Maandalizi ya Kiusalama ya Ziara ya Obama Tanzania (na Afrika kwa Ujumla)


Evarist Chahali

Evarist Chahali

Verified Member
Joined
Dec 12, 2007
Messages
599
Likes
2,445
Points
180
Evarist Chahali

Evarist Chahali

Verified Member
Joined Dec 12, 2007
599 2,445 180
Washington- Rais Obama atapokwenda Afrika Kusini mwa Sahara mwezi huu, taasisi zenye jukumu la usalama wake hazifanyi lelemama.

Mamia wa mashushushu wa Kikosi cha Ulinzi wa Rais wa Marekani (US Secret Service) watasambazwa katika maeneo ya usalama huko Senegal, Afrika ya Kusini na Tanzania. Manowari ya Jeshi la Vita la Marekani inayotumika kubeba ndege za kivita au nyambizi, ikiwa na matabibu waliokamilika, itakuwa imeegeshwa pwani kwa ajili ya dharura.

Ndege za kijeshi za kubeba mizigo zitasafirisha magari 56, ikiwa ni pamoja na 'limousines' 14 na magari ya mizigo matatu yote yakiwa na makasaha ya vioo visivyopenya risasi vitakavyowekwa katika madirisha ya hoteli atakazofikia Obama na familia yake. Ndege za kivita zitakuwa 'zikizurura' angani kwa zamu, kuwezesha ulinzi wa masaa 24 katika 'anga ya Rais' ili ziweze kuchukua hatua pindi ndege ya adui itakapoingilia kati.

Maandalizi haya mhsusi ya kiusalama-ambayo yataigharimu Serikali ya Marekani makumi ya mailioni ya dola- yapo kwenye nyaraka ya siri iliyopatikana kwa gazeti hili (la Washington Post). Wakati maandalizi hayo yanaendana na mengineyo katika safari nyingine, nyaraka husika inatoa picha ya jitihada za hali ya juu katika kumlinda Amiri Jeshi Mkuu wa wa majeshi ya Marekani anapokuwa ziarani nje ya nchi hiyo.

Safari yoyote ya Rais, kama za wiki hii huko Ireland ya Kaskazini na Ujerumani, ni zina changamoto na gaharama kubwa kilojistiki.Lakini safari hii ya Afrika inakuwa ngumu zaidi kutokana na sababu mbalimbali, na inaweza kuwa yenye gharama zaidi kuliko zote katika utawala wa Obama, kwa mujibu wa watu walio karibu na maandalizi hayo.

Familia ya Obama inatarajiwa kutembelea nchi hizo tatu kuanzia June 26 hadi Julai 3 ambapo maafisa wa Marekani ndio watakaokuwa na jukumu la kuhudumia takriban kila kitu, badala ya kutegemea hudma za polisi, jeshi na hospitali katika nchi wenyeji.

Rais Obama na mkewe pia WALIPANGA KUFANYA ZIARA KWENYE MBUGA ZA WANYAMA ('SAFARI' kwa Kiingereza), ambayo ingehitaji kikosi cha kupambana na mashambulizi dhidi ya Rais kubeba silaha maalum zenye risasi maalum za kumudu kuwaangamiza duma, simba na wanyama wengine hatariu wa mwituni endapo wangekuwa tishio, kwa mujibu wa nyaraka hiyo

Lakini maafisa walisema Alhamisi kuwa ZIARA HIYO (YA MBUGANI) IMEAHIRISHWA [ NA HII NDIO SABABU ILIYOPELEKEA UZUSHI WA BAADHI YA MABLOGA KUWA ZIARA YA OBAMA KUJA TANZANIA IMEFUTWA] na badala yake imeandaliwa ziara ya kutembelea Kisiwa cha Robben pembezoni mwa pwani ya Cape Town, Afrika Kusini, ambapo Nelson Mandela alifungwa kama mfungwa wa kisiasa.

Gazeti hili lilipowauliza maafisa wa Ikulu ya Marekani (White House) kuhusu ZIARA YA MBUGANI ('safari') mapema mwezi huu,walisema hawajafikia uamuzi wa mwisho kuhusu suala hilo.Afisa mmoja wa Ikulu hiyo alieleza Alhamisi kuwa kufutwa kwa ziara hiyo ya mbugani hakukuhusiana na udadisi uliofanywa na gazeti hili hapo awali.

