Chaliifrancisco
JF-Expert Member
- Jan 17, 2015
- 23,489
- 70,277
Maandamano makubwa yanatarajiwa kufanyika nchini Venezuela baadae hii leo katika harakati za kumataka raisi wa nchi hiyo Nicolas Maduro kujiuzulu. Harakati hizo zinachochewa na Juan Guaido ambaye wiki iliyopita alijitangaza kuwa ndie kiongozi halali wa nchi hiyo.
January 23 takribani watu millioni moja waliandamana mitaani nchini Venezuela, kuitikia wito wa Juan Guaido, wakimtaka raisi Maduro ajiuzulu.
Guaidó anaungwa mkono na mataifa mengi ya Latin America, Marekani na Ulaya. Maandamano ya leo February 2 yanatarajiwa kuwa makubwa zaidi kuliko yale ya January 23.
Raisi Maduro kwa upande wake anaungwa mkono na jeshi la nchi hiyo pamoja na Urusi, China na Uturuki na mpaka sasa inapoandikwa makala hii bado yupo madarakani.
Inakadiriwa kuwa asilimia zaidi ya 80 ya wananchi hawamuungi mkono raisi huyo na wanamtaka ajiuzulu. Nchi jirani nazo zimeathirika kutokana na hali mbaya nchini Venezuela ambapo inakadiriwa watu zaidi ya million tatu wameikimbia nchi hiyo kutokana na hali mbaya ya kiuchumi na kijamii iliyoikumba nchi hiyo toka enzi za utawala wa Hugo Chávez.
Mataifa ya Ulaya na Marekani kwa upande wao wanaathirika na hali ilivyo Venezuela kutokana na kushindwa kuthibiti uzalishaji wa dawa za kulevya kutokana na rushwa iliyokithiri.
As world leaders pile in for Mr Maduro or against him, they are battling over an important idea which has lately fallen out of favour: that when a leader pillages his state, oppresses his people and subverts the rule of law, it is everybody’s business.
My take
Utawala wa kimabavu na uonevu hautaweza kulifikisha taifa lolote sehemu salama hasa katika zama hizi. Mwenye masikio na asikie na mwenye macho haambiwi tazama.
https://edition-m.cnn.com/2019/02/01/americas/venezuela-guaido-maduro/index.html?r=https://www.google.com/
The battle for Venezuela’s future
Credit: The Economist
CNN