Maandalizi ya Kambi za Ugaidi wa Kisiasa zimeanza Kitambo | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Maandalizi ya Kambi za Ugaidi wa Kisiasa zimeanza Kitambo

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by eedoh05, Aug 25, 2012.

 1. e

  eedoh05 JF-Expert Member

  #1
  Aug 25, 2012
  Joined: Apr 20, 2011
  Messages: 633
  Likes Received: 39
  Trophy Points: 45
  Habari za wana-magamba kuandaa vijana kwa ugaidi wa kisiasa hazijaanza leo. Nape anabaraguza tu, anapopinga kuwepo njama na mikakati hiyo. Ushahidi wa kuthibitisha hoja za mafunzo ya ugaidi wa aina hiyo ambao sasa umekua na kufikia kiwango cha kukaribia au kufanana na 'al shabab' au 'al qaida' ni mojawapo ya mahojiano na kijana mmoja aliyeamua kuokoka '(kuzaliwa mara ya pili)katika kipindi cha "This is my Story" kilichorushwa na ATN miezi ya nyuma. Kijana huyo alidai kwamba alifuatwa na kuombwa kujiunga na vijana wa chama cha magamba huko kilosa. Vijana hao walifundishwa kuhujumu matokeo ya kura wakati wa uchaguzi wa siku za nyuma.

  Kwa kuwa kila mwaka wa uchaguzi chama hiki kina kawaida ya kufundisha vijana kadhaa kwa kila wilaya wa kufanya hujuma katika upigaji kura na matokeo; na kwa sasa yamkini mafunzo yao yameboreshwa sana hadi kuwa ya kigaidi. kwa hiyo,kufikia sasa kuna jeshi kubwa kabisa la vijana hawa chini ya chama hiki.

  Wasi wetu, jeshi hili linaweza kutumiwa na ye yote kufanya cho chote, po pote, wakati wo wote ili mradi wahakikishiwe "MSHIKO" unaovutia. Kwa hiyo, ni kundi hatari hata kwa wana-magamba wenyewe. Hili ni suala la wakati tu, litatokea sio baadaye sana wala si karibu sana.Kila lisemwalo lipo ama..........
   
 2. M

  Mr.Busta JF-Expert Member

  #2
  Aug 25, 2012
  Joined: Mar 24, 2011
  Messages: 672
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Haya bana!
   
 3. Kurunzi

  Kurunzi JF-Expert Member

  #3
  Aug 25, 2012
  Joined: Jul 31, 2009
  Messages: 4,006
  Likes Received: 328
  Trophy Points: 180
  Hii dhambi wanayoifanya ni mbaya sana lazima itawarudia.
   
 4. N

  NYAMKANG'ILI JF-Expert Member

  #4
  Aug 25, 2012
  Joined: Apr 1, 2012
  Messages: 223
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  UKO SAWA KABISA. TENA unajua ubishi hauna maana kabisa, kwa sababu unafanya mtu aumbuke pale sasa watu wanapolazimika kuleta taarifa nyeti kabisa. HAYA SASA NATOBOA: mwaka 2010 wakati uchaguzi mkuu 'gaidi' mmoja MIONGONI MWA MAGAIDI 5 wa CCM alikamatwa URAMBO katika kijiji cha IMALAMAKOYE karibu na URAMBO mjini USIKU WA KUAMKIA SIKU YA KUPIGA KURA 31/10/10, huko magaidi walipelekwa na CCM TABORA baada ya maombi ya mgombea wa udiwani ktk kata ya IMALAMAKOYE kupitia CCM ndg GEMBE. MAGAIDI hao walitokea TABORA mjini. MAGaidi walikuwa wakiambatana na mwenyeji wao ambaye alikuwa akiwaonyesha watu wa kukamata, kutesa, kunyang'anya kiparata cha kupigia kura na pesa na mali nyingine (watu waliofanyiwa hivyo ni wale waliokuwa wamebainika na CCM kuwa hawawaungi mkono). MAGAIDI CCM walikuwa wakijitambulisha kuwa wametokea kikosi cha TAKUKURU MILAMBO TABORA (kitu ambaacho hakipo), na kwamba walikuwa wameletwa URAMBO kwa ajili ya kudhibiti rushwa na fujo. MWANANCHI MMOJA aliwashukitia, akajiuliza, "askari gani hawa waliovaa YEBO2?". WANANCHI WAKAWA na wasi2 nao, WANANCHI wa IMALAMAKOYE walitaarifiana kijijini, wakajikusanya USIKU na kumkamata mmoja kati ya magaidi hao watano aitwae JUMA, wakampa mkong'oto, wenzake walikimbia wakamuacha. BAADA ya kumkamata walitaarifu TAKUKURU URAMBO kwa simu, wakaja wakamkamata.

  NAKUMBUKA kipindi hicho mimi nilikuwa URAMBO kwa ajili ya uangalizi wa uchaguzi. GAIDI aliyekamatwa aliwasilishwa polisi na TAKUKURU na akafunguliwa kesi ya kujifanya afisa wa umma kinyume na sheria, KWA kujitambusha kuwa ni afisa wa PCCB kutoka MILAMBO TABORA. Taarifa nilizozipata hivi karibuni zinasema kuwa GAIDI huyo alipatikana na hatia na kuhukumiwa na MAHAKAMA YA HAKIMU MKAZI URAMBO kifungo cha miaka 3 jela bila faini.


  KUTHIBITISHA jinsi gaidi alivyo mtu wa CCM, nakumbuka jinsi viongozi wa CCM na MKUU WA WILAYA URAMBO BI ANNAH MAGOA (CCM walikuwa wanadai kuwa amevamiwa na wananchi wenye hasira hivyo aokolewe na wananchi ndio wakamatwe) walivyohangaika kuhakikisha wanapindisha sheria ili gaidi asikumbane na mkono wa sheria, walishindwa kwa sababu wananchi walisimama imara kuhakikisha hilo halitokei, kwani waliwanyanyasa na kuwanyang'anya mali zao.

  SASA NNAPE ANABISHA NINI?..., GAIDI alipohojiwa alisema amepata mafunzo ya kijeshi katika kambi za CCM na walifundishwa na vyombo vya dola, yeye ndiye alikuwa kamanda wa kikundi kilichokuja URAMBO na kulikuwa na vikundi vingine vilipelekwa maeneo mbali2 TABORA.
   
 5. Bornvilla

  Bornvilla JF-Expert Member

  #5
  Aug 25, 2012
  Joined: Feb 17, 2011
  Messages: 925
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 35
  Zanzibar habari hii sio mpya.Janjaweed imefanya madhambi makubwa Zanzibar.
   
 6. C

  CHOMA Senior Member

  #6
  Aug 25, 2012
  Joined: Aug 22, 2012
  Messages: 117
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Kinyozi hata kama akiacha nywele zake ziwe ndefu kiasi gani lazima itafika siku nae atanyolewa tu .Akikataa akiwa hai basi atakapofunga kauli atanyolewa atake asitake.
   
Loading...