Maandamano baridi na Legal and Human Rights Centre, Salender Bridge

Jana usiku walisema maandamano yalikuwa yafanyike asubuhi, hatukuyaona! sasa hivi wanasema ni mchana kwa hiyo angalia usije ukatengeneza harafu likabaki nyumbani kwako likisomwa na familia yako tu!

Asubuhi walikutana ku strategise.... sasa mpango kamili ni hapo saa 8 mchana
 
Taarifa za kiinteligensia hazijawafikia wahusika? Je, wana kibali cha kukusanyika?
 
Najua Jeshi la Polisi limejipanga vizuri kupambana na wahuni FFU najua nidhamu yenu ya kazi, mkinyanyua bendera nyekundu juu apo ndio uwa nawakubali sana.

Hatutaki kusikia malalamiko eti jeshi limetumia nguvu nyingi.

Angalizo kwa wale wanaokwenda kwenye maandamano muondoke majumbani kwenu mmeaga kabisa kuna uwezekano wengine msirudi salama.
 
Najua Jeshi la Polisi limejipanga vizuri kupambana na wahuni FFU najua nidhamu yenu ya kazi, mkinyanyua bendera nyekundu juu apo ndio uwa nawakubali sana.

Hatutaki kusikia malalamiko eti jeshi limetumia nguvu nyingi.

Angalizo kwa wale wanaokwenda kwenye maandamano muondoke majumbani kwenu mmeaga kabisa kuna uwezekano wengine msirudi salama.

mkuu RITZ kwa mambo yalivyo sasa nashauri FFU walichukulie serious hili angalizo lako.
 
Hakuna haja ya kupeleka FFU wengi 15 tu wanatosha na gari 1 la maji washawasha..
 
Hakuna haja ya kupeleka FFU wengi 15 tu wanatosha na gari 1 la maji washawasha..

hapo kwenye red hapo!!labda hao ffu wawe wamejifunga mabomu ya kujitoa muhanga.FFU wamejichokea kwa kunywa komoni.
 
ritz yaani kuwa na bibi anatoka kenya unakuwa hivi,je wazazi wako wote wangetoka nje ya nchi ungekaa uonee huruma watanzania?
 
jamani ambaye yuko maeneo hayo atujuze hali ikoje .... tupo pamoja
 
Hivi hawa wanaokufa kutokana na mgomo wa madakitari sio watu?Wanaharakati wa haki za binadamu,wanawake na watoto NA MASHIRIKA YA KIMATAIFA yako wapi nasema yako wapi?
Huwa tunasikia mtu akibakwa au kutendewa ukatili tu wasemaji huwa wengi kulaani kitendo hicho, wapo wapi WAMA TGNP na wengine?
Naumia sana maana ni unafiki au huwa wanasema ili wapate sifa kwa serikali?mbona hili linalohusisha serikali hakuna anaenyanyua mdomo?
Mkuu wa wilaya alivuliwa hijabu vyombo vingapi vililaani tukio hilo?au ndio ulikuwa ni kujikosha kwa serikali,

HUU NI UKATILI KWA WANANCHI yaani bila aibu huku ndio KUTHUBUTU,KUWEZA NA KUSONGA MBELE?
JAMANI INAUMA SANA LABDA UWE HUNA NDUGU ALIYEATHIRIKA NA MGOMO HUU,kama huna angalia hata TV huru kama ITV jana utaamsha hisia zako kwenye hili,
WAKITANGAZA MAANDAMANO POTELEA MBAALI NIKAFIE HUKO nimeshachoka
 
Hivi hawa wanaokufa kutokana na mgomo wa madakitari sio watu?Wanaharakati wa haki za binadamu,wanawake na watoto NA MASHIRIKA YA KIMATAIFA yako wapi nasema yako wapi?
Huwa tunasikia mtu akibakwa au kutendewa ukatili tu wasemaji huwa wengi kulaani kitendo hicho, wapo wapi WAMA TGNP na wengine?
Naumia sana maana ni unafiki au huwa wanasema ili wapate sifa kwa serikali?mbona hili linalohusisha serikali hakuna anaenyanyua mdomo?
Mkuu wa wilaya alivuliwa hijabu vyombo vingapi vililaani tukio hilo?au ndio ulikuwa ni kujikosha kwa serikali,

HUU NI UKATILI KWA WANANCHI yaani bila aibu huku ndio KUTHUBUTU,KUWEZA NA KUSONGA MBELE?
JAMANI INAUMA SANA LABDA UWE HUNA NDUGU ALIYEATHIRIKA NA MGOMO HUU,kama huna angalia hata TV huru kama ITV jana utaamsha hisia zako kwenye hili,
WAKITANGAZA MAANDAMANO POTELEA MBAALI NIKAFIE HUKO nimeshachoka

Samahani mkuu labda nikuulize wewe ndiye uko wapi?
Wanaharakati muda huu wapo opposite na palm beach ndipo walipopanga kukutana kuanzia saa 8 mchana huu kuhusu suala hili la mgomo wa madaktari
 
08 February 2012


Muhimbili yafungwa



*Huduma zote zasitishwa hadi kitakapoeleweka
*Tamko la serikali lasubiriwa kuokoa jahazi
*Wizara yahaa kutafuta madaktari wa ziada
Na Waandishi Wetu
Majira

Vitanda vya wagonjwa vikiwa tupu kufuatia mgomo wa madaktari na wauguzi unaoendela katika Hospitari ya Taifa ya Muhimbili (MNH), madaktari bingwa na wauguzi wa hospitari hiyo wameungana katika mgomo huo kuanzia juzi, Dar es Salaam jana. (Picha na Michael Machellah)

HOSPITALI ya Taifa Muhimbili (MHN) imetangaza rasmi kusitisha utoaji wa tiba baada ya kuathiriwa na mgomo hadi hapo Serikali itakapotoa tamko rasmi kuhusu muafaka wake na madaktari.
Uamuzi wa hospitali hiyo kubwa kuliko zote nchini kusitisha kutoa huduma ulitangazwa Dar es Salaam jana na Ofisa Habari wa MNH Bw. Aminieli Aligaesha, alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari.

Alisema huduma hizo zimesitishwa kuanzia juzi kutokana na kamati ya madaktari bingwa kuandikia uongozi kwa MNH,Taasisi ya Tiba ya Mifupa (MOI) na Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi ya Tiba (MUHAS) kusitisha utoaji wa huduma zote zinazotolewa na hospitali hiyo.

Kwa msingi huo alisema huduma zitaendelea baada ya muafaka kupatikana.

Alisema kuwa wagonjwa walioko wodini wataendelea kuonwa na madaktari wachache waliojitolea, na wakuu wa idara waliopo hospitali hapo, ambapo madaktari wa JWTZ wataendelea kuona wagonjwa wa dharura.

Alisema kwa takwimu walizonazo kuanzi usiku wa juzi na jana asubuhi wapo wagonjwa 811 waliolazwa wodini na wanaendelea kupatiwa matibabu.

Hata hivyo alisema hali hospitalini hairidhisi kutokana na huduma kuendelea kudorora kila wodi, huku vitengo vingine vikiwa hakuna huduma hata moja inayoendelea.

Waandishi wa habari walipotembelea jengo la watoto walibaini hakuna huduma zozote zinazoendelea katika wodi hizo.

Akizungumza katika wodi hiyo Bi. Adela Shomari alisema kuwa tangu afike hospitali hapo mtoto wake hajapatiwa matibabu kwani licha ya kuwa anahitaji kufanyiwa upasuaji.

"Tangu nifike hospitali hapo kutoka Shinyanga mtoto wangu hajapatiwa matibabu zaidi ya kupewa vidonge vya kuongeza damu na panado," alisema.

Naye Saida Kassimu ambaye anamuuguza mtoto anayeumwa ugonjwa wa ngozi alianza kutokwa machozi baada ya waandishi wa habari kufika kwenye kitanda chake na kuanza kusimulia hali iliyopo hospitalini hapo.

