serikali imeshawazuia mara nyingi sana madaktari hata kukutana kujadili mambo yao. Hoping kweli wataruhusiwa.
 
Waruhusiwe waandamane weeeeeeee

Jioni wakalale, wanaotaka kazi waendelea wasiotaka wakatafute pengine

Unalazimishwa kuajiriwa na serikali? hakuna fedha wala mazingira bora

kama unaona vipi unasepa! simple as that.
 
Madaktari ni waajiriwa wa serikali na wana haki sawa na mwajiriwa yeyote kugoma- ILO principles.

Taratibu za ILO kuhusu migomo ni kuwa ama pande zote mbili zinazohusika lazima zikae pamoja na kukubaliana kumaliza mgomo huo au upande unaogoma unaweza kuamua kuacha mgomo. Upande unaogomewa hauwezi kumaliza mgomo kwa njia yoyote ile, ikiwamo vitisho.

Nitaendelea kuwaunga mkono madaktari wote mpaka tone la mwisho la damu yangu.
 
Mkuu PAMOKONUNDA, unasema madaktari walinde professional yao kwa kufanya "reasonable decision" na waachane na siasa! Hv ni mpaka lini watz tutaamuka toka usingizini na kuanza kudai haki yetu kwa pamoja na kuachana na haya maneno yako ya kupakana mafuta kwa mugongo wa chupa??!, huu sio muda wa porojo bali ni muda wa kuwajibika kwa kila mtu ktk nafasi yake na kwa wakati wake. In fact, as Tanzanians I think we've tested our patience enough!
 
Last edited by a moderator:
Intelijensia sijui kama itayaruhusu haya.. count me in

Mkuu hatuna kitu kama hiki nchini kwetu, bali kuna usalama wa mafisadi ambao watafanya juu chini kuhakikisha mafisadi hawapati bughudha ya aina yoyote ile ikiwemo watanzania kuandamana ili kuishinikiza Serikali DHAIFU ili waendelee kutanua kwa raha zao.
 
Sasa hawa Madaktari au Chadema, wapi na wapi maandamano ya Madaktari yanatangazwa na wafuasi wa Chadema, huu mgomo wa Madaktari ungekuwa nyuma ya Watanzania Madaktari wangefanikiwa lakini wameruhusu Chadema wateke mgomo wao.
hivi cdm ni ya zimbabwe?
 
Waende Iran wakafanye nini? wanajualia wapi operations madr wabongo? Unadhani kwanini watu wanaenda kutibiwa india, watu wanaenda India baada ya kushauriwa na hao hao madr wabongo kwamba hawawezi kazi hivyo wanamwabia mgonjwa mwenye uwezo au sometimes serikali inawafund wagonjwa kadhaa au misaada inatolewa watu wanaenda kutibwa nje.
Lazima mwenye byte 1 ya ubongo atafsiri rufaa za madaktari kwa namna yako.
 
Drs, acheni kuzungumza peke yenu, nivema mkaweka kila kitu wazi kupitia vyombo vya habari! Haiwezekani katika madai yenu zaidi ya 10 selikali ichomoke na dai 1 tu la mshahara na mengine isitake kuyazungumzia kabisa, wanalenga kuwachonganisha na raia weke kila jambo hadharani!
 
gud newz! Hope wanaharakati watawaunga mkono!

nimeongea na CCTV Africa ili waje kucover hii habari na irushwe world wide. Jamaa kaniambia hajuia kama mkurugenzi wao ambaye ni mchina kama ataunga mkono! kaniambia kama ingekuwa cairo, sauth africa au nigeria angeunga mkono lakini kwa sisi hana uhakika na huyo mkurugenzi.
 
Imeandikwa na Geofrey Nyang’oro

KITENDO cha Baraza la Madaktari Tanganyika (MCT), kusitisha usajili kwa baadhi ya madaktari waliokuwa kwenye mafunzo ya vitendo (Interns), kimekoleza moto wa mgomo wa madaktari baada ya wanataaluma hao kutangaza maandamano yatakayofanyika wakati wowote kuanzia sasa.

