Elections 2010 Maandalizi ya kusimamia kura za CDM Igunga.

SenBoy

Member
Sep 7, 2011
38
40
Niko Mza hapa, tunaishi mtaa mmoja na diwani wa Kitangiri. Nyumbani kwake kuna kundi kubwa mno la vijana pamoja na magari lukuki na Coaster ya kukodi ya Mukesh. Nilipouliza kuna nini, nikaambiwa ni vijana maalum ambao wameandaliwa kwenda kusimamia upigaji wa kura Igunga. Muda si mrefu wataanza safari.

Kilichonifurahisha, nimeambiwa wamepewa maneno mazuri sana na wamesisitizwa sana kutojihusisha na vurugu zozote zile. Ila wameambiwa waripoti matukio yoyote yale kwa ufasaha. CDM mliopo Mza na mnaosoma ujumbe huu wajuzeni ndugu zetu zaidi.
 
Hapo ndipo ninapoona mwitikio,mwamko na ari ya mabadiliko ya uongozi katika nchi yetu ya tz. Si muda mrefu sana tutaisahau ccm na dhuluma zake.
 
Kwa walioko Igunga, inatakiwa mvizunguke vituo vya kupigia kura kwa Mita 100 mpaka shughuli ya kuhesabu kura iishe na matokeo yatangazwe. Mkilala tu, tumeliwa CCM wezi mno
!
 
Dr Slaa kaishasema kura zitaibiwa hakuna haja ya kuangaika na uchaguzi.

Hakuna siku nzito kwa Kashidye, kama jumapili jioni kwanza lazima akatae kusahini matokeo ya uchaguzi
 
Hapo ndipo ninapoona mwitikio,mwamko na ari ya mabadiliko ya uongozi katika nchi yetu ya tz. Si muda mrefu sana tutaisahau ccm na dhuluma zake.

namuomba Mungu atufikishe huko mapema.
 
Dr Slaa kaishasema kura zitaibiwa hakuna haja ya kuangaika na uchaguzi.

Hakuna siku nzito kwa Kashidye, kama jumapili jioni kwanza lazima akatae kusahini matokeo ya uchaguzi

mmeshapanga matokeo?
 
Nimesikia kuwa msimamizi wa uchaguzi bwana Magayane amesema kuwa Mawakala wanatakiwa kutoka katika jimbo husika la uchaguzi na kwamba hiyo ndiyo sheria, sa itakuwaje hapo mkubwa?
 
Msisumbuke mkaangalia mikutano ya CCM mkadhani wale ni wapiga kura halisi,pale wapiga kura ni robo na wengi wao ni mamluki kutoka kahama,nzega na singida ambao kisheria hawaruhusiwi kupiga kura,kwa hyo CDM ushindi huko palepale ukizingatia waliokuwa kwenye mikutano wote ni wapiga kura maana ni wenyeji wa Igunga waliokuja kwa miguu na baiskeli zao

Na iwe hivyo!!
 
Nimesikia kuwa msimamizi wa uchaguzi bwana Magayane amesema kuwa Mawakala wanatakiwa kutoka katika jimbo husika la uchaguzi na kwamba hiyo ndiyo sheria, sa itakuwaje hapo mkubwa?

Kwani tatizo lipo wapi hapo mkuu, CDM si mnakubalika Igunga mawakala si wengi tu
 
Dr Slaa kaishasema kura zitaibiwa hakuna haja ya kuangaika na uchaguzi.

Hakuna siku nzito kwa Kashidye, kama jumapili jioni kwanza lazima akatae kusahini matokeo ya uchaguzi

wewe ni jinsia gani?
 
Kila kukicha najikuta nakipenda CHADEMA kuliko jana yake. Sababu hasa ni kwamba viongozi wetu ni WASIKIVU SANA, wanatutafuta maoni, na hawachelewi utekelezaji wake mara baada ya kutafakari kiundani zaidi.

CHADEMA tuhakikishe ya kwamba
kila kituo cha kupigia kura kuwepo na wasimamizi si chini ya wanne; demokrasia siku zote ni gharama!!!!!!!!

hapa tuko wana cdm 70 kutoka Moshi. Haibi mtu kura.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom