S.N.Jilala
JF-Expert Member
- Jan 26, 2012
- 540
- 507
Ninavyojua ni kwamba; ili kitu kiwe official kuwa huu ni wizi lazima Mahakama ihakikishe yaani iprove pasipo na mashaka yoyote. Kwa mfano nikija nyumbani kwako nikachukua kitu fulani haimanishi moja kwa moja kuwa Mimi ni mwizi mpaka mahakama ionyeshe mazingira ya uizi wangu. Nikirudi katika swala la Mchanga kusafirishwa Je, ni uizi huo au Sisi ndo tunakagua kila siku na kujiridhisha pasipo na shaka kuwa ule Mchanga wanatakiwa wausafirishe?. Kama tunaibiwa hata mamlaka zetu kuziamini karibu zote ni ngumu sana. Je, ni mfumo gani tutautumia kulinda rasilimali zetu?. Je, ni kweli ACACIA wanatuibia kimabavu au wanatumia sheria na Ujinga wetu kutuibia halafu ndo tunaanza kulalamika tuuuu.