Kwa muda wa wiki tatu sasa, madaktari wamekuwa katika mgomo wakitaka kuboreshewa masilahi yao na huduma za afya hospitalini, lakini wanataaluma hao walionekana kuchukizwa zaidi baada ya tukio la kutekwa, kupigwa na kutelekezwa porini kwa Mwenyekiti wa Jumuiya ya Madaktari, Dk Steven Ulimboka huku rais wa Chama cha Madaktari (MAT), Dk Namala Mkopi akifunguliwa mashtaka ya kukiuka amri ya mahakama.

Jana, akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam, Katibu Mkuu wa MAT, Dk Rodrick Kabangila alitaja lengo la maandamano hayo kuwa ni kupinga dhuluma na uonevu dhidi ya taaluma ya udaktari na madaktari wenyewe.

Dk Kabangila alitaja sababu ya pili kwamba, ni kulaani kitendo alichofanyiwa Dk Ulimboka cha kutekwa, kupigwa, kuteswa na kutupwa katika msitu wa Pande nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam na sababu ya tatu ni kushinikiza Serikali kuunda Tume Huru ya kuchunguza suala hilo, ili wahusika wajulikane na kuchukuliwa hatua za kisheria.

Alisema pia kwamba hatua hiyo imekuja kutokana na kitendo cha Serikali kuendelea kuchukua hatua ya kuwafukuza madaktari na kusitishiwa leseni wale waliokuwa chini ya mafunzo, badala ya kusikiliza na kutatua madai yao yaliyolenga kuboresha huduma hiyo nchini.

“Kama mnavyofahamu, mpaka sasa takriban madaktari 400 walio chini ya usimamizi na wale walio kazini wamesitishiwa usajili na wengine kusimamishwa kazi, na haya yanaendelea wakati suala la msingi likiwa mahakamani na pia Tanzania ikiwa na upungufu mkubwa wa madaktari kwa daktari mmoja kuwa na uwiano wa kuhudumia wagonjwa 30,000,” alisema Dk Kabangila na kuongeza:

“MAT inasikitishwa na dhuluma hii inayoendelea dhidi ya taaluma ya udaktari na madaktari wenyewe na hivyo inapanga kuitisha mkutano mkubwa kesho (leo) na inatangaza maandamano ya amani ya madaktari na wale wote wenye mapenzi mema na taaluma hii na sekta ya afya kwa ujumla.”

Dk Kabangila aliongeza kuwa, maandamano hayo yatafuata taratibu zote za kisheria, ikiwa ni pamoja na kutoa taarifa polisi saa 48 kabla ya kuandamana na madaktari wote watavaa makoti meupe na wasio madaktari watatakiwa kuwa na vitambaa vyeupe.

Alisema maandamano hayo ya amani yataanzia katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) hadi Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, ambako watakabidhi madai yao serikalini.

“Tunajua tunachotakiwa kufanya ni kutoa taarifa kwa ajili ya kuhitaji ulinzi. Maandamano yetu ni ya amani na ndiyo sababu tutakuwa na makoti pamoja na vitambaa vyeupe kwa wasio madaktari,” alisisitiza.

Katika mkutano huo, Dk Kabangila alielezea kusikitishwa kwake na makundi ya watu mbalimbali na mtu mmoja, mmoja kuwatuhumu kuwa ni wauaji kwa kuendesha mgomo, akisema kitendo hicho ni hatari kwa kuwa kinawakatisha tamaa madaktari nchini.

“Yameibuka makundi yanayowatuhumu madaktari kupitia vyombo vya habari, wapo wanaosema madaktari ni wauaji, hii ni hatari. Madaktari wanafanya kazi ngumu na katika mazingira magumu, hawana vitendea kazi lakini badala ya kuwafariji, watu wanajitokeza na kuwasema vibaya, sijui nini malengo yao na hatima ya taaluma ya udaktari nchini,” alisema.

