Maandamano/fujo zinazoendelea Zimbabwe ni nini chanzo

At Calvary

JF-Expert Member
Aug 22, 2018
4,513
3,552
Habari wakuu.

Tafadhali naomba kufahamishwa moja mbili tatu kuhusiana na hio mambo.

IMG_20200804_152117.jpg

-----

Rais wa Zimbabwe Emmerson Mnangagwa ameshutumu vyama vya upinzani, na nchi za kigeni kwa kutekeleza vitendo vya uchokozi dhidi ya nchi yake huku makundi ya watetezi wa haki za binadamu wakisema polisi na wamajeshi wameendelea kuwakamata wakosoaji mbalimbali.

Picha za vikosi vya usalama vikiwapiga raia zimesababisha ghadhabu miongoni mwa raia na wito wa chama cha upinzani cha AN nchini Afrika Kusini kutaka kufungwa kwa ubalozi wa Zimbabwe nchini humo mpaka pale haki za binadamu zitakapofuatwa.

Mnangagwa ameapa kupambana vikali na wapinzani na wanaharakati wa haki za binadamu baada ya kuongezeka kwa maandamano ya kupinga vitendo vya rushwa na kutoridhishwa na namna hali ya uchumi inavyoshughulikiwa nchini humo.

Uchumi wa Zimbabwe umeporomoka, serikali ikinyooshea kidole vitendo vya unyonyaji wa kiuchumi na vikwazo vilivyowekwa na nchi za magharibi. Hashtag ya Zimbabweanlivesmatter ni kampeni iliyo maarufu duniani kote wakati huu.

Akitoa hotuba kwa njia ya Televisheni siku ya Jumanne, Bwana Mnangagwa alikemea kile alichokiita '' mipango ya uharibifu ya makundi ya kigaidi ya upinzani''.

''Wale wanaochochea chuki na kuvunja umoja hawatashinda. Watu ambao wamejaribu kuwagawana watu wetu na kudhoofisha mifumo yetu watashughulikiwa,'' alisema.

Wapinzani na wanaharakati juma lililopita liliitisha maandamano dhidi ya serikali, lakini taasisi za kiulinzi ziliwataka wat kusalia majumbani mwao.

Wanasheria wa wanaharakati wa haki za binaadamu wamesema zaidi ya watu 60 wamekamatwa.

Mnangagwa katika hotuba yake amesema ''vikosi vya usalama vitaendelea kutekeleza majukumu yao''.

Sera ya mkono wa chuma dhidi ya wanaharakati wa upinzani

Robert Mugabe alipoondolewa madarakani kwa mapinduzi ya mwaka 2017, watu wengi nchini humo walikuwa na matumaini ya kuwa ni mwisho wa ukandamizaji na uongozi mbaya uliokuwepo kwa miaka 37 alipokuwa madarakani.

Mnangagwa aliingia madarakani akiwa ametoa ahadi ya kufanya mabadiliko lakini wakosoaji wake wamekuwa wakimhusisha na matendo yale yale yaliyoeleza sifa ya Mugabe: utawala wa mabavu, matumizi mabaya ya fedha, kutetereka kwa uchumi na hali ya maisha..

Mnangagwa, 77, ambaye alitegemewa kuwa kiongozi ambaye angekuwa wa tofauti na kiongozi aliyemtangulia, wanaharakati wanamuona kuwa ni rais mkali zaidi kuliko hayati Mugabe.

Kwa mujibu wa New York Times, idadi ya wanaharakati wa upinzani walioshtakiwa kwa vitendo vya uhaini wakati wa utawala wa miaka mitatu wa Mnangagwa ni idadi kubwa kuliko ilivyokuwa kipindi cha Mugabe chote cha kuwepo madarakani, kwa mujibu wa utafiti wa muungano wa mashirika 22 ya wanaharakati wa Zimbabwe.

Wanaharakati wapinzani walikuwa na matumaini ya kufanya mkutano Ijumaa juma lililopita, kupinga miongoni mwa mengine wimbi la vitendo vya ukamataji na utekaji nyara mwezi Mei, pale wanaharakati wanawake watatu, akiwemo Mbunge, walitekwa, kupigwa na kudhalilishwa kingono na watu waliodaiwa kuwa mawakala wa serikali, shutuma ambazo serikali ilikana kuhusika nazo na baada ya kuruhusiwa kutoka hospitalini wanawake hao walishtakiwa kwa kutoa shutuma za uongo dhidi ya serikali.

Zimbabwe na virusi vya corona

Jinsi serikali inavyoshughulikia janga la vizuri vya corona pia kumeibua hisia kuhusu hali ya mfumo wa afya nchini humo na kuchochea zaidi shutuma za rushwa, hali iliyosababisha ongezeko la ghadhabu miongoni mwa raia.

