Maandamano makubwa ya kudai maji na umeme kutoka kwa barrick buzwagi mjini kahama

TUNTEMEKE

JF-Expert Member
Jun 15, 2009
4,587
579
Wadau kwa mjibu wa radio kahama inayomilkiwa na mbunge wa kahama ccM ndugu Lembeli imetangaza kuwa kesho kutakuwa na maandamano ya kudai maji na umeme katika kijiji cha mwendakulima km 0.2 kutoka mgodi wa dhahbu wa buzwagi .
Maandamano hayo yameratibiwa na wanharakati mbalimbali wa maendeleo na wapinga ufisadi ambapo yatapokelewa na mbunge mwenyewe , yatapitia njia gani sijui nitaendele kuwapa taarif kadri nitakavyokuwa nazipata
nawasilisha
source; radio kahama fm

Sasa ni wakati wa wanaKahama kudai haki yao kwani naona serikali inashirikiana na hao Barrick kuwaibia. WanaKahama tupo pamoja kabisa katika hili. Tunahitaji maji, umeme, barabara bora, shule nzuri zenye walimu na vifaa, hosipitali zenye vifaa katika mji wa Kahama na vijiji vinavyozunguka huo mji. Jitokezeni wanaKahama na huu uwe ndo mwanzo wa kudai haki zetu.

Wadau kwa mjibu wa radio kahama inayomilkiwa na mbunge wa kahama ccM ndugu Lembeli imetangaza kuwa kesho kutakuwa na maandamano ya kudai maji na umeme katika kijiji cha mwendakulima km 0.2 kutoka mgodi wa dhahbu wa buzwagi .

Maandamano hayo yameratibiwa na wanharakati mbalimbali wa maendeleo na wapinga ufisadi ambapo yatapokelewa na mbunge mwenyewe , yatapitia njia gani sijui nitaendele kuwapa taarif kadri nitakavyokuwa nazipata

nawasilisha

source; radio kahama fm

aliyetangaza ni Digital Kongo (BARAKA MKASIWA)? Maana ni kada wa Magamba anayeponda CDM

Kazaneni ila huyo mbunge ameshapoteza sifa na atatolewa kwenye kura za maoni na magamba,subirini tuone.

Mnamdai muwekezaji maji badala ya selikali????!........selikali inatakiwa kubeba jukumu hilo kupitia kodi inayolipwa na mgodi husika!.

Buzwagi wenyewe wanatumia grid ya taifa...na wao hawana umeme maeneo ya vyumbani wakati wote wa mchana...kule kwenye plant ndio kuna umeme wa generator.

Kumbukeni wakati mgodi wa buzwagi unajengwa...serikali iliahidi kuwapatia umeme full hilo wameshidwa..ambapo mgodi ulibidi kununua gerator zake..kwa ajiri ya production..Jeez Hii nchi.

Wa Buzwagi wanatumia maji kutoka wapi? Wana visima vyao? Hongereni wanaKahama. Daini haki zenu vinginevyo mtakufa maskini.

Wa Buzwagi wanatumia maji kutoka wapi? Wana visima vyao? Hongereni wanaKahama. Daini haki zenu vinginevyo mtakufa maskini.

Ndugu yangu yaani maisha ya pale (Mwendakulima)kijiji kilicho hatua chache kabisa kutoka geti kuu la mgodi ni mateso makubwa.Maji ya bomba kwao ni hadidhi,wanatumia maji ya visima na kwakweli ni maji yasiyo salama kabisa.

Mimi binafsi nimekaa pale kwa wiki kadhaa lakini nimeshindwa kabisi kuimudu kasi ya mdororo wa maendeleo wa kijiji kile ambacho kama unawasha njiti ya kiberiti kutoka geti la mgodi unaufikisha moto ng'ambo ya pili kabla njiti haijazimika.So utaona ni jinsi gani raia wa pande hizo walivyo na kila haki ya kuhakikisha mgodi uliozunguka vijiji vyao wanalazimisha sio kuomba ili wapatiwe huduma za jamii zinazotakikana katika maeneo yao.Nawaunga mkono kwa % zote.

0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom