Maandalizi makubwa ya kumpokea kamanda millya yazidi kufana, vijana waapa kuvua magamba | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Maandalizi makubwa ya kumpokea kamanda millya yazidi kufana, vijana waapa kuvua magamba

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mbelwa Germano, May 22, 2012.

 1. Mbelwa Germano

  Mbelwa Germano JF-Expert Member

  #1
  May 22, 2012
  Joined: May 7, 2011
  Messages: 789
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Heshima Kwako,

  Katika hali ya kufurahisha vijana wa CDM jimbo la Lushoto wamepokea kwa furaha ujio wa Kamanda Ole Millya tarehe 24/05 na kuapa siku ya mkutano tarehe 25/05 itakuwa siku ya kutuma saalamu kwa chama cha mapinduzi kwamba upepo unaovuma Kilimanjaro, Manyara na Arusha sasa unaelekea Tanga na kuanzia Lushoto
  na kuvunja majigambo ya Magamba kwamba Mkoa wa Tanga ni ngome yao.

  Aidha wengi wameomba viongozi wa kitaifa kufika Lushoto kwani manaamini Lushoto ndio inaweza kuwa starting point ya kukubalika kwa CDM mkoa wa Tanga. Zaidi kilio chao ni kumuona Dr.Slaa akifika Lushoto kutokana na kushindwa kufika kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka 2010 kutokana na mabadiliko ya hali ya hewa.


  Nategemea kuwapa updates zaidi mpaka siku ya tukio.

  Nawakilisha.
   
 2. M

  Molemo JF-Expert Member

  #2
  May 22, 2012
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 13,287
  Likes Received: 580
  Trophy Points: 280
  Hongereni sana makamanda
   
 3. t

  thatha JF-Expert Member

  #3
  May 22, 2012
  Joined: Apr 29, 2011
  Messages: 15,234
  Likes Received: 179
  Trophy Points: 160
  Jamani huu nao ni kama usanii, huyu Millya kajiunga CDM juzi kajua lini falsafa, itikadi, sera na taratibu za cdm kiasi cha kuwa mjumbe wa kupeleka habari njema za cdm kwa watu wa lushoto. Huyu atulie akijue kwanza chama chake kipya na si kubuni safari za kutengeneza posho kwa kisingizio cha kwenda kuinadi cdm ambayo siamini kama anaijua vizuri.
   
 4. P

  Precise Pangolin JF-Expert Member

  #4
  May 22, 2012
  Joined: Jan 4, 2012
  Messages: 12,197
  Likes Received: 1,978
  Trophy Points: 280
  Mkuu alipokuwa CCM alikuwa anatumia muda mrefu kujifunza falsafa ya CDM ndio maana muda wote alikuwa akigombana na yule fisadi mtoto wa kwanza wa baba mwanaasha
   
 5. K

  Kiboko Yenu JF-Expert Member

  #5
  May 22, 2012
  Joined: Feb 12, 2012
  Messages: 312
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  hakuna habari hapa hili jukwaa linaanza kushuka heshima sasa
   
 6. S

  Sheshejr JF-Expert Member

  #6
  May 22, 2012
  Joined: Jan 14, 2012
  Messages: 435
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  kwani case? Pamoja na mambo mengine anaenda kuwaeleza wanalushoto uozo ulioko ccm, sababu ya yeye kuachana na magamba na kuwaeleza kuwa ni muda wa wanalushoto kuachana na ccm iliyowakandamiza kwa muda mrefu, n' mind you huko raia bado wana imani kias fulan na ccm.
   
 7. STK ONE

  STK ONE JF-Expert Member

  #7
  May 22, 2012
  Joined: Dec 31, 2011
  Messages: 628
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  It's a good move as far as ni katika hatua za awali za kuifanya CDM ikubalike Tanga....naamini hakuna chama tawala milele duniani, CCM WILL LASTLY GO!!!
   
 8. babalao 2

  babalao 2 JF-Expert Member

  #8
  May 22, 2012
  Joined: Apr 6, 2012
  Messages: 4,217
  Likes Received: 1,270
  Trophy Points: 280
  mabadiliko lazma watake wasitake watabadilika tu
   
 9. Mark Francis

  Mark Francis Verified User

  #9
  May 22, 2012
  Joined: Nov 19, 2010
  Messages: 605
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Namfananisha Ole Milya na mtume Paulo wa kwenye BIBLIA.... Mara baada ya kuongoka akaanza mara moja kazi mpya ya kumtangaza Kristo. Hata Ole Milya, baada ya Kuongoka kutoka utawala dhalimu wa CCM inabidi mara moja aanze kuitangaza CDM na sera zake nzuri.
   
 10. M

  MAMENGAZI JF-Expert Member

  #10
  May 22, 2012
  Joined: Dec 31, 2010
  Messages: 781
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
  Mapogolo, huyu anaonesha alikua anaisoma kimoyomoyo!!!! ameikariri CDM akiwa huko huko alikotoka.
   
 11. Marire

  Marire JF-Expert Member

  #11
  May 22, 2012
  Joined: May 1, 2012
  Messages: 11,420
  Likes Received: 259
  Trophy Points: 180
  Ni rahisi kueneza sera za cdm kuliko zilizoshidwa za ccm,hata nape akijiunga leo ni rahisi kunadi sera zetu kuliko za mafisadi.
   
 12. M

  Morinyo JF-Expert Member

  #12
  May 22, 2012
  Joined: Aug 26, 2011
  Messages: 2,472
  Likes Received: 463
  Trophy Points: 180
  Wakati mwingine chama kinaingia matatizoni kwa sababu ya haya makapi yanayopoteza uelekeo kisiasa na kuamua kujiunga na CDM. Mtu amejiunga juzi hata katiba ya chama haijaingia kichwani vizuri mnaanza kumpa sifa za ajabu. Nakumbuka 2010 kila alilokua analiongea Shibuda linaonekana kama lulu leo yakowapi. Katika kuimarisha chama ni vizuri kupokea wanachama wapya lakini hawa wanaohama baada ya kukosa vyeo ni wa kuogopa sana. Unaweza ukamuamini kumbe katumwa kwa ajili ya kuhujumu chama. Ukimpa sifa kama hizo halafu kesho ukagundua kua lilikua pandikizi wananchi utawambia nini.
   
Loading...