Maandalizi ya kujifungua

majeshi 1981

JF-Expert Member
Dec 7, 2013
2,090
812
Wanajamvi ni mara yangu ya kwanza kusababisha mimba na mke wangu ana mimba ya miezi nane hivi, je nifanye maandalizi gani muhimu? Clinic tulianza kwenda tangu akiwa na miezi miwili.
 
Andaa hela
Begi la mama lenye vitu muhimu lipo
Hospitali mtakayojifungulia mpaka sasa natumaini mshaijua (unless iwe dharula)
Natumaini sio mwananyamala wala temeke maana hospitali zetu hizi manesi wanaweza kujuangalia macho tu
 
andaa hela
begi la mama lenye vitu muhimu lipo
hospitali mtakayojifungulia mpaka sasa natumaini mshaijua (unless iwe dharula)
natumaini sio mwananyamala wala temeke maana hospitali zetu hizi manesi wanaweza kujuangalia macho tu

asante , kunafaida na hasara gani kujifungulia private au hospitali ya serikali ukiacha suala la fedha?
 
Hongera sana mkuu..kikubwa mshukuru Mungu maana ni Jambo la kheri hilo...Mtoto hana gharama zaidi ya Upendo mkuu...
 
faida na hasara. Private hospitals mtoto akichelewa kutoka tu wanapenda sana operation, huwa si wavumilivu na ninafikiri operations kwao inalipa zaidi na inawapa mafunzo zaidi ya practical. Ila hospitali za serikali mkeo ataumia kwa uchungu sana na si rahisi kupigwa kisu hadi iwe necessary.

nashukuru , lakini nasikia hospitali nyingine za serikali hawajali!
 
La kwanza. acha tendo la ndoa till further notice.
La pili kwa mimba ya kwanza nakushauri uende Muhimbili. mtafute mmama mmoja mtip kitu kidogo na matokeo utayapenda.
La tatu hakikisha wife anakua happy. najua kipindi hiki ana mambo ya ajabu ajabu lkn mvumilie sana.
La nne nakutakia baraka na furaha ktk maisha ya ndoa.
Mwisho. kipindi hichi acha pombe hasa viroba na jitahidi kurudi home mapema.
 
Anza maombi yasiyokokma.Ni kipindi kigumu sana, shetani anapenda hizo sehemu si mchezo. Kuwa wa maombi na kimbilia Muhimbili nidyo mambo yote. Tunakuombea sana. Mungu akutie nguvu.
 
Back
Top Bottom