Maandalizi ya halaiki ya sherehe za kuzima mwenge yagharimu shilingi milioni 100 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Maandalizi ya halaiki ya sherehe za kuzima mwenge yagharimu shilingi milioni 100

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Zimamoto, Oct 17, 2012.

 1. Z

  Zimamoto JF-Expert Member

  #1
  Oct 17, 2012
  Joined: Mar 28, 2012
  Messages: 464
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 33
  Maandalizi ya halaiki kwa ajili ya sherehe za kuzima mwenge yaliigharimu serikali kiasi cha shilingi milioni mia moja (mil 100). Pamoja na kugharimu kiasi hicho cha fedha ni dhahiri kuwa wanafunzi walioshiriki walikosa kushiriki kikamilifu katika masomo yoa. Cha kujiuliza ni; Je, matumizi makubwa kama hayo katika shughuli kama hiyo yana tija kwa taifa na wanafunzi ikizingatiwa kuwa ni wanafunzi hao hao kila siku tunasikia kilio cha madawati na huku serikali ikidai haina pesa!Source: Star TV, taarifa ya habari saa 2.
   
 2. s

  sung69 Member

  #2
  Oct 17, 2012
  Joined: Dec 9, 2011
  Messages: 21
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Nina ndugu yangu alikuwa kwenye kamati maandalizi ya sherehe ya kuzima mwenge anasema gharama ilikuwa M200 aachia mbali gharama za mzee dhaifu na watalii wenzake kwani kama unavyojua gharama zao huwa ni siri.

  Piga mahesabu gharama ya dawati moja ni shilingi ngapi then jaza mwenyewe ..........................how the so called mwenge unavyokula pesa bila sababu za msingi na ukiuuliza utaambiwa mwenge unaibua miradi....... miradi gani hiyo zaidi ya guest houses za wafadhili wa sisiemu.
   
 3. S

  Sheshejr JF-Expert Member

  #3
  Oct 17, 2012
  Joined: Jan 14, 2012
  Messages: 435
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Dah..! Hafu watoto wa halaik walioshirik kuuzma mwenge walihaidiwa posho na hawakupewa, imewabid waandamane leo!
   
 4. M

  Mjenda Chilo JF-Expert Member

  #4
  Oct 18, 2012
  Joined: Jul 20, 2011
  Messages: 1,425
  Likes Received: 63
  Trophy Points: 145
  Bado nasisitiza mwenge kama mwenge si kitu kibaya kama kitakuwa cha kitaifa, kila mtu akawa proud nao na ukahamasishwa na kuwa na nguvu kama enzi zile watu mnaline up toka asubuhi mwenge unapita jioni. Kila mtu alifundishwa jinsi ya kupokea mwenge na jinsi ya kuushika na maana juzi mtu akahoji iweje Mh. Rais akosee kuushika? kwa maana ya mkono wa kulia ni lazima uwe juu. Mwenge unabeba sehemu muhimu ya ideology na historia ya taifa hata kama ni symbol ya kusadikika. Mwenge ni sehemu ya utamaduni wetu, hata kama ulidurufiwa. Tatizo kubwa ni pale tunapotumia mwenge kwa mrengo wa kisiasa na si taifa kwa ujumla taking into acount of the curent political status . Ni gharama kweli, lkn bado ni kitu muhimu sana ambacho laiti kikitumiwa vyema kinaweza kurejesha utaifa wetu. kwani kuna ugumu gani kama makada ndo wawe makamanda wa mwenge kusiwe na uwakilishi wa vyama vyote? ili kuweka sura ya kitaifa? wawepo wa CDM, CCM, CUF nk, lkn tunaweza kuupa sura halisi ya kitaifa na kufuta kabisa muonekano kwamba mwenge ni kama vile ni wa chama tawala. Utaifa ni kitu muhimu sana coz hujenga umoja wa kweli, kujenga utaifa pia kuna gharama zake, hatuna tena nyimbo mpya za kizazi hiki za kujenga utaifa, ni ccm ni cdm ni kafu. Chama tawala kinatumia kila mbinu ili kibaki madarakani including mwenge na kuishia kuutoa hamasa na thamani yake. vijijini kwenye mikesha ya mwenge ni mashati na vitenge vya kijani pekee, badala ya kuunganisha unazidi kututenga. Lets redefine madhumuni ya mwenge actualy ni kuimplement na kuacha kuweweseka. Leo mtanzania akishika mwenge wa olympic atajisikia fahari sana lkn mtu huyohuyo anaweza asishawishike hata kuchungulia dirishani mwenge ukipita nje kwake. why? tubadilike.
   
 5. Nyanya mbichi

  Nyanya mbichi JF-Expert Member

  #5
  Oct 18, 2012
  Joined: Nov 10, 2011
  Messages: 3,197
  Likes Received: 1,328
  Trophy Points: 280
  serikali haina pesa
   
 6. Kakulwa P

  Kakulwa P JF-Expert Member

  #6
  Oct 18, 2012
  Joined: Feb 8, 2012
  Messages: 200
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga leo clouds fm (jicho la ng'ombe) anasema wanafunzi hawapashwi kudai hela maana walipewa suti za sherehe zenye thamani ya 30,000/- kwa idadi ya washiriki 650 hivyo wakipewa elfu 20,000/- kwa Taifa maskini hela karibu 13,000,000 ingetumika, waliwaita watoto ili wajitolee bure na wazazi wao wanajua pia (Nchi haina hela hiyo). Watoto anadai walipewa chakula na matunzo muda wa miezi miwili hivyo walikuwa kambini kwa ajili ya kula. Watoto wanadai walikunywa uji bila sukari na mchele bokoboko na walipoteza masomo kwa muda huo.
  Tujiulize kwa mapana bila ushabiki wowote, ilikuwa na haja gani kwa Halaiki ya watoto ambao wapo masomoni? Kwa nini wasingetumia majeshi ambayo kimsingi wapo kazini na mishshara yao ipo palepale? Hawa viongozi wa kitaifa kuanzia huyo Mkuu wa mkoa magari yao hayakujazwa mafuta walijitolea bure kama watoto?
   
 7. S

  SINDBARD Member

  #7
  Oct 18, 2012
  Joined: Oct 5, 2012
  Messages: 79
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mwenge hauna maana ni alama mojawapo ya miungu inayoendelea kuwadumaza na kuwadidimiza watanzania huku wanaouabudu wakinufaika maradufu katika nchi hii yenye rasilimali lukuki
   
 8. S

  Savannah JF-Expert Member

  #8
  Oct 18, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 238
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  mwenge ni ujinga mtupu.
   
Loading...