Maandalizi ya Mkutano Mkuu Maalum wa CCM 23 July, yamekamilika

figganigga

JF-Expert Member
Oct 17, 2010
25,658
55,487
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Chama Cha Mapinduzi kitafanya Mkutano Mkuu Maalumu wa Taifa tarehe 23 Julai, 2016 mjini Dodoma. Maandalizi ya Mkutano huo yamekamilika.

Kabla ya kufanyika kwa Mkutano Mkuu huo kutatanguliwa na Vikao vifuatavyo:-
  1. Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa tarehe 21 Julai, 2016

  2. Halmashauri Kuu ya Taifa tarehe 22 Julai, 2016.
Wajumbe wote wa Mkutano Mkuu wa CCM wanakaribishwa na tunawatakia safari njema ya kutoka mikoani mwao kuelekea mjini Dodoma.

Imetolewa na:-

upload_2016-7-15_15-36-21.jpeg

Nape Moses Nnauye (Mb.),

KATIBU WA HALMASHAURI KUU YA TAIFA

IDARA YA ITIKADI NA UENEZI

15/07/2016
 
View attachment 366487

Nape Moses Nnauye (Mb.),

KATIBU WA HALMASHAURI KUU YA TAIFA

IDARA YA ITIKADI NA UENEZI

15/07/2016

Habari njema hii, dadadeki,

Raisi wa JMTZ na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM),

Pombe Magufuli (PhD)!
 
Inasemekana ameapa kulala nao Mbele akina Bulembo. Cha kwanza kukifanya ni kumuagiza CAG akague UWT, Jumuia ya Wazazi na UVCCM.

Inasemekana amedai inatakiwa chama kiache utaratibu wa kutumia fedha za serikali badala yake kiendeshe mambo yake kwa vyanzo vyake yenyewe. Na inasemakana kaanza kuchukia mapema si kawaida. Kuna mtafaruku wa maana huku wandugu.

Ngoja tuendelee kusubiria kwa hamu hayo mapichapicha ya hawa CCM.
Kila la Kheri Magufuli katika kuisuka CCM.
 
Si ndio vizuri, anakinyoosha chama kama anavyonyoosha Serikali, chama kitazidi kuimarika baada ya muda na imani ya wananchi itazidi mara dufu. Unatakiwa kuionea wivu CCM kwani inasafishwa. Endelea Magu hayo ndio mabadiliko, hata kama yataumiza baadhi ya watu
 
Hivi Kolimba sababu ilikuwa ni nini vile? Sikuwa na umri wa kufuatilia siasa, baadae naanza kusikia " nita kukolimba nita kukolimb"".
 
Inasemekana ameapa kulala nao Mbele akina Bulembo.
Cha kwanza kukifanya ni kumuagiza CAG akague UWT, Jumuia ya Wazazi na UVCCM.
Inasemekana amedai inatakiwa chama kiache utaratibu wa kutumia fedha za serikali badala yake kiendeshe mambo yake kwa vyanzo vyake yenyewe. Na inasemakana kaanza kuchukia mapema si kawaida. Kuna mtafaruku wa maana huku wandugu.
Ngoja tuendelee kusubiria kwa hamu hayo mapichapicha ya hawa CCM.
Kila la Kheri Magufuli katika kuisuka CCM.
Mkuu utawashitua mapema watamnyima uenyekiti, we kaa kimyaa ili wampe uenyekiti ndiyo tuanze kuchochea kuni ili ugali uive haraka
 
Back
Top Bottom