Maandalizi ya Ufisadi Mkubwa 2010/11wa hadi 100 Billioni | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Maandalizi ya Ufisadi Mkubwa 2010/11wa hadi 100 Billioni

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Bill, Jun 10, 2010.

 1. Bill

  Bill JF-Expert Member

  #1
  Jun 10, 2010
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 4,163
  Likes Received: 1,251
  Trophy Points: 280
  Nilijiuliza sana, inakuwaje mkuu aliyetajwa kuandaa mazingira ya Kagoda apewe ukurugenzi TIB?
  Ninajiuliza hizi fedha TZS 100 billion anazopewa anawezaje kuzisimamia kwa ukamilifu ukiondoa Mazingira yaliyojitokeza kipindi cha Kagoda kuelekea uchaguzi mkuu?
  Najiuliza pia ni kwa nini fedha hizi zitengwe kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi, tena msimamizi ni yule yule mwandaaji wa Kagoda? Maumivu mengine kwa WaTZ, najua Wabunge wetu watapitisha kwa kuunga mkono mia kwa mia na lakini .... japo kwa mbali.

  JK adokeza bajeti 2010/ 11: TIB yatengewa Sh100 bilioni

  Source: Mwananchi,
  Thursday, 10 June 2010
  Daniel Mjema, Moshi

  [​IMG]
  Rais Jakaya Kikwete

  RAIS Jakaya Kikwete amedokeza kitakachokuwamo katika bajeti itakayotangazwa leo Bungeni na Waziri wa Fedha, Mustapha Mkullo kuwa ni pamoja na Benki ya Rasilimali nchini (TIB) kutengewa Sh100 Bilioni.

  Fedha hizo zitakuwa ni kwa ajili ya kuwakopesha mikopo ya muda mrefu wale wanaotaka kuanzisha viwanda na wafanyabiashara ambao watakopa fedha hizo kwa ajili ya kufanya biashara kubwa zitakazoinua uchumi wa nchi.


  Rais Kikwete alitoa kauli hiyo jana jioni mjini Moshi wakati akizindua rasmi tawi la Benki ya KCB ambalo linaifanya Benki hiyo sasa kufikisha jumla ya matawi 11 tangu ianze kutoa huduma zake hapa nchini mwaka 1997.


  "Tumeamua kufanya hivi ili kuwazesha wafanyabiashara wetu wenye shughuli za muda mrefu ili waweze kukopa kwa sababu tunafahamu wanaweza wasikopeshwe na Benki hizi na tunaomba KCB mtuunge mkono," alisema.


  Rais Kikwete alisema kwa muda mrefu serikali imekuwa haiipatii TIB fedha za kutosha, lakini safari hii alilazimika kumwambia Waziri wa Fedha kuwa ni lazima wafanye uamuzi mgumu wa kuitengea TIB fedha za kutosha.


  Alisema lengo la serikali ni kuitengea TIB sh1 trilioni ili wafanyabiashara waweze kukopa benki mikopo ya muda mrefu na kuipa changamoto KCB kuangalia uwezekano wa kuanzisha dirisha na kutoa mikopo ya aina hiyo.


  Kwa mujibu wa Rais Kikwete, serikali hivi sasa iko katika mchakato wa kuanzisha benki ya wakulima na tayari serikali ya China imekubali kusaidia katika uanzishwaji wake na kwamba, mchakato wako uko hatua za mwisho.


  Awali mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa KCB, Dk Edmund Mndolwa alimweleza Rais Kikwete kuwa Benki hiyo ndiyo yenye mtandao mpana Afrika Mashariki ikiwa na rasilimali zenye thamani ya dola za Marekani 2.6 bilioni.


  Dk Mndolwa alisema japokuwa KCB ni benki ya wawekezaji wa kigeni lakini inawajali Watanzania na ndio maana kati ya wafanyakazi wake 250 walioko katika matawi yake 11 nchini, wafanyakazi watano tu ndio raia wa kigeni.


  Mwenyekiti huyo wa Bodi ya KCB alisema kuwa Benki hiyo imeamua kutumia tekinolojia ya kisasa ya kielektroniki ya T24 anbayo humuwezesha mteja wa benki hiyo kupata huduma haraka zaidi ikilinganishwa na tekinolojia nyingine.
   
 2. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #2
  Jun 10, 2010
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Nionavyo mimi haraka haraka wale mafisadi watakaokuwa tayari kuipa CCM watakopeshwa hizo fedha kabla ya October, na baada ya miaka michache itaripotiwa biashara zao ziliingiza hasara. Hili suala inabidi lifuatiliwe kwa makini na bila shaka watu wetu -- yaani wale wenye uchungu wa nchi hii walio ndani ya TIb -- watakuwa tayari kutuletea jinsi fedha hizo zitakavyotumika. Kazi kwenu.
   
 3. M

  Mdondoaji JF-Expert Member

  #3
  Jun 10, 2010
  Joined: Mar 17, 2009
  Messages: 5,106
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  Wakuu tusiwe society isiyokuwa shukrani na kila kitu tukawa na negative views. I am optimistic on this kwasababu a Tanzania Investment Bank ni financial institution hivyo basi ina taratibu zake na miongozo yake ambayo ikiwa haifuatwi benki itakufa na sidhani wafanyakazi na washikadau wako tayari kwa hilo. b. Malengo ya kukopesha sio mbaya ila wakopeshwaji fekindio ishu maana wakiwa wakopeshwaji feki ni ada na tatizo la nchi yetu.Hilo jambo ni systemic risk kuliondoa kunainvolve tabia za wanasiasa wetu, ulafi wa viongozi na pia jamii kwa ujumla kitu ambacho sio wala kesho tunaweza kukitatua. Tusiwe watu wa kuwa na shaka na kila jambo
   
 4. Ulimbo

  Ulimbo JF-Expert Member

  #4
  Jun 10, 2010
  Joined: Aug 14, 2009
  Messages: 678
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 45
   
 5. Bill

  Bill JF-Expert Member

  #5
  Jun 10, 2010
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 4,163
  Likes Received: 1,251
  Trophy Points: 280
  Hakika hatuna shaka na hiyo mipango, tatizo ni huu muda huu ambao serikali inatoa hizo fedha, tena inatoa kwa wa aiana gani - yaani wafanyabiashara wakubwa ambao ndio wamekuwa wakituliza siku zote kuanzia Import surport, EPA, Deep Green etc. Na swali rahisi la kujiuliza, ni kwa nini hii miradi mikubwa inaanzishwa katika kipindi cha kuelekea uchaguzi?

  Swali kwamba TIB ina wafanyakazi na mfumo wa kiutendaji unaoeleweka, sio kweli katika mazingira haya ya siasa za Tanzania na Bunge letu zezeta, huku Rais akipewa madaraka makubwa na hata Katibu wa Chama nae kuwa na madaraka makubwa ya kumtisha hata mtunga sheria aliyetumwa na jamii yake.

  Tutarajie maumivu mengine:A S-confused1:
   
 6. M

  Mdondoaji JF-Expert Member

  #6
  Jun 10, 2010
  Joined: Mar 17, 2009
  Messages: 5,106
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  Sidhani matatizo ya Deep Green,EPA, na mengineyo yataendelea kwani sasa hivi mafisadi wanajua tumekuwa wakali kwa pesa zetu. Hata kama wameanzisha hili hebu tuliangalie upande wa pili unadhani ni busara kukopesha akina mama ntilie, wamachinga ndio tutaweza kunyanyua uchumi? au tuwakopeshe watu wenye investment ambao wanaweza kuja kuajiri wananchi na kulipa kodi? Ziko wapi zile pesa za JK walikuwa wakopeshwe walalahoi lakini mwishoe hakuna lolote zaidi ya kwamba zile pesa zimetokomea kwa wakubwa na jamaa zao???. Vilevile ukiwakopesha wafanyabiashara wadogo wadogo na start up business risks huoni kubwa kuliko well established business?

  Yes I do agree with you kwamba uchaguzi unakuja na CCM pengine wanatafuta pesa za kupiga kampeni but isiwe ndio kigezo cha kuchelea kufanya maamuzi yenye faida kwa taifa. Mpango utanufaisha zaidi wananchi kama utekelezaji wake utakuwa makini. Viwanda vingi vimekufa Tanzania na main reason ni kukosa pesa ya kuviendesha. Pengine labda ili kudhibiti CCM wasifuje hizo pesa ni kwa kutoichagua CCM kwani kura hulazimishwi na mtu. Binafsi nadhani tukitilia mkazo uchaguzi uwe wa haki na usawa na pia swala la mgombea binafsi liruhusiwe pamoja uhuru wa vyama vya siasa. Tukiweka mazingira hayo hata kama CCM itakusudia kufisadi tutampigia kura mgombea binafsi tunayemkubali na pia wabunge binafsi tunaowataka hilo litaua meno ya CCM na kurudisha demokrasia ya kweli nchi.

  CCM ni chama na sio mungu na iko siku itakufa kama zilivyokufa dola zilizopita na watu wataisahau kabisa. Ila haimanishi mambo yenye faida kwa jamiii tuyaache kisa tunatofautiana kisiasa au kimtazamo hivyo nchi haitakwenda mbele
   
 7. PhD

  PhD JF-Expert Member

  #7
  Jun 10, 2010
  Joined: Jul 15, 2009
  Messages: 3,819
  Likes Received: 818
  Trophy Points: 280
  mkurugenzi mkuu wa TIB ndug. Peter Noni duhh kala EPA na sasa wanamtumia tena kula bilioni 100 za uchaguzi , wiki iliyopita alikuwa na Rostam aziz Dubai wakipanga mipango ya kuiepa na kuikagoda Nchi kwa baraka za mkuu wa pale baharini, na bado mtamkumbuka nyerere na mzee mkapa, huy mkweereee tutakoma tu
   
 8. W

  WaMzizima Senior Member

  #8
  Jun 10, 2010
  Joined: Jun 25, 2009
  Messages: 154
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Wa Tz tuna kila haki ya kuwa pessimist na hii mipango ya utoaji hela kwa sababu za kihistoria. Lakini kama mdau Mdodoaji alivyosema ni lazima tuanze hii mipango ya kuendeleza biashara kubwa. Mi ushauri wangu ni kuwa pamoja na watu binafsi ningependekeza pia baadhi ya mashirika ya umma yenye potential nayo pia yapewe hii mikopo. Vilevile ni muhimu tuanze kuwa na mortgage loans Tz maana hii pia ni overdue hapa kwetu.

  Kwa ujumla ni wazo zuri tatizo kama kawaida ni suala la utekelezaji, naamini baada ya kibano cha EPA na Richmond hawa watu wanaopenda kutafuna hela za umma watakaa kando. Lakini si wa tu ndio tatizo ni wajibu wetu wote kama wananchi kuwafichua wote watakao hujumu hizi hela maana watajulikana. vilevile ni bora bunge likaendelea kuwa makini katika kufuatilia namna hiyo mikopo itakavyotolewa. Lakini kwa ujumla ni wazo zuri, na si kweli kuwa kila kitu CCM inachoanzisha nyuma yake kuna mpango wa kifisadi ni muhimu kuumpa Jack Mrisho benefit of the doubt ili aweze kufanya kazi zake kwa ufanisi.
   
 9. Bill

  Bill JF-Expert Member

  #9
  Jun 10, 2010
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 4,163
  Likes Received: 1,251
  Trophy Points: 280
  Tatizo sio hiyo mipango, tatizo lipo kwenye usimamizi wa hizo hela. Hela za EPA tuliambiwa zimeenda TIB, lakinin bado hatujaona impact (matokeo) yake katika uchumi, sasa hivi tena kama haitoshi hizo hela za kiini macho zilizorudishwa na wana EPA kuwa hazijawa na uthibitisho wowote tunatoa tena Bilion 100 kwa kwenda TIB, tuan improt surport, tumeshindwa kuziridisha halafu tunatoa tena zingine. Huu ni upuuzi. Ninyi subirini tu muone hayo makampuni yatayokopeshwa. Mtaendelea kukamuliwa vijikodi kwenye vijimishahara vyenu hadi mtakoma.
   
 10. M

  Mdondoaji JF-Expert Member

  #10
  Jun 10, 2010
  Joined: Mar 17, 2009
  Messages: 5,106
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  Lakini Swala la EPA ni kwanza hizo hela zilikuwapo? Unategemea matokeo wakati hatujui hata kama hizo hela zipo au la? Tukishafahamu kama hizo pesa zimerudishwa then ndio tuseme zimetumikaje? Kuhusu haya maswala mawili TIB haihusiki ni Serikali ya Kikwete na watendaji wake ambao tunaweza kuwaadabisha katika uchaguzi watueleze hela za EPA zimerudi au la? Kama hazijarudi zimechukuliwa hatua gani? Kama zimerudi zilienda wapi mbona hatuzioni?

  TIB wameahidia hela za EPA wameahidiwa hela hizi but wanasiasa huahidi kufanya baadae tulijue hilo hivyo basi kama hawajazipeleka TIB hizo pesa ni ngumu kujua impact yake katika uchumi. Tusiwalalamikie TIB wakati ishu ipo kwenye serikali ya Kikwete yenyewe hapo ndio penye matatizo yaani no utendaji!!!!
   
 11. Z

  Zhule JF-Expert Member

  #11
  Jun 10, 2010
  Joined: May 22, 2008
  Messages: 354
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mkuu unatuchanganya, Kikwete alisema pesa za EPA zilizorudishwa ziliperekwa TIB na wizara ya kilimo. Hadi leo hatujaona impact wala TIB hawajakanusha kwamba hawakupewa sesa hizo. Leo kikwete huyo huyo anasema TIB imetengewa Bilioni 100. Baada ya uchaguzi tusipoona impact utasema ilikuwa ni ahadi tu za wanasiasa pesa hazikutolewa? Acha siasa mkuu rais atanii tusipoona matumizi tujue moja kikwete na TIB lao moja.
   
