Maandalizi ya mgomo - leo, kesho na mtondo ni elimu ya uraia na kuhamasishana

MPadmire

JF-Expert Member
Mar 7, 2006
3,928
3,224
Watanzania wengi wapo gizani, hawaelewi mambo yote yanayoendelea.

Watanzania wengi hawaelewi kwa sababu hawana muda wa kufikiri, kujadili na kupata habari za ufedhuli wa Xicmm.

Wananchi wapo na mawazo ya shida, na wanaamka mapema kukimbilia kwenye shughuli za kujipatia angalao mlo mmoja.

Sio watanzania wote wanaweza kupata gazeti au kusoma hapa JF.

Nasema watanzania wengi wamefungiwa katika mtungi na hawaelewi kutokana na mfumo wa maisha.


Kitu ambacho kimesaidia kuongeza uelewa wa wananchi ni mikutano na maandamano ya CDM.

Sasa nashauri hivi, tuanze na kutoa habari na elimu kwa wananchi.

Kuandaaa vipeperushi na kuvisambaza nchi nzima. Wanaharakati kama LHCR na NGOs watusaidie

Pia vyama vya siasa visaidie hili.


Wananchi wakishaelimika, inakuwa raisi kuanzisha maandamano maana wananchi wataelewa maana ya maandamano na faida zake.

Sasa hivi serikali ya Xicm imewapuuza wananchi sana na hata kujiongezea posho na kuwanyima madokta na waalimu mishahara
 
Ni kweli kabisa watanzania wengi wanakosa fursa kutokana na kupanda kwa gharama za vyanzo vya taarifa(mfano:leo gazeti la kila siku la Mwanachi limepanda bei toka Tsh 500 hadi Tsh 800)za kujua kinachoendelea katika harakati za kuhakikisha mustakabali wa maendeleo ya taifa lao kama uko sawa au hauko sawia.Kuna umuhimu wa kutumia njia mbadala kutoa elimu kwa umma ili wengi wajue hali halisi inayolikabili taifa hili na hivyo kupata mwamko wa kupigania haki za watanzania.Naunga mkono hoja.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom