Maandamano makubwa ya Madaktari yaja (wiki ijayo)

Molemo

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
14,534
13,225
Chama cha madaktari Tanzania-MAT kimeitisha maandamano makubwa dhidi ya serikali wiki Ijayo.Maandamano hayo yataanzia Hospitali ya Muhimbili mpaka wizara ya Afya.

Sababu kubwa ya maandamano ni kulaani tukio la kupigwa mwenyekiti wa jumuiya ya madaktari Stephen Ulimboka. Pili wanalaani kufutiwa usajili madaktari wanafunzi-Interns. Tatu wamesema madaktari bingwa wameanza kuacha kazi na wengine wanahangaika kutafuta kazi nje ya nchi.

Pia wamelaani kufunguliwa mashtaka kwa Rais wa MAT Namala Mkopi.Katibu Mkuu wa MAT amewaomba Watanzania wote wenye mapenzi mema kujitokeza kwa wingi siku ya. Maandamano ya madaktari ili kuwaunga mkono.

Source:CHANEL TEN
 
naisubiri interijensia itoe majibu juu ya haya maandamano lakini interijensia hii ina makengeza maana mambo mengine huwa haiyaoni wako wapi waliomteka dr Uli hadi leo haijawaona huu ndo umakengeza wa interijensia ya kova na mwema
 
Maandamano bila kuwashirikisha waataalamu wa maandamano (M4C) hawawezi kufanikiwa.
Nawashauri waresign wote then tuone serikali inafanyaje ila hili la maanadamano wataishia pale diamond jubilee na kutawanywa na askari washwawashwa (FFU)
 
Kesho watakuwa na kikao cha ndani kuanzia saa tatu.
J3 wata waalika waandishi wa habari kwenye maandamano yao.
Wanafadhaishwa sana na wanayo tendewa.
Mjadala wa kesho utafanyika kwa kirefu kujadili hatima ya sekta ya afya nchini kwa ujumla.
 
Haya maandamano hata kama yataongozwa na Ban Ki moon mwenyewe hayatafanyika! Chama kipya cha siasa kwa jina la Jeshi la polisi watatoa onyo kali.
 
Chama cha madaktari Tanzania-MAT kimeitisha maandamano makubwa dhidi ya serikali wiki Ijayo.Maandamano hayo yataanzia Hospitali ya Muhimbili mpaka wizara ya Afya.
Sababu kubwa ya maandamano ni kulaani tukio la kupigwa mwenyekiti wa jumuiya ya madaktari Stephen Ulimboka.Pili wanalaani kufutiwa usajili madaktari wanafunzi-Interns.Tatu wamesema madaktari bingwa wameanza kuacha kazi na wengine wanahangaika kutafuta kazi nje ya nchi.Pia wamelaani kufunguliwa mashtaka kwa Rais wa MAT Namala Mkopi.Katibu Mkuu wa MAT amewaomba Watanzania wote wenye mapenzi mema kujitokeza kwa wingi siku ya.maandamano ya madaktari ili kuwaunga mkono.

Source:CHANEL TEN
nawaunga mkono...
 
Maandamano bila kuwashirikisha waataalamu wa maandamano (M4C) hawawezi kufanikiwa.
Nawashauri waresign wote then tuone serikali inafanyaje ila hili la maanadamano wataishia pale diamond jubilee na kutawanywa na askari washwawashwa (FFU)
anal spincters are torn..tight them u idiot
 
Kova na makengeza yake, atuletee tena hadithi za 'intelejensia'...
 
Back
Top Bottom