Tayari kumekuwa na hali ya siutafahamu hata kabla ya kuingia kwa janga la virusi vya corona nchini, hospitali hazina dawa za kutosha, vifaa vya kujilinda vya wahudumu wa afya na wafanyakazi wengine kwa kuwa madaktari wengi na wauguzi wameelekea nje ya Zimbabwe kwa ajili ya kutafuta mishahara mizuri, au kuingia kwenye mgomo kupinga malipo duni.

Ofisi ya kamishna wa Umoja wa mataifa inayoshughulikia haki za binadamu imesema ''imesikitishwa'' na kwamba ni kama vile Zimbabwe inavyotumia janga la Covid 19 kama kisingizio cha kubana uhuru wa raia.

Mwezi uliopita polisi walimkamta mwandishi wa habari za uchunguzi na kiongozi wa upinzani, wakishutumiwa kuchochea vurugu.

Kwanini maandamano yamepamba moto nchini Zimbabwe? - BBC News Swahili
 
1.rais wao anarudisha mashamba kwa wazungu
2.raia wanauliwa na polisi,mfano juzi mmoja kapigwa risasi ndani ya gari kama alivopigwa lisu ndani ya gari (yeye alipigwa na polisi wa zimbabwe)
3.hali ya kimaisha inazidi kuwa mbaya
4.hakuna uhuru wa maoni
 
Ahaa, akhsante mkuu.
 
Asante kwa updates, nikajua tatizo la Zimbabwe alikuwa Mugabe kama ilivyokuwa Gaddafi wa Libya
 
Ukombozi wowote uliofanyika duniani, ni lazima damu imwagike.
Hakuna ukombozi pasipo damu(bible say)
 
Asante kwa updates, nikajua tatizo la Zimbabwe alikuwa Mugabe kama ilivyokuwa Gaddafi wa Libya

mkuu,unajua hata Gaddafi walimsema tu vibaya mabeberu,wakati wake mambo yalikuw mazuri kasoro tu hakukuwa na uhuru wa kutoa maoni
hapo zimbabwe wakati wa mugabe matatizo yalikuwa ni madogo kulinganisha haya ya sasa,yani jamaa ni mbaya zaidi ya mugabe maana mugabe yeye alikuwa dikteta tu ila raia hawakuuwawa hovyo
 
Rais wa Zimbabwe Emmerson Mnangagwa ameshutumu vyama vya upinzani, na nchi za kigeni kwa kutekeleza vitendo vya 'uchokozi' dhidi ya nchi yake huku makundi ya watetezi wa haki za binadamu wakisema polisi na wanajeshi wameendelea kuwakatama wakosoaji mbalimbali.

Picha za vikosi vya usalama vikiwapiga raia zimesababisha ghadhabu miongoni mwa raia na wito Afrika Kusini kutaka kufungwa kwa ubalozi wa Zimbabwe nchini humo mpaka pale haki za binadamu zitakapofuatwa.

Mnangagwa ameapa kupambana vikali na wapinzani na wanaharakati wa haki za binadamu baada ya kuongezeka kwa maandamano ya kupinga vitendo vya rushwa na kutoridhishwa na namna hali ya uchumi inavyoshughulikiwa nchini humo.

Uchumi wa Zimbabwe umeporomoka, serikali ikinyooshea kidole vitendo vya unyonyaji wa kiuchumi na vikwazo vilivyowekwa na nchi za magharibi. Hashtag ya Zimbabweanlivesmatter ni kampeni iliyo maarufu duniani kote wakati huu.

Akitoa hotuba kwa njia ya Televisheni siku ya Jumanne, Bwana Mnangagwa alikemea kile alichokiita '' mipango ya uharibifu ya makundi ya kigaidi ya upinzani''.

''Wale wanaochochea chuki na kuvunja umoja hawatashinda. Watu ambao wamejaribu kuwagawa watu wetu na kudhoofisha mifumo yetu watashughulikiwa,'' alisema.
Wapinzani na wanaharakati juma lililopita waliitisha maandamano dhidi ya serikali, lakini taasisi za kiulinzi ziliwataka watu kusalia majumbani mwao.

Wanasheria wa wanaharakati wa haki za binadamu wamesema zaidi ya watu 60 wamekamatwa.

Mnangagwa katika hotuba yake amesema ''vikosi vya usalama vitaendelea kutekeleza majukumu yao''.

Sera ya mkono wa chuma dhidi ya wanaharakati wa upinzani
Robert Mugabe alipoondolewa madarakani kwa mapinduzi ya mwaka 2017, watu wengi nchini humo walikuwa na matumaini ya kuwa ni mwisho wa 'ukandamizaji na uongozi mbaya' uliokuwepo kwa miaka 37 alipokuwa madarakani.
1596552791795.png

Mnangagwa aliingia madarakani akiwa ametoa ahadi ya kufanya mabadiliko lakini wakosoaji wake wamekuwa wakimhusisha na matendo yale yale yaliyoeleza sifa ya Mugabe: utawala wa mabavu, matumizi mabaya ya fedha, kutetereka kwa uchumi na hali ya maisha.

