Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Maana ya Ufisadi - Kutoka kwa Mwl. Lwaitama

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by MashaJF, May 16, 2011.

 1. MashaJF

  MashaJF JF-Expert Member

  #1
  May 16, 2011
  Joined: Nov 9, 2010
  Messages: 247
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  Nimeipenda hii kutoka kwa Mwalimu Lwaitama

  ----- Reply message -----
  From: "Azaveli Lwaitama"
  To:
  Subject: MPENDAZOE ASEMA NAPE ALISHIRIKI KUANZISHA CCJ
  Date: Sun, May 15, 2011 11:21 am

  Mimi nadhani ndugu zangu wanahabari tunasaidia kupindisha hoja juu ya dhana ya ufisadi...Kuwa na mshahara mkubwa au kuwa na kipato kikubwa ulichopata kwa makubaliano na waajiri wako au kwa juhudi zako halali au za ndugu zako si ufisadi...Kutembelea gari la kifahari ulilopewa au kuazimwa au kununua kwa kipato halali chako au ndugu yako... ilo pekee alikufanyanyi mtu kuwa fisadi...Ufisadi, kwa maana yenye mashiko kisiasa, ni kushiriki kwenye vitendo vya kupata kipato cha siri kama malipo kwa kutumia cheo chako serikalini au katika chama tawala kufanikisha malengo yakujitajirisha kinyume cha sheria ya mtu au kakundi ka watu..Sasa ndugu yangu Nape kusema eti Dr. Slaa naye ni fisadi maana yake ni nini kimantiki? Kama Dr. Slaa ni fisadi basi kwa vile tu Chadema wamempa mshahara mkubwa kwa cheo chake cha ukatibu wa chama taifa ( ambayo si sawa na kuwa mbunge wa jimbo moja!!!!) sasa CCM wanajivua gamba kwa nini yalabi? Kama hiyo ndiyo dhana ya ufisadi ya ndugu yangu Nape basi haina maana kusambabisha uwezekano wa mifarakano ndani ya CCM kwa kutaka mafisadi wake wajiuzuru....Wanyime tu mishahara mikubwa!!!!!Eti?!!!..

  Maana sasa kumbe ufisadi ni kupokea milioni 7 au hata 10 kwa kazi ya chama chako cha kisiasa kitaifa eti vile uliwai kusema wabunge wajimbo moja la watu wasiozidi milioni moja wasipate mshahara "mkubwa" wa milioni 7????!!! Hii inamantiki kweli??!!! Kashfa ya EPA, rada, Richmond...makashfa yenye harufu ya rushwa kubwa kubwa ya watu wenye madaraka makubwa makubwa serikalini, sasa yanalinganishwa na eti Dr. Slaa kulipwa mshahara wa milioni 7 au hata 10 kwa kazi ya ukatibu wa chama kitaifa chenye Wabunge na Madiwani na wafuasi kibao nchi nzima????!!!...Kweli kabisa hiyo ndiyo dhana ya ufisadi ya ndugu yangu Nape???

  Huyu ndiye Nape anayetaka mimi na wewe tumwamini kuwa anakisaidia chama cha wakulima na wafanyakazi cha CCM kijivue gamba??? Gamba la nini kama si matajiri wanaoajiri mamia ya wafanyakazi na hivyo ni wanyonyaji lakini wameteka chama cha wakulima na wafanyakazi badal ya kuanzisha chama chao cha liberal democratic union au republican??? Gamba la nini kama si wafanya biashara wakubwa wakubwa wenye kutuhumiwa ufisadi kama ule wa EPA, Richmondi na Rada??? ...Kumbe ndugu yangu Nape tafsiri yake ya ufisadi ni kule kuwa na mshara wa milioni 7 au hata 10...Ina maana Maximo aliye kuwa kocha wa TFF na Gavana wa Benki Kuu ni fisadi vile waanapokea/walipokea mshahara mkubwa tulio wapangia sie? Kweli ndugu huyu Nape anataka tumwamini kuwa ni mpambanaji dhidi ya ufisadi? Kwa nini tusiamini kuwa lengo la uteuzi wake ni kupotosha umma juu ya dhana mzima ya ufisadi ili baadaye kusiwepo hata mmoja hatayeondoka CCM kwa kutajwa kuwa fisadi??? Yaani ufisadi ndani ya CCM utaondoka kwa kuzunguka nchi nzima tukishutumu ufisadi wa Dr. Slaa wa Chadema??!!!Maana sasa CCM itakachoitaji kufanya ni kuchapisha nakala za malipo ya mishahara ya wote wanaotuhumiwa kuwa mafisadi, eti? Hapo kweli sasa mafisadi watabaki akina Dr. Slaa na Gavana wa Benki Kuu, na Mkurugenzi Mkuu wa TRA, siyo?Tuache utani bwana!!!!Nape? Unatukatisha tamaa sisi CCM wafu!!! Tulidhani kumekucha kumbe bado giza totoro?!!
  Wakatabahu,

  Mwalimu Lwaitama
   
 2. nsimba

  nsimba JF-Expert Member

  #2
  May 16, 2011
  Joined: Oct 7, 2010
  Messages: 785
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  hoja nzito, Nape itabidi atafakari upya, vinginevyo, atazidi kujidhalilisha!
   