"Hatuna nyenzo zisizo na ukomo kufanikisha safari ya Rais, na tumeipa kipaumbele ziara ya Kisiwa cha Robben badala ya ziara ya MASAA MAWILI mbugani nchini Tanzania," alieleza msemaji Josh Earnest. "Kwa bahati mbaya, hatuwezi kufanya mambo yote mawili." [HEBU ANGALIA HAPA JINSI BLOGA HUSIKA ALIVYOCHAPIA SENTENSI HIYO NA HATA JINA LA MSEMAJI HUYO WA IKULU]

Nyaraka za ndani za kiutawala zilizosambazwa mwezi April zilionyesha kuwa familia ya Obama ilipanga kufanya ziarazote mbili- ya mbugani na kisiwani, kwa mujibu wa mtu anayefahamu maandalizi hayo.

Marais wa zamani, Bill Clinton na George W. Bush pia waliwahi kufanya ziara za mataifa mbalimbali ya Afrika, ambazo zilihitaji maandalizi magumu kama haya. Bush alikwenda mwaka 2003 na 2008, akiambatana na mkewe katika safari zote hizo. Mabinti wawili wa Bush pia walisafiri naye katika ziara ya kwanza, ambayo ilijumuisha 'safari' kwenye hifadhi ya wanyama katika mpaka wa Botswana na Afrika Kusini.

"Hata katika nchi zilizoendela za Ulaya ya Magharibi, kiwango cha huduma kinachohitajika kwa ajili ya ziara ya rais ni cha hali ya juu," alisema Steve Atkiss, ambaye alikuwa mwandaaji wa ziara akiwa msaidizi maalum wa hudma kwa Bush. "Kadri unavykwenda mbali zaidi, katika maendeo yenye maendeleo duni, kwa hakika ni changamoto ya kilojistiki."

Ikulu ya Marekani na Mashushushu wa Secret Service wamekataa kuzungumzia mipango ya kiusalama, na wasiaidizi wa kiutawala wametahadharisha kuwa maandalizi ya safari ya rais hayajahitimishwa.

Safari za nje za Obama zinakuja wakati taasisi za serikali, ikiwa pamoja na Secret Service, zinapambana na kukata matumizi kwa lazima. Walizni hao wa Rais walilazimika kukata dola milioni 84 katika bajeti yao ya mwaka huu, na mwaka huu Idara hiyo ilifuta ziara za wageni kutembelea Ikulu ya Marekani (kiutalii) ili kuokoa dola 74,000 kwa wiki ambazo ni gharama za watumishi kufanya kazi nje ya muda (overtime).

Taarifa nyingi kuhusu ziara za Rais nje ya nchi hufanywa siri kwa sababu za kiusalama wa taifa, na kuna ufahamu kidogo tu kwa umma kuhusu gharama za jumla. Ripoti kutoka Ofisi ya Uwajibikaji wa Serikali ilionyesha kuwa ziara ya Clinton barani Afrika mwaka 1998 alipozuru nchi sita iliigharimu Serikali ya Marekani angalau dola miloni 42.7.Kiwango hicho kilitumika zaidi na Jeshi, ambalo lilifanya safari 98 kusafirisha watendaji na magari,na kuandaa maendeo ya dharura za kimatibu katika nchi tano.

Kiwango hicho hakikujumuisha gharama za Secret Service ambazo zinachukuliwa kama siri.

Ziara ya Obama inaweza kugharimu kati ya dola milioni 60 hadi milioni 100 kwa kuzingatia gharama za safari za nyuma barani Afrika. Nyaraka ya Secret Service kuhusu ziara hiyo,ambayo ilionwa na gazeti hii, iliyowasilishwa na mtu anayeguswa na gharama za ziara hiyo, haikuonyesha Idara hiyo itatumia kiasi gani cha fedha.

