Maandalizi ya kushusha bei ya umeme yaanza

diana chumbikino

JF-Expert Member
May 29, 2018
428
368
WAZIRI wa Nishati na Madini, Dk Medard Kalemani amesema serikali inatarajia kufanya mabadiliko ya gharama za bei ya umeme na gesi asilia viwandani. Hivyo ametoa mwezi mmoja kuangaliwa upya gharama za bei ya gesi asilia viwandani huku mabadiliko ya gharama za umeme yakitarajia kufanyika baada ya kukamilika kwa mradi mkubwa wa uzalishaji umeme kwa maji kwani gharama za uzalishaji zitapungua.

Kalemani alisema hayo jana wakati akizindua matumizi ya gesi asilia katika kiwanda cha Lodhia Plastic Industries Limited kinachozalisha mabomba ya plastiki na nondo kilichopo Mkuranga Mkoa wa Pwani kinachotumia futi za ujazo za gesi asilia 200,000 kwa siku.

Waziri alibainisha kuwa mpaka sasa viwanda 48 vinatumia gesi asilia ambayo inapunguza gharama za uzalishaji kwa asilimia 50 hadi 30 ukilinganisha na matumizi ya mafuta mazito. Alisema baada ya kukamilika kwa miradi mikubwa ya umeme yatafanyika mapitio ya gharama ya kununua umeme jambo litakalofanya bila shaka kushuka kwa bei ya umeme hivyo kutaka uongozi wa kiwanda wanaotaka ruzuku ya asilimia tano kwa kununua megawati 14 za umeme kusubiri mabadiliko hayo.

Alisema uwekezaji gesi asilia viwandani hauchangamki inawezekana kuna vikwazo mbalimbali lakini bei ya kununua gesi inaweza kuwa changamoto kwani kwa sasa ni dola 4.7 hadi 7.72 kwa uniti. Alitoa mwezi mmoja kwa Shirika na Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC), Mamlaka ya Udhibiti wa Nishati na Maji (EWURA), Mamlaka ya Udhibiti wa Mkondo wa Juu wa Petroli (PURA), wataalam wa wizara na wanasheria husika kufanya mapitio ya bei ya gesi viwandani kama ni kikwazo kwa wawekezaji kutumia gesi asilia.

Alisema gharama hiyo lazima ilingane na mahitaji ya serikali, wawekezaji kunufaika bila kuathiri mapato ya serikali ili wahakikishe kunakuwa na bei inayoendana na mahitaji kwa watumiaji viwandani kwani kumekuwa na malalamiko ya gharama za bei lazima iwe na usawa kwa TPDC na serikali hivyo kuwa na bei muafaka bila kuathiri mapato ya serikali.

Pia alitaka kuwepo kwa takwimu za viwanda vinavyohitaji gesi kwa muda mahususi kama siku, mwezi mpaka mwisho wa mwaka. Waziri alisema serikali katika mwaka huu wa fedha ilitenga Sh bilioni 20 kusambaza gesi asilia viwandani kwa mgawanyo katika gesi asilia iliyopo nchini ambayo ni trilioni 57.54 na matumizi katika viwanda vya mbolea na kemikali ni trioni 4.56 na viwanda vya vyuma trilioni 1.1.
 
Nini kinashusha bei za umeme, je uwepo wa umeme mwingi au gharama za umeme?
Au anataka kusema kwamba bei ya sasa ni kwa sababu ya 'scarcity' ya umeme?
Hawa watu ukiwasikiliza na hizi ngonjera zao unabaki kuwashangaa. Waliimba sana kwenye gesi ya mtwara na wakawaaminisha wananchi lakini baadae bila aibu wakasema kwamba kwenye ile gesi tumepigwa!!!Tumepigwa vipi na wahusika ni wao??????
Hakuna kitu hapa. Gharama za uzalishaji wa umeme wa Stigglers ziko juu sana na naamini feasibility study itakuwa imepanga na bei tayari kwahiyo hakuna jipya
 
Mtetea tu ndio umetoka kumalizana na jogoo, haraka ya kuanza kuhesabia idadi ya vifaranga sijui inatoka wapi! Kila jambo linakuja hatua kwa hatua, ni kutulizana tu mpaka mradi ufikie hatua ya uzalishaji ndipo haya yahusuyo punguzo la bei ya umeme yaje.
 
Wasambazie watu umeme vijijini ili Watanzania wote tufaidi walau keki hii ya Taifa, umeme usiwe wa watu wa mjini tu.
 
Shusheni bei ya umeme acheni siasa za kiki, kujiandaa kushusha ndio nini? Shusheni bei haraka na hatutawasifia maana mshatuumiza sana.
 
Mafuta,gesi,umeme,vinamchanganya.Hajui hata gharama zake.Na huyo ndio waziri mwenye thamana.
 
Back
Top Bottom