Maandamano dhidi ya ufalme, Waziri Mkuu yaendelea Thailand

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
5,001
9,866
Licha ya kutangaza kutoongeza eneo la hali ya hatari, Waziri Mkuu wa Thailand ameitisha kikao maalum cha bunge katika wakati ambapo maandamano ya kumshinikiza kujiuzulu na mageuzi ya mfumo wa kifalme yakipamba moto.

Thailand Proteste in Bangkok (Jorge Silva/Reuters)

Katika kile kinachoonekana kama kulegeza misimamo yake, Waziri Mkuu Prayuth Chan-ocha aliwaambia waandishi wa habari kwamba hataongeza tena maeneo ya kuwa chini ya hali ya hatari nchini humo, na wakati huo huo akiwaomba waandamanaji kuandamana kwa amani. Hii ni hata baada ya kutowa amri ya kupiga marufuku mikusanyiko ya watu zaidi ya wanne.

"Hakuna mpango wa kuongeza maeneo ya kuwa na hali ya hatari. Serikali inajaribu kufikia muafaka kadiri iwezekanavyo. Ninataka kuwaomba mambo machache: musiharibu mali za umma wala za binafsi musifanye makosa na muhimu zaidi musiruhusu mapigano," alisema Waziri Mkuu Prayuth.

Lakini wakati waziri mkuu huyo akiitisha kikao cha dharura cha bunge kujadiliana mwenendo wa mambo, hakutaja lini vikao hivyo vitaanza. Kwa upande mwengine, maandamano yanayoongozwa na wanafunzi yanazidi kupamba moto katika taifa hilo la kifalme.

Waandamanaji wamekataa kabisa kutii maagizo ya serikali kuwazuwia kuingia mitaani, na badala yake jana Jumapili maandamano yalisambaa kwenye majimbo zaidi ya 10 nje ya mji mkuu, Bangkok.

Ajenda kuu za maandamano
Ajenda kuu kwenye maandamano hayo ni kuufanyia marekebisho mfumo wa kifalme ambao kawaida ulikuwa unalindwa na kuheshimwa sana nchini humo. Hata hivyo, utamaduni wa kuutukuza ufalme unazidi kuporomoka kutokana na khulka binafsi za Mfalme Maha Vajiralongkorn.

Mfalme huyo anatuhumiwa kwa matumizi ya anasa na ya kupindukia, na kwa siku za karibuni kuishi kwa muda mrefu zaidi akiwa kwenye hoteli moja ya kifakhari nchini Ujerumani. Hata hivyo, Waziri Mkuu Prayuth Chan-ocha, alisema hilo ni jambo lisilojadilika, akidai kuwa serikali ina wajibu wa kulinda ufalme "kwa sababu hilo ni jukumu la watu wote." Badala yake aliwaomba waandamanaji waandamane kwa amani."

Maandamano hayo ya wanafunzi, ambayo hayana uongozi maalum, yanadai pia kuachiliwa kwa watu waliokamatwa kwa sababu ya harakati za kisiasa, na kujiuzulu kwa Waziri Mkuu Prayut, mkuu wa zamani wa jeshi na kiongozi wa mapinduzi ya 2014.

Madai mengine ya kimsingi ni kuanzishwa upya kwa rasimu ya katiba iliyoandikwa na jeshi ambalo wanalituhumu kuiba uchaguzi wa mwaka jana.

Polisi ilisema zaidi ya watu 20,000 waliingia mitaani jana Jumapili, ingawa wanaharakati na vyombo vya habari vya ndani vinasema watu walikuwa wengi zaidi.
 
Back
Top Bottom