"Miundombinu inayoambatana na ziara za Rais zipo nje ya uwezo wetu," alisema Ben Rhodes, Naibu Mshauri wa Usalama wa taifa wa Obama katika mawasiliano ya kimkakati. "Mahitaji ya kiusalama hayapangiw na Ikulu, hupangwa na Secret Service."

Maafisa wa zamani na wa sasa wa usalama wa serikali waliohusika na ziara za rais walibainisha kuwa watendaji wa Ikulu nao husaidia katika kuainisha mahitaji hayo, kwani hupanga sehemu za kutembelea na mipaka yake. Secret Service na Jeshi hufuatilia maandalizi hayo ya ziara yaliyowasilishwa kwao kwa kutaja mahitaji ya kiusalama.

Maafisa wa Ikulu ya Marekani wamesema kuwa dhamira ya ziara hiyo imekuwepo kitambo sasa, na itakuwa ya kwanza kwa Obama kama Rais kutembelea Afrika Kusini mwa Sahara licha ya 'kusimama' kwa masaa 22 nhini Ghana kwa msaa 22. Demokrasia changa zilizomo kwenye ratiba ya ziara hiyo ni washirika muhimu wa kiusalama katika eneo hilo, Rhodes alisema.

Obama atafanya mikutano na kila kiongozi wa nchi atakayotembela kwa minajili ya kujenga ushirikiano bora wa kiuchumi katika wakati huu ambapo China inawekeza vya kutosha barani Afrika. Pia atapigia mstari programu za afya, ikiwa ni pamoja na mapambano dhidi ya Ukimwi.

Mke wa Rais, ambaye alitembelea Afrika Kusini na Botswana bila ya mumewe mwaka 2011, atashiriki kwenye baadhi ya amtukio katika ziara hiyo. Hilo pia ni changamoto la kilojistiki kwa vile naye atahitaji maandalizi tofauti ya kiusalama kuhusu walinzi na magari, kwa mujibu wa nyaraka hiyo.

Msemaji wa Secret Service, Ed Donovan, alikataa kuzungumzia maandalizi ya ziara hiyo. "Siku zote huwa tunatoa kiwango stahili cha ulinzi kutengeneza mazingira salama," alisema.

Kwa mujibu wa nyaraka ya Secret Service, Obama atakaa siku moja Dakar, Senegal, siku mbili Johannesburg,Afrika Kusini, na siku moja Dar es Salaam, Tanzania.

KATI YA MAGARI 56 KWA AJILI YA ZIARA HIYO NI 'LIMOUSINES' KWA AJILI YA RAIA NA MKEWE , GARI MAALUM LA MAWASILIANO YA SIMU NA VIDEO, GARI LA KUZUWIA MAWASILANO YA RADIO KUZUNGUKA GARI LA RAIS, GARI LILILOJITOSHELEZA LA WA WAGONJWA (ambulance) AMBALO LINAMUDU MAABUKIZI YA KIBAIOLOJIA NA KIKEMIKALI NA GARI LA VIFAA VYA MIONZI YA X-RAY

Mashushushu wa Secret Service husafirisha magari kama hayo, pamoja na vioo vya kuzuwia risasi, katika ziara nyingi, ikiwa ni pamoja na zile za ndani ya Marekani, msemaji wa Ikulu alieleza. Lakini kwa vile kuna nchi tatu zinazohusika katika ziara hiyo, kunahitajika seti tatu za maandalizi hayo,kwa sababu hakuna muda wa kutosha wa kuhamisha vifaa, kwa mujibu wa nyaraka hiyo.

Mashushushu 100 wanahitajika kama 'waangalizi' - kumudu maeneo ya kumzunguka Rais- katika kila mji atakaozuru. 66 wanahitajika kumpokea Obama jijini Dar es Salaam. Kabla 'safari' ya Mbuga ya Taifa ya Mikumi haijaahirishwa wiki iliyopita, ziada ya mashushushu 35 ilijumuishwa kwenye maandalizi hayo ili kumlinda Rais, mkewe na mabinti zao wawili, kwa mujibu wa nyaraka hiyo.

Kadhalika, kati ya mashushushu 80 hadi 100 watasafiri na kufanya kazi kwa shifti kwa masaa 24, kwa ajili ya ulinzi wa Obama na familia yake, vikosi vya kupambana na mashambulizi (counterassault teams) na waandaaji wa lojistiki.

