Maandalizi ya ujenzi wa bomba la gesi toka Mtwara hadi Dar es salaam umoja wa wabunge wa kusini mpo


D

dostum

JF-Expert Member
Joined
Nov 1, 2010
Messages
215
Likes
55
Points
45
D

dostum

JF-Expert Member
Joined Nov 1, 2010
215 55 45
Huu ni mradi mwingine mkubwa ambapo pesa zake ni mkopo na hivyo watanzania kwa mara ingine watahitajika kuulipa pamoja na wewe, mtoto wako na mjukuu wako. Mradi huu utaaanza katikati ya Oct 2011 na kukamilika kati ya 2012 na 2013. kama wananchi tuliosahaulika!!! mradi huu ni fursa kwetu kupaza sauti na kuchukua hatua...? au tuache tu bomba la gesi lipite miguuni mwetu au ingekuwa busara kama tutappaza sauti "TUPATE WOTE UMEME AU TUKOSE WOTE....." ili badala ya kupitisha bomba wapitishe nyaya ili tuunganishwe kwenye gridi ya taifa na hivyo tutahitaji mtambo wa kufufua umeme ujengwe kanda yetu. Je mradi huu utakuwa na manufaa kwetu au watakao nufaika wengine? Bali sisi tutapaswa tunawalipie watu madeni bali umeme utakaozajishwa utawanufaisha wengine???? Mitambo ya Uzaliswaji wa umeme mchumchuma na kiwira utafanywa kule kule kule makaa ya mawe yalipo...... KWANINI? umeme wa gesi uzaliswe dar kwanini?.... Ni hekima na busara kwetu tuachwe asilimia zaidi ya 85% ambapo bomba hili litapita wasipate huduma ya umeme bali wabaki walipa madeni? KWA KILE TUNACHOSIFIWA KUWA SISI NI WATU WA AMANI NA UTULIVU, NA HIVYO KULETA MADAI KAMA HAYO TUTAHATARISHA AMANI............ Hadi sasa hakuna mpango wowote wa kuunganisha kanda ya kusini kwenye gridi ya taifa. Wengine watasema hakuna viwanda hivyo umeme kwetu si muhimu, swali nini huanza kati ya umeme au kiwanda?. Imefahamika kuwa gharama zilizotumika kuweka bomba la songas kama wangetumia uadilifu mtambo wa kufufulia umeme ungejegwa kilwa, gharama zilizotumika ziliweza kupitishwa nyaya za umeme wa gridi ya umeme wa taifa, toka Kilwa hadi dar, pesa hiyo hiyo zingewezeshwa jengwa daraja rufiji, kujenga barabara ya lami Lindi na hadi kibiti na hivyo kuvutia wawekezaji katika ukanda huu. Bali kwakuwa tulikosa wawakilishi wabunge na nawaziri kwa kwa wakati ule beni maamuzi mabovu yakapitishwa. Juzi Juzi tuliambiwa tatizo la umeme lililopo linatokaana na kuwepo kwa mchanga kwenye bomba la gesi na hivyo kumesababisha gesi kutopita kirahisi...... Kosa hilo hilo linarudiwa tena badala ya kujengwa mtambo wa kufufua umeme, na kupitishwa nyaya kwenye kanda yetu sisi tutaambulia bomba la gesi tu na kuachwa 85% ya mkoa ukiwa hauna umeme. kwa taarifa kwasasa tunalipa deni la umeme wa IPTL ambapo ambapo dola 163.5 sawa na milioni 766 hulipwa kwa siku. Pia Dowans wanapaswa kupitwa deni la dola 152 kwa siku kwani tayari dowans wameshinda kesi hiyo ya kudai malipo. Sijui Songas, Symbion Power, mikopo ya Kiwira na Mchuchuma tutalipa kiasi gani...... Ukweli na sasa tujiandae kulipa mabilioni ya fedha ambayo hadi sasa serikali haijaweka wazi ni kiasi gani....... MWISHo sijui kama ndugu zangu mtanielewa kwani nimeandika mawazo haya nikiwa na hasira nyingi zinazouumiza moyo wangu na hivyo kuamua kutapika.........nikipinga moja kwa moja mradi huu...... kuwa hauna manufaa kwa kanda yetu na kwa taifa kwa nionavyo mie. bali ningeunga mkono kama mradi zingeletwa nyaya tu na mtambo kujengwa kanda yetu. Nimesikia kuna umoja wa wabunge wa kusini kwa manufaa ya kanda yao bali wako kimya na wameziba pamba masikioni...... ningependa watuwekewe wazi suala hili..... otherwize nitakosa imani nao. NI MTAZAMO Tu
 

Forum statistics

Threads 1,235,907
Members 474,863
Posts 29,240,122