"Roho inaniuma, nalia kwa uchungu nikiona mwanangu akiteseka, sina amani kwani leo ni siku ya tano tangu nilipofika hospitali hapo sijawahi kuonwa na daktari," alisema.

Habari ambazo gazeti hili lilipata ni kuwa Waziri wa Afya na ustawi wa jamii,Dkt. Haji Mponda,Naibu waziri Dkt. Lucy Nkya, Katibu Mkuu Bi Blandina Nyoni na Mganga Mkuu wa Serikali, Bw. Deogratasia Mtasiwa, jana usiku walitembelea hospitali hiyo saa sita usiku wa kuamkia jama ili kujionea hali ilivyo.

Wakati huo huo viongozi wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, kutwa nzima ya jana walishinda wakihaha kwa lengo la kutafuta madaktari wa kupeleka Muhimbili ili kuokoa jahazi.

Akizungumza na gazeti hili Dar es Salaam jana Ofisa Habari, Bw. Nsachris Mwamwaja alisema jana walikuwa wakitafuta madaktari wa kwenda kutoa huduma kwa baadhi ya wodi.

"Juzi kilikaa kikao na kuchukulia suala hilo kama dharura, hivyo iliamuliwa wachukuliwe madaktari wa wizara na kupelekwa Muhimbili," alisema na kuongeza;

"Jana tumehangaika huku na kule kutafuta madaktari hao, lakini hadi muda huu sina uhakika wamepatikana wangapi."

Alisema madaktari hao si mbadala wa tatizo, lakini watakuwa wanatoa msaada kwa zile kazi zilizopo hospitali hapo ambazo zimeachwa kabisa wakati ufumbuzi wa mgogoro huo ukiendelea.

"Sasa hivi tupo tunahangaika ili kuona ni jinsi gani tunaweza kupunguza idadi ya vifo," alisema. Wakati hayo yakiendelea suala hilo liliibuka bungeni jana mjini Dodoma baada ya Mbunge Godfrey Dhambi, kuomba mwongozo kwa Spika Bi Anna Makinda, akitaka kusitishwa kwa kikao cha bunge ili kujadili mstakabari wa madaktari.

Lakini mwongozo huo ulipingwa na Spika Makinda kwa maelezo kuwa suala hilo lipo katika kamati maalumu, hivyo ni vema kusubiri majibu kutoka kwa kamati hiyo.

Kutokana na kusitishwa lwa huduma katika hospitali hiyo, baadhi ya wadau wamesema ni lazima serikali itambue kuwa wananchi wanapoteza maisha, hivyo suala hilo linahitaji ufumbuzi wa haraka.

Mtanzania aliyeishi Ufaransa, Bw. Mohamed alisema Serikali imeshindwa kuonesha utu kwa kushindwa kumaliza suala hilo.

"Hili ni tatizo kubwa na hasa inapofikia hata kiongozi mkuu akashindwa kusema jambo lolote," alisema Bw. Mohamed .

Alisema viongozi wengi ni wabinafsi ndiyo maana wameshindwa kuchukua uamuzi mapema.

Naye Bw. Bw.Edgar Mwankuga alisema serikali imeshindwa kuweka maslahi ya wananchi mbele hasa katika huduma za muhimu kama sekta ya afya.

"Rais kuendelea kukaa kimya kuhusu mgogoro huo ni ishara tosha kuwa hana uchungu na sisi wananchi ambao kipato chetu hakituruhusu kwenda kutibiwa nje ya nchi",alisema Bw.Mwankuga

Naye Bi.Julieth Swai mkazi wa Dar es Salaam alisema watendaji wa JK wameshindwa kusuruhisha mgogoro huo kwa sababu kila kukicha hali inakuwa mbaya hasa katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili.
 
Tayari wanaharakati wamefunga Ally Hassan Mwinyi na Ocean Road jijini Dar es Salaam ili kufikisha ujumbe kwa wenye mamlaka. Lengo ni kuwaonyesha watoa maamuzi kuwa haturidhiki na hatua wanazochukua katika kushughulikia mgogoro wa madaktari.
 
Back
Top Bottom