Nyaraka hiyo ya maandalizi ya ziara haionyeshi idadi ya mashushushu watakaohusika na ziara hiyo, japo baadhi watafanya kazi katika kituo zaidi ya kimoja.

Maafisa walisema Secret Service haitaki ziara ya Rais pasipo kituo cha hali ya juu cha jirani cha kukabili maradhi. Kitengo cha utabibu cha Ikulu hufanya maamuzi kuhusu hospitali gani Rais awapo ziarani nje ya nchi kinakidhi viwango, kwa kufanya ziara kwenye nchi husika, maafisa walieleza.

Katika nchi zinazoendelea, Jeshi la Majini la Marekani huweka 'hospitali inayoelea' kwenye manowari ya kubeba ndege au nyambizi, jirani.

"Hivi ndivyo inavyohitajika kuilinda taasisi ya urais wa Marekani," alisema Atkiss kuhusu mahitaji husika, "pasi kujali nani ni rais."

NIMEITAFSIRI HABARI HII KAMA ILIVYO KATIKA GAZETI LA WASHINGTON POST

 
manyimbo

manyimbo

JF-Expert Member
Joined
Dec 23, 2011
Messages
515
Likes
34
Points
45
manyimbo

manyimbo

JF-Expert Member
Joined Dec 23, 2011
515 34 45
umetafsiri au google imetafsiri?
 
Ngalikivembu

Ngalikivembu

JF-Expert Member
Joined
Oct 6, 2010
Messages
1,920
Likes
364
Points
180
Ngalikivembu

Ngalikivembu

JF-Expert Member
Joined Oct 6, 2010
1,920 364 180
Kwa mlolongo huu ina maana Rais wa Marekani hawezi kutembelea nchi kam Zambia ua Ethiopia ambazo hazina bahari ya kuweza kuegesha manowari yao.Kumbe ndio maana Rais wao hatembei ovyo kama walivyo maris wa Kiafrika ambao kila baada ya wiki huenda London, Washington au Brussels.

Thanks Mr Chahali.
 
Bavaria

Bavaria

JF-Expert Member
Joined
Jun 14, 2011
Messages
45,245
Likes
13,782
Points
280
Bavaria

Bavaria

JF-Expert Member
Joined Jun 14, 2011
45,245 13,782 280
1. Kwan wazungu wengine wanaoenda mbugani kutembea wanabeba snippers wasiliwe na wanyama?
2. Obama anakuja kufanya nini hasa? Utalii? Ziara ya kiuchumi?
 
M

Manhunt

JF-Expert Member
Joined
Apr 20, 2013
Messages
218
Likes
2
Points
33
M

Manhunt

JF-Expert Member
Joined Apr 20, 2013
218 2 33
Sawasawa nasikia vijana wa utalii Arusha wanapokea wageni wengi kipindi hiki tofauti na miaka iliyopita
 
B

bdo

JF-Expert Member
Joined
Nov 20, 2006
Messages
5,759
Likes
1,656
Points
280
B

bdo

JF-Expert Member
Joined Nov 20, 2006
5,759 1,656 280
Malimwengu! ninaogopa huko baadaye inaweza kuwa kasumba kwa viongozi wetu wanaweza hitaji gharama hizi hata watakapofanya ziara za namna hii huko Tandahimba au Arusha kisa hakuna amani, Mungu aepushe mbali, Obama bora usije
 
Sabayi

Sabayi

JF-Expert Member
Joined
Dec 4, 2010
Messages
2,321
Likes
83
Points
145
Sabayi

Sabayi

JF-Expert Member
Joined Dec 4, 2010
2,321 83 145
Very interesting hapa akija wang'oa kucha wetu wa Tiss watawekwa kando kabisa hata Fastjet atalindwa na hao secret service
 
K

Kifarutz

JF-Expert Member
Joined
Aug 7, 2012
Messages
1,743
Likes
69
Points
145
K

Kifarutz

JF-Expert Member
Joined Aug 7, 2012
1,743 69 145
Kwa mlolongo huu ina maana Rais wa Marekani hawezi kutembelea nchi kam Zambia ua Ethiopia ambazo hazina bahari ya kuweza kuegesha manowari yao.Kumbe ndio maana Rais wao hatembei ovyo kama walivyo maris wa Kiafrika ambao kila baada ya wiki huenda London, Washington au Brussels.

Thanks Mr Chahali.
Za JK ni za low cost but due to the frequency the overall cost equals Obama
 
Sabayi

Sabayi

JF-Expert Member
Joined
Dec 4, 2010
Messages
2,321
Likes
83
Points
145
Sabayi

Sabayi

JF-Expert Member
Joined Dec 4, 2010
2,321 83 145
Kwa mlolongo huu ina maana Rais wa Marekani hawezi kutembelea nchi kam Zambia ua Ethiopia ambazo hazina bahari ya kuweza kuegesha manowari yao.Kumbe ndio maana Rais wao hatembei ovyo kama walivyo maris wa Kiafrika ambao kila baada ya wiki huenda London, Washington au Brussels.

Thanks Mr Chahali.
Viongozi wetu wa Kiafrica hawana thamani kwasababu ya ufisadi wao na uzururaji wao ng'ambo kila siku so wala hawahitaji ulinzi
 
Transporter

Transporter

JF-Expert Member
Joined
Sep 26, 2011
Messages
774
Likes
105
Points
60
Transporter

Transporter

JF-Expert Member
Joined Sep 26, 2011
774 105 60
duh! Hawa majamaa bana ni noma ila ni kweli hakuna hospitali yenye hadhi ya obama hapa bongo??hahaha
 
mossad007

mossad007

JF-Expert Member
Joined
Dec 21, 2012
Messages
1,168
Likes
137
Points
160
mossad007

mossad007

JF-Expert Member
Joined Dec 21, 2012
1,168 137 160
Hii ndio USA taifa lenye nguvu duniani ziara yao ya siku moja bajeti ya wizara yetu kwa mwaka mzima!
 
Jalood

Jalood

JF-Expert Member
Joined
Dec 13, 2012
Messages
750
Likes
2
Points
0
Jalood

Jalood

JF-Expert Member
Joined Dec 13, 2012
750 2 0
Mgeni njoo wenyeji tupone. Au kinyume chake Mgeni njoo wenyeji tukome
 
B

Benno

JF-Expert Member
Joined
Nov 21, 2009
Messages
332
Likes
0
Points
33
B

Benno

JF-Expert Member
Joined Nov 21, 2009
332 0 33
Umeharibu maana, tafsiri yako sio kamili. Ungeweka tu english version
 
Papizo

Papizo

JF-Expert Member
Joined
Feb 24, 2008
Messages
4,655
Likes
441
Points
180
Papizo

Papizo

JF-Expert Member
Joined Feb 24, 2008
4,655 441 180
Daaaa kwa hiyo wale wachomoa kucha za watu TISS watakuwa hawana kazi hiyo siku au sio??kweli Marekani taifa kubwa...

Sent from my BlackBerry 9800 using JamiiForums
 
Root

Root

JF-Expert Member
Joined
Jan 23, 2012
Messages
29,723
Likes
17,352
Points
280
Root

Root

JF-Expert Member
Joined Jan 23, 2012
29,723 17,352 280
This is just sooooo nice I really love it
 
epson

epson

JF-Expert Member
Joined
Oct 1, 2012
Messages
534
Likes
118
Points
60
epson

epson

JF-Expert Member
Joined Oct 1, 2012
534 118 60
duu hu ugeni sasa kero, anakuja kutalii na vifaa vya kijeshi kama anakwenda kuipiga North Korea
 
W

WorstMare

Member
Joined
Mar 19, 2013
Messages
34
Likes
0
Points
0
Age
113
W

WorstMare

Member
Joined Mar 19, 2013
34 0 0
duu hu ugeni sasa kero, anakuja kutalii na vifaa vya kijeshi kama anakwenda kuipiga North Korea
Lol unafikiri hajui fitna zilizopo yeye mwenyewe haelewi what hell the ---- is going in!
 

Forum statistics

Threads 1,273,542
Members 490,428
Posts 30,484,610