Maandalizi ya Mapishi ya Ndizi mshale na nyama ya ng'ombe

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,266
33,039

Mahitaji ya pishi hili ni pamoja na ndizi mshale kiasi unachopenda kulingana na familia yako, nyama ya ng'ombe nusu kilo vitunguu maji vikubwa viwili nyanya moja pilipili hoho moja, karoti moja, mafuta ya kupikia kijiko kikubwa kimoja na chumvi kiasi..Jinsi ya ya kuandaa na na kupika anza kwa kuosha nyama vizuri na katakata vipande vidogo unavyopendelea na kisha chemsha hadi iive.Nyama yenye mafuta kidogo na mifupa kidogo inafaa sana kwa ndizi, kisha menya ndizi zako vizuri na kuzikata katikati kwa urefu na kisha kwa upana (msharazi) kisha zioshe na kuweka kwenye sufuria yenye maji masafi.
Hivi ni viungo unavyotumia,katakata vitunguu,nyanya karoti na pilipili hoho halafu chukua sufuria ya kupikia na weka ndizi kiasi kisha weka nyama na supu yake na vitu vyote ulivyokatakata weka pamoja(vitunguu, nyanya,hoho na karoti)Kisha weka na ndizi zilizobaki kwa juu
Hakikisha supu uliyoweka inatosha kuivisha ndizi kama ni kidogo sana ongeza maji ya moto na pia hakikisha ndizi hazizami zote kwenye supu,bandika jikoni kwa moto wa kiasi na ziache zichemke,geuza na kisha weka mafuta ya kupikia (na nazi tui la kwanza ukipenda) Acha ziive kabisa bila kuwa na kiini katikati ukiridhika kuwa zimeiva ipua.
Andaa meza tayari kwa kula ni chakula kitamu sana pembeni ukiwa na juice,chai au maji ya kunywa pamoja na matunda kama avocado mlo unakuwa umekamilika farkhina upo mama mkwe?
 
Last edited by a moderator:
Hongera MziziMkavu kumbe nawe jikoni wamo eeh!!!! Nasubiri mapishi ya ndizi mzuzu za nazi na Tambi za kukaanga :):)
 
Last edited by a moderator:
Haya na wewe ukakarangize bwana mkubwa!!

Huyo BAK anakarangiza balaa anajua kupika hasa (kama nimeonja vile) hadi wajirani nyumba ya saba wanapata habari wanajishibia hasa ila haleti recipe huyo mchoyo huyo sijapata kuona...siku akileta recipe naja huko kwako kwa miguu tena winter na ndala na kigauni cha summer tu lol

Sent from my BlackBerry 9320 using JamiiForums
 
Last edited by a moderator:
Hahahahahahaha lol!!!!!! karibu sana karibu mpaka ndani :):)

Heee sio kwako ivoo kwa gorgeousmimi nije kwako wataka nipigisha makofi na mwenye mali kwanza kupigana siwezi ndo kabisaaa watu wakali na vyao yakheee mie sisibutuuuu alafu mara kwenye geti pana dog kimo kama cha ng'ombe ndama aku mwenzangu.......

Sent from my BlackBerry 9320 using JamiiForums
 
Last edited by a moderator:
Mkwe wangu Viol chakula upendacho ichi hebu jipikie

Sent from my BlackBerry 9320 using JamiiForums
 
Last edited by a moderator:
LOL!!!! Beware of Dogs, enter at your own risk...Sinasikia una black belt? umesahau yale mazoezi yako ya panda shuka ili kujenga pumzi.....Hao dogs wakikuona tu watakupa mgongo kwa woga :)

Heee sio kwako ivoo kwa gorgeousmimi nije kwako wataka nipigisha makofi na mwenye mali kwanza kupigana siwezi ndo kabisaaa watu wakali na vyao yakheee mie sisibutuuuu alafu mara kwenye geti pana dog kimo kama cha ng'ombe ndama aku mwenzangu.......

Sent from my BlackBerry 9320 using JamiiForums
 
Mahitaji ya pishi hili ni pamoja na ndizi mshale kiasi unachopenda kulingana na familia yako, nyama ya ng'ombe nusu kilo vitunguu maji vikubwa viwili nyanya moja pilipili hoho moja, karoti moja, mafuta ya kupikia kijiko kikubwa kimoja na chumvi kiasi..Jinsi ya ya kuandaa na na kupika anza kwa kuosha nyama vizuri na katakata vipande vidogo unavyopendelea na kisha chemsha hadi iive.Nyama yenye mafuta kidogo na mifupa kidogo inafaa sana kwa ndizi, kisha menya ndizi zako vizuri na kuzikata katikati kwa urefu na kisha kwa upana (msharazi) kisha zioshe na kuweka kwenye sufuria yenye maji masafi.
Hivi ni viungo unavyotumia,katakata vitunguu,nyanya karoti na pilipili hoho halafu chukua sufuria ya kupikia na weka ndizi kiasi kisha weka nyama na supu yake na vitu vyote ulivyokatakata weka pamoja(vitunguu, nyanya,hoho na karoti)Kisha weka na ndizi zilizobaki kwa juu
Hakikisha supu uliyoweka inatosha kuivisha ndizi kama ni kidogo sana ongeza maji ya moto na pia hakikisha ndizi hazizami zote kwenye supu,bandika jikoni kwa moto wa kiasi na ziache zichemke,geuza na kisha weka mafuta ya kupikia (na nazi tui la kwanza ukipenda) Acha ziive kabisa bila kuwa na kiini katikati ukiridhika kuwa zimeiva ipua.
Andaa meza tayari kwa kula ni chakula kitamu sana pembeni ukiwa na juice,chai au maji ya kunywa pamoja na matunda kama avocado mlo unakuwa umekamilika farkhina upo mama mkwe?

Kwa jinsi mtiririko huu ulivyo sytematic,hakuna atayeshindwa kujipikia hiki chakula.
Amani kwako mkuu..
 
Last edited by a moderator:
3 Reactions
Reply
Back
Top Bottom