Maandamano makubwa kupinga ujio wa Dk Slaa Kigoma Mjini

Mkuu Feedback hakika nakuambia timing ya Dr. Slaa kwenda Kigoma ni mbaya na kama nyinyi ndio mmemshauri basi ushauri wenu pia ni mbaya. Mimi si mtu wa Kigoma ila nafahamu jinsi Zitto anavyokubalika Kigoma na nyinyi hilo mnalifahamu kabisa. Sasa mnamvua vyeo halafu mwende kuwaambia watu wa Kigoma kwamba mwanenu mshenzi tumemvua vyeo vyote kwenye chama chetu na tunataka kumfukuza? Siamini kama wanakigoma watawaelewa. Busara inaonyesha kwamba Dr. Slaa angesubiri vumbi litulie ndio aende huko. Kwa sasa ni kama kwenda tu kuwadhihaki wana Kigoma na matokeo yake ndio hayo. Tuvumilie tu


Anadhani Waha ni misukule! Basi ajue hakuna watu wabishi na wanaojua kulipa kisasi kama waha! Atakoma kulinga! Shida sio kuimarisha chama,bali kumalizia hela za ruzuku kwa kujilipa night za safari na mambo kibaao ili hesabo ipigwe dabo! Wakilamba ruzuku na hapo hapo deni la safari ya Kigoma linafanywa mara 2 au 3 ! Hao ndio wanye saccos ya Chadema!
 
Last edited by a moderator:
Hakuna tatizo kama maandamano yenyewe yamepata baraka (kibali) kutoka mamlaka zinazolinda usalama (polisi), na pia waandamanaji wasivunje sheria. Kuandamana ni haki yao! Hata hivyo CHADEMA wanatakiwa kupokea maandamano hayo na kuwasikiliza!

Umenena vema sana ndugu.
 
Nipo hapa mwanga naona gari linapita likitangaza Maandamano ya kupinga ujio wa Dk Slaa mjini kigoma, Maandamano hayo yataanzia mwandiga hadi viwanja vya community center ambapo ndipo Dk Slaa anategemea kufanya mkutano wa hadhara kesho, Maandamano yatafanyika tarehe 8.12.2013 kesho jumapili. Maandamano yataanza saa 2 asubuhi. Gari kwa sasa limeelekea maaneo ya ujiji.

Dr amevulugwa aiseee
 
Naona nyumba ya majani hapo ndio wanadanganywa na rafiki yao zitto

Nyie mtamlaumu kila mtu! Mara Zito, mara ccm, mara masalia! Kiukweli sisi waafrika siasa za kweli za ushindani wa kidemokrasia wengi hatuwezi! Msitafute mchawi! Fanyeni demokrasia ya ukweli na sio kulaumu kila mtu!
 
vijana hao walioandamana wote wapewa pesa za kiroba na maccm wanafiki wakubwa wanafikiri zitto yupo juu ya katiba akili za kukuu
 
Mimi sielewi kitu hapa, kama hao wanaoandamana ni wafuasi wa CCM ni kweli kuwa POLISI wa Tanzania wamefikia kiwango cha kuwakamata wafuasi wa CCM? Kweli POLICCM hawahawa ninaowajua leo hii wametenda haya?


Halafu msitufanye wajinga jamani, kwani nani hajui kuwa nguvu ya CDM mkoa wa KIGOMA inatokana na Zitto?
 
Angekuwa anakubalika basi Tanzania nzima wangeandamana but kwa vile ni kigoma tu hii inaonyesha jinsi hawa watu walivyo wabinafsi na wanafiki,mbona hawajaandamana kupinga adhabu za wengine,nadhani yote ni kwa sababu kupitia zzk basi waliamini kigoma itatoa raisi na kumbe sasa matarajio yao yamekatizwa na hiyo adhabu!
Nyie waha badirikeni na muache ubinafsi na unafiki!

Ha! Look who is talking! Ubinafsi! Ubinafsi! Leo ndio unaliona hilo! Chama kimeshikwa na wabinafsi wafuatao.
1. Mbowe- Hataki kuachia uenyekiti!.
2.Mtei- Hataki chama kishikwe na mtu nje ya familia.
3.Slaa-Hataki mtu ahoji ruzuku wala safari zake na hawala yake zinagharamiwa na nani!
1.Lema- Hamtaki Zito anataka viongozi kutoka kaskazini na vibaraka wao, eg Lisu, Msigwa n.k! Acha ujinga wewe usidhani hatuoni!
 
uko sahihi kabisa mkuu hata cc watu wa kg tushamchoka

Sasa baada ya hili saga asubiri mrejesho kwenye siasa, itakuwa bora lusinde a.ka kibajaji ama nkamia au nani yule mkigoma aliyesema bungeni neno(tusi) jina linafanana sana na jina la waasi wa faki...nani ...nani...vileee.....niiiii ahaaa anaitwa serukamba
 
vijana hao walioandamana wote wapewa pesa za kiroba na maccm wanafiki wakubwa wanafikiri zitto yupo juu ya katiba akili za kukuu

Usitokwe povu! Kamanda mwabie kibabu kile kimrudishie zito nyadhifa zake na kimwombe radhi mara moja, tena hadharani,or else!.......!
 
Mimi sielewi kitu hapa, kama hao wanaoandamana ni wafuasi wa CCM ni kweli kuwa POLISI wa Tanzania wamefikia kiwango cha kuwakamata wafuasi wa CCM? Kweli POLICCM hawahawa ninaowajua leo hii wametenda haya?


Halafu msitufanye wajinga jamani, kwani nani hajui kuwa nguvu ya CDM mkoa wa KIGOMA inatokana na Zitto?

utaelewaje km Kigoma ni ngome ya NCCR tayari...na si ahta ya Zitto....Hii game ni ngumu sana kwa polisi .Tatizo ni kwamba hakuna nafasi ya kuigiza.Ukiigiza unawashika ndio umewashika.Na ukiwaacha wengine wajenge scene kwanza dr. anawakaribisha.


WELL, KWA KIFUPI NI KWAMBA POLISI WANAWASHIKA ILI KUWALINDA WASIPOKEE KICHAPO KIBAYA TOKA KWA REDBRIGADE.....KWANI SOWETO WALIPIGWA RISASI NANI?POLISI WANAJUA WAKIWAACHA BAADAYE WATAJIBU KWA CCM CDM WAKIWAPOTEZA.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom