Elections 2010 Maandalizi ya uchaguzi Mkuu kutafuna Bil. 67/-

MwanaFalsafa1

JF-Expert Member
Feb 26, 2008
5,565
836
Sharon Sauwa


Jumla ya shilingi bilioni 67 zinatarajiwa kutumika katika kufanikisha maandalizi ya uchaguzi mkuu utakaofanyika Oktoba mwakani kwa ajili ya kuwapata madiwani, wabunge na rais.

Makadirio ya gharama hizo, yameelezwa Jijini Dar es Salaam na Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, (NEC) Jaji Lewis Makame na Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar (ZEC), Bw. Khatib Mwinyichande.

Waliyaeleza hayo katika hafla ya kusaini mkataba wa mradi wa kusaidia uchaguzi mkuu.

Wamesema fedha hizo ni kwa ajili ya kugharamia maandalizi ya uchaguzi huo Zanzibar na Bara, ambapo Shirika la Kimataifa la Maendeleo (UNDP) pamoja na wafadhili wengine ambao wamekuwa wakisaidia katika kufanikisha chaguzi mbalimbali.

Wameeelza kuwa UNDP, Uingereza, Denmark, Sweden, Umoja wa Ulaya (EU), Finland, Uholanzi, Norway na Uswis zimetoa jumla ya Sh. Bilioni 40 kusaidia katika uchaguzi huo.

Kwa upande wake, Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini, Oscar Fermandez Taranco, amesema mradi huo utaendelea hata baada ya uchaguzi mkuu.

Akasema mradi huo utasaidia kupanga na kusimamia baadhi ya mahitaji ya mchakato wa uchaguzi, ikiwemo uandikishaji wapiga kura, kuratibu wasimamizi wa uchaguzi na mawasiliano.

"Lengo kubwa ni kuimarisha uwezo wa kitaifa wa kuendesha uchaguzi ulio huru wa haki na wa kuaminika," akasema Bw. Taranco.

Akizungumzia msaada huo, Jaji Makame akasema fedha hizo zitatumika katika kuwezesha elimu ya upigaji kura, kuboresha daftari la wapiga kura, kuwawezesha waangalizi wa uchaguzi wa ndani na nje na kuviwezesha vyombo vya habari kuripoti shughuli za uchaguzi kwa uwazi bila upendeleo.

Naye Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bw. Benard Membe, amesema uchaguzi huru, wa haki, wazi na amani ni muhimu katika kuthibitisha uwepo wa demokrasia nchini.

"Hii inailazimu serikali kuanza maandalizi muhimu ili kuhakikisha kila mtu ambaye ana uwezo wa kupiga kura kwa mujibu wa sheria anapata nafasi ya kufanya hivyo kwa haki na uwazi," akasema.

Akasema tangu kuingia kwa mfumo wa vyama vingi nchini mwaka 1992, Serikali imekuwa ikihamasisha na kuzingatia vigezo vya demokrasia.

ALASIRI
 
Hii ni habari njema kwa wapenda Demokrasia. Shida ni moja tu: hatujui kama zitatumika ilivyokusudiwa.
 
Ingekuwa habari njema kama kungekuwa na "ELECTION" lakini bongo kuna "SELECTION" hivyo si habari njema. Bora pesa hizo zingetumika kufanya mambo mengine ya maendeleo kuliko uchaguzi hewa wakati wataoshinda wanakuwa wameshateuliwa!
 
Back
Top Bottom