Maandamano kumuunga mkono Makamu wa Rais, Mama Samia Suluhu

Hivi nyie bavichaa huwa mnafurahia nini kukonect dot??? Yani sijaona ambapo Mh. Samia akisema watoto wajawazito warudi shule baada ya kujifungua...
 


Wadau napendekeza maandamano kote nchini kwa wale wanaokubaliana na kauli ya makamu wa Rais kuwa watoto hawapaswi kuhukumiwa kwa kubakwa bali wale waliofanya unyama huo!
Tumuunge mkono kwa kutaka watoto hawa wapewe nafasi ya kupata elimu!Maneno hayo aliongea kwa uchungu mkubwa kama umemsikia hapo juu kwenye video!

Haya yatakuwa maandamano ya amani ya kumuunga mkono so tuna imani hatutapata usumbufu wowote!
Karibuni wadau tujadili namna ya kufanya maandamani haya!Akina mama tunawategemea sana kujitokeza!

Utakamatwa kwa ujinga wako
 
Hii nchi kila siku ni "Contradictions" tu. Huyu anasema mambo ya mitandao sifuatilii, huyu anamkamata mtu kwa makosa ya mtandao. Huyu anasema hatuwezi kukubali watoto wetu wakike wakose elimu kwa kuzaa, huyu anasema ukizaa nisikuone kwenye shuleni zangu. Mpango wa serikali unasema ifikapo 2025 tuwe na wananchi wote wamama kwa wababa walioelimika, huyu anasema siwasomeshi wamama. Huyu anasema Mtaisoma namba, huyohuyo anasema mimi nipo kwa ajili yenu. Huyu anasema mimi ni wa wote bila kujali itikadi ya siasa, huyo huyo anasema kwenye serikali yangu hakanyagi mguu mtu ambaye si wa chama changu, hata kwenda kumjulia hali asiye wa chama chetu ni marufuku. Huyu anasema natengeneza nchi ya viwanda na ya uchumi wa kati, mwingine anasema ukiwa na cherahani tu ndio nchi ya viwanda hiyo. Huyu anasema haikubaliki kwa mtumishi yeyote wa umma kuwa na cheti feki, mwingine anasema vyeti feki haviwahusu wakuu wa mikoa, wilaya, wabunge, madiwani na mawaziri. Huyu anasema ni marufuku kuuza mazao nje ya nchi, huyu anasema hakuna kumpangia mkulima wapi auze mazao yake kwa sababu anapolima wewe hukumsaidia sasa kwa nini umpangie pa kuuza, ni soko huria. Huyu anasema msiba ni wa sisi wote bila kujali siasa zetu, huyo huyo anawakamata wasio wa chama chake wanaoenda msibani. Hawa wanasema sheria hizi za madini ni nzuri na hao wanaopinga hawawatakii mema watanzania, wanataka kufukuza wawekezaji, hao hao tena wanasema hizi sheri za madini ni wizi mtupu, hatukubali na wanaandaa na maandamano ya kujipongeza kwa kutetea maslahi ya nchi kwa kupinga sheria za madini zinazotunyonya, zilezile sheria walizozipitisha kwa ndiyooooooooo!Jamani!
 
Nchi hii bwana..

Waziri anasema hili jukwaani, makamu anasema lile jukwaani na rais naye anakuja kusema lake la tofauti kabisaa!

Ili kulinda heshima yako, mtu wa juu yako anapokuja kupinga kitu ulichokisema hadharani kabisa inakubidi uachie ngazi tu!
 
Maandamano yanayoruhusiwa nchi hii bila hata kibali cha polisi ni ya kumsifu mkulu tu
Ukiwa na kibango chako cha "sizonje miaka mia, utawale milele" unaandamana hata kwenye barabara za mwendo kasi!
 
Halafu iweje, itifaki ya nchi imetamka no, hata azimio la arusha, kambona alikimbia nchi, usilete uchonganishi, mama Samia alitoa maoni yake haikuwa agizo au sheria
Ilani ya CCM inasemaje khs wanafunzi waliopata mimba?
 


Wadau napendekeza maandamano kote nchini kwa wale wanaokubaliana na kauli ya makamu wa Rais kuwa watoto hawapaswi kuhukumiwa kwa kubakwa bali wale waliofanya unyama huo!
Tumuunge mkono kwa kutaka watoto hawa wapewe nafasi ya kupata elimu!Maneno hayo aliongea kwa uchungu mkubwa kama umemsikia hapo juu kwenye video!

Haya yatakuwa maandamano ya amani ya kumuunga mkono so tuna imani hatutapata usumbufu wowote!
Karibuni wadau tujadili namna ya kufanya maandamani haya!Akina mama tunawategemea sana kujitokeza!

Kumuunga mkono mama suluhu ni kuhalalisha na kuendekeza Ngono Zembe za utotoni. Watoto /wanafunzi wa Sec na msingi wanatakiwa kukaa mbali na Vishawishi Ngono kwa kuwaarifu Wazazi wao wanapochokozwa. Wasipoarifu Wazazi na kuamua kujihusisha adhabu yao ni Mimba na kusitishwa masomo ya shule za Serikali. Yaani Rais anataka wanafunzi wazingatie nafasi ya Masomo waliopata kwa dhati na bidii. Nadhani kauli ya Mhe Rais itawazibua wengi fahamu na utambuzi wa wajibu wao.
 
Njia bora ya kumuunga mkono ni kuwapa vijana mashababi mabinti zenu wa shule za msingi na sekondari wawaingilie kingono, wapate ujauzito halafu muwapeleke shule. Hapo mtakuwa mmeunga mkono kauli zake kwa vitendo. Vijana wa kufanya kazi hiyo mkiwahitaji ni PM
 
Maandamano yanategemea ni nani ameshika remote maana sisi waandamanaji tulio wengi ni kama robots mkuu!
 
Back
Top Bottom