 12. Ntemi Kazwile

  Ntemi Kazwile JF-Expert Member

  #12
  Jun 10, 2010
  Joined: May 14, 2010
  Messages: 2,145
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
   
 13. A

  Audax JF-Expert Member

  #13
  Jun 10, 2010
  Joined: Mar 4, 2009
  Messages: 444
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Mimi sometimes huwa nalia kwa uchungu nilonao kwa mtanzania maskini ambaye hakwenda shule!!
   
 14. H

  Hofstede JF-Expert Member

  #14
  Jun 10, 2010
  Joined: Jul 15, 2007
  Messages: 3,584
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 0
  Kama EPA iliidhinishwa na Mkapa how come tumkumbuke?. Mkapa na JK wote ni waarabu wa pemba...Tatizo letu watanzania tunashindwa kujua kuwa Accounting officer wa nchi ni Rais- Kama tuna accounting officer aliyepata kazi kifisadi ni dhahiri kuwa pesa zetu zitaendelea kuwa mashakani mpaka pale tutakapompata accounting officer muadilifu. katika historia ya nchi yetu labla JKN, the rest ni wolves
   
 15. MchunguZI

  MchunguZI JF-Expert Member

  #15
  Jun 10, 2010
  Joined: Jun 14, 2008
  Messages: 3,623
  Likes Received: 590
  Trophy Points: 280

  Sijui una mfano gani mzuri, lakini ni serikali gani hiyo inayopanga mipango mipya kila mwaka kwa miaka 5 iliyopita, inayopandisha kodi kila mwaka kwa miaka 5 iliyopita? If tax scheme is unstable what economy is that one? Ni elimu ya form 6 tu ndo inayohitajika hapo.

  Mipango kama hii ingepangwa miaka mitano iliyopita, sasa tungepata matokea yake na iwe ishara ya kupewa kipindi kingine.
   
 16. m

  muheza2007 JF-Expert Member

  #16
  Jun 10, 2010
  Joined: Mar 19, 2010
  Messages: 232
  Likes Received: 121
  Trophy Points: 60
  Nyie laleni halafu baadaye mnalalamika na kulia umaskini! Hivi mmewahi hata kwenda TIB na mkaambiwa hakuna pesa za kilimo?

  Hata hizi pesa badala ya kuungana tuanzishe miradi ya maana, mtabaki kulalamika hapa huku wajanja wanachukua wao.

  TIB kuna pesa, tumia akili ya Mbayuwayu changanya na ya kwako kisha nenda TIB.
   
 17. M

  Mdondoaji JF-Expert Member

  #17
  Jun 11, 2010
  Joined: Mar 17, 2009
  Messages: 5,106
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  Mie sijakuchanganya ila mie ninachosema kuna mtu ameziona pesa zilizorudishwa na sio lazima azione wabunge wa upinzani wamehakikishiwa kitu. Kikwete namjua ni mwanasiasa anasema vitu vingi lakini vilivyokuwapo ni vichache but kuhusu hili la EPA naona bado halijaisha na nadhani dawa ni sie wananchi kuwalazimisha tuliowachagua 2005 watuambie zimekwendaje zimekuaje pesa za EPA amasivyo hamna kura. Lakini tukija ishu ya TIB hawana kosa wao ni financial institutions wanapokea pesa na kukopesha huwezi kusema eti hizi pesa zitaliwa zishapelekwa kwanza? Wanataratibu gani za mikopo? Nani wamekopa? Mteja akishindwa wanafanyaje? Maswali ni mengi but TIB watahusika ikiwa wametumika kuzitafuna pesa which mpaka sasa mie na wewe hatujui zaidi ya base less speculations!!!
   
 18. mtuwatu

  mtuwatu Member

  #18
  Jun 11, 2010
  Joined: Oct 21, 2009
  Messages: 95
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Duh,
  Bongo inatisha jamaani,kila siku kuna jambo linaloshangaza ulimwengu - Mungu tusaidie sisi na watoto wetu,Amen.
   
 19. Z

  Zhule JF-Expert Member

  #19
  Jun 11, 2010
  Joined: May 22, 2008
  Messages: 354
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  This is not base less speculation. KUNA MTU KAONA PESA? well zikifanya nini pesa hizo?. MIMI naongelea impact yaani investments kama ilivyokusudio la TIB. Tusipoona list ya investments (majengo, viwanda, mashamba, huduma n.k) wala majina ya wakopaji na tumeambiwa walipewa pesa za EPA na sasa bil.100 tutasema kuna pesa hapo, na kama zilikwepo hazijatafunwa?
   
Loading...