majeshi 1981
JF-Expert Member
- Dec 7, 2013
- 2,090
- 812
Wanajamvi ni mara yangu ya kwanza kusababisha mimba na mke wangu ana mimba ya miezi nane hivi, je nifanye maandalizi gani muhimu? Clinic tulianza kwenda tangu akiwa na miezi miwili.
andaa hela
begi la mama lenye vitu muhimu lipo
hospitali mtakayojifungulia mpaka sasa natumaini mshaijua (unless iwe dharula)
natumaini sio mwananyamala wala temeke maana hospitali zetu hizi manesi wanaweza kujuangalia macho tu
hongera sana mkuu..kikubwa mshukuru mungu maana ni jambo la kheri hilo...mtoto hana gharama zaidi ya upendo mkuu...
faida na hasara. Private hospitals mtoto akichelewa kutoka tu wanapenda sana operation, huwa si wavumilivu na ninafikiri operations kwao inalipa zaidi na inawapa mafunzo zaidi ya practical. Ila hospitali za serikali mkeo ataumia kwa uchungu sana na si rahisi kupigwa kisu hadi iwe necessary.