Maandalizi ya kulinda kura ni sasa, mjue CCM hawalali

Shocker

JF-Expert Member
Sep 15, 2012
1,930
3,803
Muanze na kuwasunda mawakala, wakala atakeuza utu wake ni hatari sana kwa jamii,mnaweza mkaona msimamizi ndio tatizo lakini hawa mawakala hasa wa upande wa Tanganganyika hurahisika zaidi kupokea donge nono, kisha siku ya uchaguzi anasepa au anajiteka, mjue CCM moja ya mipango yao ni kuwanunua hawa watumike kupika matokeo maana CCM wana mikakati miovu sana.

Hatua muhimu ni kudhibiti matokeo ya kura katika vituo na udhibiti ni pale kamanda aliekabidhiwa kuhakikisha kila kitu kimefika kwa wakati na hababaishwi na hongo na yupo in high alert.
 
Masikitiko yangu yapo kwa CHAMA CHA MAPINDUZI CCM, hivi kwanini wana tabia za kuiba kura?

Kwa nini viongozi wanataka kuongoza wananchi ambao hawajawapigia kura?

Kwa nini CCM ni wezi wa kura?
 
Ebu tuongelee hili suala katika muktadha wa maadili.

Kama CCM ya magufuli inaamini inakubalika, ni nini hasa kinawasukuma kuweka mipango ya kuiba kura?

Kwa uelewa wangu mdogo kupanga wizi wa kura ni dalili kwamba haukubaliki
 
Masikitiko yangu yapo kwa CHAMA CHA MAPINDUZI CCM.
hivi kwanini wana tabia za kuiba kura?

Kwa nini viongozi wanataka kuongoza wananchi ambao hawajawapigia kura?

Kwa nini CCM ni wezi wa kura????


Sizani lakini Kama itakuwa ni kweli kuwa wanaweza kufanya hivyo basi wajue ni makosa makubwa sana na ni machukizo makubwa sana mbele za MwenyeEnzi Mungu na mbele za Wanadamu!

Ikumbukwe huwa wanaapa kwa kushika vitabu vitakatifu vya Mungu !

Hasira ya Mungu isijeikawaka juu ya mtu au watu!

Kisasi cha Mungu kisije kushuka juu ya mtu au watu fulani!

Mungu anatisha jamani!

Mungu anaheshimu sana la upigaji kura wa watu kwaajili ya uchaguzi kupitia maandiko Matakatifu.

Actually nyakati kama hizi viongozi wa dini walipaswa kusisitiza swala la haki kufanyika kabla , wakati wa kupiga kura, zoezi la kuhesabu kura kuwepo na ushirikishwaji wa pande zote na uwazi na hatimae utangazwaji wa washindi.

Huu ndiyo wakati mmojwapo wa kuzungumzia ushiriki, uwazi, haki n.k.

Mungu anatisha sana!

Mungu ni wakuogopwa sana!

Ni wangapi leo hawapo ambao walikuwepo uchaguzi ulopita?!
 
Back
Top Bottom