Maandamano makubwa ya kumng'oa mbunge bandia wa SHY MJINI yaja. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Maandamano makubwa ya kumng'oa mbunge bandia wa SHY MJINI yaja.

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Jiwejeusi, May 9, 2011.

 1. Jiwejeusi

  Jiwejeusi JF-Expert Member

  #1
  May 9, 2011
  Joined: May 3, 2011
  Messages: 755
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Ndugu wanajf, kwa jina la demokrasia, utu, heshima na HAKI, mimi Jj, napenda kuwajulisha na kuwaomba misaada yenu ya hali na mali kuwa, ule wasaa wa kuandaa maandamano makubwa dhidi ya mbunge bandia wa shy mjini, sasa umewadia. Watu wa jimbo la shy mjini, wamevumilia kiasi cha kutosha kuisubiri haki ambayo matumaini yake yanapotea siku baada ya siku. Watu wa shy wanapenda amani, wanapenda endapo tu, HAKI na matakwa yao hayatapuuzwa. Kumpa masela ubunge bandia ni kupuuza haki na matakwa ya watu wa shy mjini, kwa hilo hawalikubali. Kwa niaba ya watu wa shy, natoa wito kwa watu wote wapenda haki na demokrasia kutuunga mkono katika maandamano yatakayokuwa na jina MASELE ONDOKA, HUKUSHINDA, SISI TUNAPENDA HAKI. Tumeamua kufanya hivyo baada ya kutafakari misingi ya kisheria na kujiridhisha kwamba haki ambayo aliipigania mbunge wetu, marehemu SHELEMBI, hatutaipata. Tunawaomba watz wote watupe ushirikiano. Asanteni.
   
 2. MAYOO

  MAYOO JF-Expert Member

  #2
  May 9, 2011
  Joined: Feb 14, 2011
  Messages: 200
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 35
  Heko mkuu, kila la heri.
   
 3. d

  daniel.nickson Member

  #3
  May 9, 2011
  Joined: Apr 30, 2011
  Messages: 33
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  pamoja na kukuunga mkono, ninaomba mungu atupe hekima na maarifa ya kufanikisha hili kwa muda mfupi ili tupate muda wa kushughulikia mambo mengine yanayohusu nchi yetu iliyowekwa rehani kwa wageni na baadhi ya wenzetu wasiokuwa na utu hata asilimia moja.
   
 4. TUNTEMEKE

  TUNTEMEKE JF-Expert Member

  #4
  May 9, 2011
  Joined: Jun 15, 2009
  Messages: 4,582
  Likes Received: 55
  Trophy Points: 145
  Ni kweli naamini masele au hata wapambe wake , hata akina Ridhiwan na Bashe waliomtuma aje kugombea halafu akashindwa vibaya naamini mmoja wenu yumo humu kwa kweli huyo ndugu mimi kama mwanashinyanga hatumhitaji , ni heri tusiwe na muwakilishi kuliko kuwa na muwakilishi ambaye siyo chaguo letu.
  Pia wewe Masele kama wewe ni mzalendo, tena naamini ni mzalendo maana nakufahamu vizuri ila najuwa unaogopa kujiuzulu ubunge kwa sababu ya madeni makubwa unayodaiwa ila kwa kinywa chako uliwahi kuniambia huna raha na huu ubunge wako maana hata kanisani ulipokuja shy ulikuwa unasindikizwa na polisi, sasa huo ni wa nini,
  Ombi langu kila mtu ameona ni mengi tu ambayo Makamba aliwadanganya wewe ukiwemo kuwa komaa tu baada ya miezi miwili au mwezi wananchi watasahau, watanzania wa leo siyo wale wa enzi za Makamba na kingunge, ndiyo maana mwenzio Kaijage yameanza kumtokea puani, Sarakana Kafuta kesi, Masumbuko Lamwai anambembeleza Marando amuombee msamaha kwa watanzania ili naye aje CDM, maana hivi hivi si CHADEMA tu hata wananchi wengine hawatamuelewa, pia mwakyembe kapigwa mawe kwao na kuzomewa, sasa ndugu yangu Masele wewe ni Kijana mwenzangu aliyekudanganya uchukue ubunge kwa mabavu ameonekana ndani ya Chma chenu ni Gamba na ameenda kuwaandalia makao, Ridhwani mwenzio ni Billionaire na kesho Limtikila linampeleka mahakamani kama yeye hataenda maana 7dayz alizotoa zinaisha leo, kwanini na wewe usiache tu huo ubunge usio na faidi kwako na familia yako
  Historia itawahukumu haa wanao kuwa baba yenu aliongoza kwa mabavu SHY mjini bila RIDHAA YA WANACHI, utaharibu hata future ya kizazi chako maana wa Tanzania wa leo siyo wa kesho
  Na labda tu kwa kukukumbusha kuna shujaa wetu mmoja anaandika kitabu kuhusu yote yalijojiri kwenye kampeni za ubunge , matokeo ya kila kituo anayo na jinsi wewe,. rpc, mkuu wa mkoa na mkurugenzi mlivyobadilisha matokeo hicho kitabu very soon kitakatoka na kitakuwa na title "Uchakachuaji wa matokeo shinyanga mjini, Bogus alizawadiwa ushindi na mabogus wenzie", sasa hicho kitabu kitabaki kuwa ni kumbukumbu hata kwa wanao na wajukuu zako
  Taarifa tunazo kuwa mara tu baada ya kifo cha shelembi ulimlipa hata mwanasheria wako na ulifanya party kwamab yamekwisha ulijidanganya , ngoma bado mbichi, tumeshindwa kukutoa kwa sheria tutakutoa kwa mbinu tunayoijua sisi na moja wapo ni maandamano kuwa hatukutaki
   
 5. Gurudumu

  Gurudumu JF-Expert Member

  #5
  May 9, 2011
  Joined: Feb 5, 2008
  Messages: 2,350
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Kumbe Tunisia na Misri inaweza kuanzia majimboni ee? Chapa mwendo vijana, tuko nyuma yenu.

  Kama hatarudi jimboni mtampinduaje? Mkiandamana asipoondoka mtamuondoaje?
   
 6. j

  jnuswe JF-Expert Member

  #6
  May 9, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 1,271
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  hoja ya kuwataka viongozi wake hasa mawaziri na makatibu kutokaa ofisini muda wote badala yake wafike kwa wanainch ili kuweza kujua yale yanayofanyika na kusimamia utekelezaji wa shughuli. Wasiwasi wangu mimi ni kwamba pengine Mh. hawajui vizuri viongozi wake aliowachagua kumsaidia.

  Viongozi wenye ujasiri wa kufanya hivyo alionao ni wachache pengine 20%, asilimia inayobaki wataendeje huko wakati hata wanachokisimamia hawakijui ? kiongozi kama Magufuli na wengine wachache wanaweza kwa sababu majukumu na wajibu wao wanaujua.

  viongozi alionao si ajabu wakaenda kwa wanainch, wapiga kura wakawa ndio wa kuwaelimisha juu ya shughuli zilizo ndani ya Wizara zao, Mh. anaposema waseme yale mazuri yanayofanywa na serikali wasiwachie wapinzani kuchukua nafasi na kuendelea kupotosha umma hilo haliwezi kuwa sahihi sana, kwani viongozi wachache alionao wachapa kazi mbona wamesimama hadharani wakaeleza yanayofanywa na wizara zao.

  Hao ambao hawawezi kusema mazuri yanayofanywa na serikali inamanisha hayapo. Kuendelea kuwalazimisha hao waseme ambayo hayapo ni kutaka waendelee kutudanganya.
   
 7. j

  jnuswe JF-Expert Member

  #7
  May 9, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 1,271
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  hoja ya kuwataka viongozi wake hasa mawaziri na makatibu kutokaa ofisini muda wote badala yake wafike kwa wanainch ili kuweza kujua yale yanayofanyika na kusimamia utekelezaji wa shughuli. Wasiwasi wangu mimi ni kwamba pengine Mh. hawajui vizuri viongozi wake aliowachagua kumsaidia.

  Viongozi wenye ujasiri wa kufanya hivyo alionao ni wachache pengine 20%, asilimia inayobaki wataendeje huko wakati hata wanachokisimamia hawakijui ? kiongozi kama Magufuli na wengine wachache wanaweza kwa sababu majukumu na wajibu wao wanaujua.

  Hao viongozi alionao si ajabu wakaenda kwa wanainch, wapiga kura wakawa ndio wa kuwaelimisha juu ya shughuli zilizo ndani ya Wizara zao, Mh. anaposema waseme yale mazuri yanayofanywa na serikali wasiwachie wapinzani kuchukua nafasi na kuendelea kupotosha umma hilo haliwezi kuwa sahihi sana, kwani viongozi wachache alionao wachapa kazi mbona wamesimama hadharani wakaeleza yanayofanywa na wizara zao.

  Hao ambao hawawezi kusema mazuri yanayofanywa na serikali inamanisha hayapo. Kuendelea kuwalazimisha hao waseme ambayo hayapo ni kutaka waendelee kutudanganya.
   
 8. POMPO

  POMPO JF-Expert Member

  #8
  May 9, 2011
  Joined: Mar 12, 2011
  Messages: 6,694
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  Fukuza huyooooooooooo anyway Masele sijui kabailisha na number maan kila wakati not rechable,
  Tutakupata...ananenepeana kama nguruwe ok watu wangu wa Shy Town tupo pamoja
   
 9. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #9
  May 9, 2011
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  Hili likiwezekana, basi mageuzi yatakua yametimia!!!
   
 10. POMPO

  POMPO JF-Expert Member

  #10
  May 9, 2011
  Joined: Mar 12, 2011
  Messages: 6,694
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  [​IMG]
  Wanted in Shy
   
Loading...