Alisema lengo la kushinikiza madai yao ni kutaka Serikali iweke mazingira mazuri
yatakayowezesha wanataaluma hao ambao Serikali hutumia fedha nyingi kuwasomesha, kufanya kazi nchini badala ya kukimbilia nje ya nchi.

Waliositishiwa usajili wanena
Kwa upande wao madaktari waliokuwa katika mafunzo ya vitendo (Interns) wamelaani kitendo cha kusitishiwa leseni zao wakidai ni cha uonevu.

Mwakilishi wa wanataaluma hao, Dk Frank Kagoro alilituhumu Baraza la Madaktari Tanganyika akisema limewahukumu bila
kuwasikiliza, kitendo ambacho kimewanyima haki ya kujitetea.

“Tumeshtakiwa kwa makosa yasiyo yetu, tumeambiwa tuwasilishe barua na tumefanya
hivyo. Zile barua ilikuwa geresha, mbona hawakutuita kutuhoji? Huu ni uonevu, hata makosa waliyotuhumu nayo si makosa yetu,” alisema Dk Kagoro.

Dk Kagoro alifafanua kuwa, katika barua za mashtaka kutoka Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii kwenda katika baraza hilo, madaktari hao walituhumiwa kuwa hawakutekeleza wajibu wao wa kutoa huduma kwa wagonjwa, hali iliyohatarisha maisha ya wagonjwa.

Akifafanua hilo, Dk Kagoro alisema tuhuma hizo siyo zao na kwamba wao wanafanya kazi chini ya madaktari bingwa, ambao wanapogoma moja kwa moja wanafunzi wanakosa kazi za kufanya.

“Sisi tunafanya kazi chini ya madaktari bingwa, wao wanapogoma na sisi moja kwa moja tunakuwa hatuna kazi za kufanya, tupo kwa ajili ya kujifunza, iweje leo tuambiwe sisi ndio tuliohatarisha maisha ya watu, tungefanyaje kazi bila maelekezo ya madaktari bingwa?” alihoji Dk Kagoro.

Alisema, baraza hilo limewachukulia hatua bila ya kuwasikiliza kutokana na kuwa chini ya Serikali kupitia Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, ambapo Mganga Mkuu wa Serikali ndiye mwenyekiti.

“Kama lingekuwa baraza huru la madaktari lingetusikiliza, lakini hawa wamechukua hatua bila ya kufanya hivyo, na hii ni kutokana na kutekeleza matakwa ya Serikali, ndiyo sababu tunatarajia kujadili namna ya kuwa na Baraza Huru la Madaktari Tanganyika,” alisema.

Kuhusu hatua ya kufukuzwa kazi madaktari na kusitishiwa leseni zao, alisema siyo tu inakiuka haki zao bali inahatarisha maisha ya Watanzania watakaokosa huduma za madaktari na pia kuliingizia hasara Taifa kutokana na kutumia fedha nyingi kugharimia elimu ya wanataaluma hao.

“Daktari mmoja hadi anafikia hatua hii anatumia zaidi ya Sh30 milioni kwa ajili ya kupata elimu, je, ni shilingi ngapi kwa madaktari zaidi ya 380? Haya ni mabilioni ya fedha za walipa kodi ambayo Serikali inapoteza kwa kuwafukuza madaktari,” alisema.
 
Tunaomba Serikali muwawache wandamane na mturuhusu wananchi twende tukawalambe bakora.

Maandamano yanini na wameshaambiwa kinaga ubaga asiyetaka aache kazi. Milango iko wazi. Wanaandamana nini? waondoke wakatafute kazi za kufanya hatuwataki tumeshachoka nao.
Ni wateule wachache tu humu JF tuliowaza hilo jamaa wengine wamekariri kwamba kila madr wanachosema inabidi kifanywe papo hapo bila kuzingatia mambo mengine.
 
Back
Top Bottom