Mnangagwa, 77, ambaye alitegemewa kuwa kiongozi ambaye angekuwa wa tofauti na kiongozi aliyemtangulia, wanaharakati wanamuona kuwa ni rais mkali zaidi kuliko hayati Mugabe.

Kwa mujibu wa New York Times, idadi ya wanaharakati wa upinzani walioshtakiwa kwa vitendo vya uhaini wakati wa utawala wa miaka mitatu wa Mnangagwa ni idadi kubwa kuliko ilivyokuwa kipindi cha Mugabe chote cha kuwepo madarakani, kwa mujibu wa utafiti wa muungano wa mashirika 22 ya wanaharakati wa Zimbabwe.

Wanaharakati wapinzani walikuwa na matumaini ya kufanya mkutano Ijumaa juma lililopita, kupinga miongoni mwa mengine wimbi la vitendo vya ukamataji na utekaji nyara mwezi Mei, pale wanaharakati wanawake watatu, akiwemo Mbunge, walitekwa, kupigwa na kudhalilishwa kingono na watu waliodaiwa kuwa mawakala wa serikali, shutuma ambazo serikali ilikana kuhusika nazo na baada ya kuruhusiwa kutoka hospitalini wanawake hao walishtakiwa kwa kutoa shutuma za uongo dhidi ya serikali.

Zimbabwe na virusi vya corona
Jinsi serikali inavyoshughulikia janga la virusi vya corona pia kumeibua hisia kuhusu hali ya mfumo wa afya nchini humo na kuchochea zaidi shutuma za rushwa, hali iliyosababisha ongezeko la ghadhabu miongoni mwa raia.

Tayari kumekuwa na hali ya siutafahamu hata kabla ya kuingia kwa janga la virusi vya corona nchini, hospitali hazina dawa za kutosha, vifaa vya kujilinda vya wahudumu wa afya na wafanyakazi wengine kwa kuwa madaktari wengi na wauguzi wameelekea nje ya Zimbabwe kwa ajili ya kutafuta mishahara mizuri, au kuingia kwenye mgomo kupinga malipo duni.

Ofisi ya kamishna wa Umoja wa mataifa inayoshughulikia haki za binadamu imesema ''imesikitishwa'' na kwamba ni kama vile Zimbabwe inavyotumia janga la Covid 19 kama kisingizio cha kubana uhuru wa raia.

Mwezi uliopita polisi walimkamta mwandishi wa habari za uchunguzi na kiongozi wa upinzani, wakishutumiwa kuchochea vurugu.

BBC Swahili
 
Ndio maana nikiona baadhi ya wapu***u wa humu wanaomshabikia wakala wa Mabeberu naumia sana. Kwa kariba ya huyo jamaa, JPM akasome. Yale Yale ya Mgabe na Mnagangwa. Tuliyasema haya Mambo humu.
 
Yule raisi si alimpindua mugabe dah, kumbe ata ss tukijichanganya mwaka huu lazima tunyooke zaidi ya ruler
 
Ndio maana nikiona baadhi ya wapu***u wa humu wanaomshabikia wakala wa Mabeberu naumia sana. Kwa kariba ya huyo jamaa, JPM akasome. Yale Yale ya Mgabe na Mnagangwa. Tuliyasema haya Mambo humu.
Mnangagwa baada tuu ya kupata Urais alitembelea Tanzania. Baada ya kurudi Zimbabwe akaanza kutawala kwa mkono wa chuma kama vile alikuja Tanzania kutafuta uzoefu flani. Unakumbuka ziara yake ile? Alikuja kutafuta nini Tanzania?
 
Hayo matatizo ya kiuchumi wanayolalamikia raia wa Zimbabwe ni matokeo ya vikwazo walivyowekewa na mabeberu.
 
Ndio maana nikiona baadhi ya wapu***u wa humu wanaomshabikia wakala wa Mabeberu naumia sana. Kwa kariba ya huyo jamaa, JPM akasome. Yale Yale ya Mgabe na Mnagangwa. Tuliyasema haya Mambo humu.
Hao mabeberu mnawasingizia tu!!! Viongozi waue watu, watese watu, maisha magumu, uchumi ndio huo unapolomoka, watu kukataa hali hiyo ndio uwakala wa ubeberu?!! Mbona sasa amekubali kuufyata kwa kuwalipa fidia hao mabeberu waliowachukulia mashamba!!!? Huyo rais ndio wale wale tu hatukutegemea jipya na ndicho kinachoonekana!!! Halafu anaibuka prof. Majalala eti vikwazo dhidi ya Zimbabwe viondolewe!!!
 
3 Reactions
Reply
Back
Top Bottom