Maandamano kudhibitiwa

Mzee Uchwara

Senior Member
Oct 28, 2013
119
35
Kamati ya bunge ya ulinzi na usalama imeitaka serikari kutunga sheria ya kudhibiti maandamano yasiyo na tija. Ni kweli lazima kudhibiti maandamano,kwa sababu sasa hivi mbunge analeta fujo bungeni akidhibitiwa na wanausalama anasema ataandaa maandamanao, kila kukicha maandamano. Safi sana kamati.
 
Mbali ya makaburu wa Afrika kusini, sheria za aina hii hazikumsaidia Gaddafi, hazikumsaidia Saddam wala madikteta wengine wa sasa
 
Safi sana, tumechoka kuona damu ya watz wasio na hatia ikimwagika bila sababu ya msingi
 
Safi sana, tumechoka kuona damu ya watz wasio na hatia ikimwagika bila sababu ya msingi

Maandamano na kumwagika damu vina uhusiano gani ?

...au wewe pia ulihusika kuandaa dili la umwagaji damu kwenye maandamano ili yaonekane hayafai.

Maana ndio madili yenu siku hizi wkt wenzenu wanafanya madili ya kujenga reli
 
Kule Misri Sheria hii ipo lakini Maandamano yanafanyika takribani kila siku, Unataka kusema hawa wananchi wa Misri hawaijui hio sheria?
 
Kamati ya bunge ya ulinzi ni mzigo kwa wananchi

Sent from my BlackBerry 9780 using JamiiForums
 
Kule Misri Sheria hii ipo lakini Maandamano yanafanyika takribani kila siku, Unataka kusema hawa wananchi wa Misri hawaijui hio sheria?
Ni sheria inayotumika na serikali za kidikteta zinazowaogopa wananchi wake.
 
Mbali ya makaburu wa Afrika kusini, sheria za aina hii hazikumsaidia Gaddafi, hazikumsaidia Saddam wala madikteta wengine wa sasa
mkuu labda nikuulize hizo nchi kama zina amani tangu hao uliowataja waondolewe madarakani na kuuliwa kikatili. kwa kifupi waliowaondoa hao sio wananchi bali ni nchi za magharibi kupitia mgongo wa vibaraka wao. ndo maana mpaka leo nchi hizo hazina amani na watu wanakufa kama kuku. au wewe ndo furaha yako na ndo maana unatolea mfano wa nchi hizo? think!
 
Kule Misri Sheria hii ipo lakini Maandamano yanafanyika takribani kila siku, Unataka kusema hawa wananchi wa Misri hawaijui hio sheria?

Tofauti ya misri na Tanzania ni kuwa misri hakukuwa na uhuru wa kutoa mawazo lakini Tanzania leo hii watu wanawezi kumdhihaki mkuu wa nchi lakini usichukuriwe hatua.lakini hakuna uhuru huo misri. kama hicho. Tatizo letu huku tunatumia vibaya uhuru mfano kila kukicha watu wanaandaa maandamo yasiyo na tija. Misri maandamano yamekatazwa huku hayajakatazwa ila tunataka kuwe na sheria ya kudhibti maandamano yenye tija.
 
Safi sana, tumechoka kuona damu ya watz wasio na hatia ikimwagika bila sababu ya msingi
Yani wewe ni ifweero kabisa !
... kama jina lako.
Huna hata upeo wa kujua kuwa nchi zote duniani zilikombolewa kupitia maandamano.
Na mkoloni mweusi ni mbaya zaidi, we hujui.
... ifweeeero kbs ww
 
Mbali ya makaburu wa Afrika kusini, sheria za aina hii hazikumsaidia Gaddafi, hazikumsaidia Saddam wala madikteta wengine wa sasa

wale kina gadafi na wenzake waliminya uhuru, ulikuwa huna uwezo wa kukosoa, lakini tanzania uhuru huo upo wa kukosoa leo hii watu wanaweza kusema kuna mawaziri mzigo au kutaja vigogo wala rushwa. Lakini libya haikuwa hivo. Sisi tunataka maandamano lakini sio kila siku. Lazima kuwe na utaratibu maalumu.
 
Binafsi sidhani kama kufanya hvyo kutazidi kuboresha maisha yetu zaidi ya kuleta chuki na hisia za kuoneana miongoni mwetu na ni nani ambaye atakuwa na jukumu la kutambua kwamba maandamano yapi yenye tija na yapi hayana tija tuko na mambo mengi ya kufikiria kama taifa zaidi ya hili sina hakika kama kuna uhusiano wa upatikanaji wa madawa, maji safi na salama hapa kijijini kwetu licha ya kuwa mita chache karibu na ziwa na maandamano.
 
Back
Top Bottom