 3. samora10

  samora10 JF-Expert Member

  #3
  May 16, 2011
  Joined: Jul 21, 2010
  Messages: 6,017
  Likes Received: 679
  Trophy Points: 280
  kama ana masikio na asikie.. somo/ufafanuzi/uchambuzi mzuri toka kwa mwalimu lwaitama!
   
 4. C

  Capitalist Senior Member

  #4
  May 16, 2011
  Joined: Feb 3, 2011
  Messages: 165
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Jamani msipoteze mda kuhusu huyu kilaza Nape hana jipya hata Makamba ana nafuu, juzi alikuwa Kijiji cha Ngamu Singida (v), hakuna cha maana alichoongea zaidi ya kumpaka Dr. SLAA eti Malaya, fisadi, ameasi kanisa, ooh aliba kura ndio maana ccm ilishuka....
  Mi namshangaa kwanza uchaguzi umepita lakini inaonekana Nape ndo kwanza ameanza kampeni... Mi nafikiri kazi anayotakiwa kufanya ni kukijenga chama upya kwa maana ya kutoa SERA ambazo zitawashawishi Wananchi kurejesha Imani kwa chama chake na sio kutoa porojo na matusi yasi na tija kwa taifa.
   
 5. Gsana

  Gsana JF-Expert Member

  #5
  May 16, 2011
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 4,081
  Likes Received: 73
  Trophy Points: 145
  Mwalimu Lwaitama,usihangaike na mwanaCCJ Nape. Uyu ni mtu mwenye uwezo mdogo sana kisiasa. Si mtu wa kulisumbua akili taifa. Bora mr makamba mpayukaji kuliko jasiri ujinga uyu.
   
 6. n

  ngurati JF-Expert Member

  #6
  May 16, 2011
  Joined: Feb 14, 2011
  Messages: 221
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  ninakushukuru sana mwalimu wangu Azaveli Lwaitama. Kila wakati najivunia kupita kwenye mikono yako kitaaluma.
   
 7. Smartboy

  Smartboy JF-Expert Member

  #7
  May 16, 2011
  Joined: Nov 12, 2010
  Messages: 1,110
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 135
  Natamani Shivji aliongelee hili, Nape is nothing
   
 8. THINKINGBEING

  THINKINGBEING JF-Expert Member

  #8
  May 16, 2011
  Joined: Aug 9, 2010
  Messages: 2,438
  Likes Received: 640
  Trophy Points: 280
  Elimu ya bure kwa nape.
  Ni hiari yake kuipokea ama kuiachia mbali na kuukumbatia ujinga wake.
   
 9. mhalisi

  mhalisi JF-Expert Member

  #9
  Oct 15, 2011
  Joined: Sep 9, 2011
  Messages: 1,182
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Wadau naomba kuuliza dr azaveli lwaitama anafundisha kozi gani udsm?

  Kwasababu naona ni dokta wa ukweli kwasababu amekuwa akialikwa kwenye mdidahalo mbalimbali inayozungumzia changamoto za nchi yetu.
   
 10. kingxvi

  kingxvi JF-Expert Member

  #10
  Oct 15, 2011
  Joined: Feb 11, 2011
  Messages: 883
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  kualikwa kwenye midahalo haimaanishi eti wewe ni dr wa ukweli yule ni mtu mwenye tamaa na wivu wa umaarufu
   
 11. bullet

  bullet JF-Expert Member

  #11
  Oct 15, 2011
  Joined: Oct 31, 2009
  Messages: 927
  Likes Received: 37
  Trophy Points: 45
  Anafundisha falsafa na kiingereza
   
 12. Kigarama

  Kigarama JF-Expert Member

  #12
  Oct 15, 2011
  Joined: Apr 23, 2007
  Messages: 2,476
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Tamaa na wivu wa nini au kuhusu nani? Lwaitama hata asingekuwa na PHD wengine tungemuita DK!!
   
 13. rosemarie

  rosemarie JF-Expert Member

  #13
  Oct 15, 2011
  Joined: Mar 22, 2011
  Messages: 6,689
  Likes Received: 464
  Trophy Points: 180
  Tuna wakina lwaitama wachache sana nchi hii'kumbuka wakati wa uchaguzi alivyokuwa akitoa analyist za siasa'ana akili timamu halafu ni msomi mzuri'
   
 14. only83

  only83 JF-Expert Member

  #14
  Oct 15, 2011
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 5,020
  Likes Received: 59
  Trophy Points: 145

  Una matatizo ya ubongo,huna uwezo wa kuhoji uwezo wa Dr Lwaitama hata kidogo na elimu yako ya shule ya msingi....nenda katibiwe kwanza ndio utoe comments hapa JF...
   
 15. Gosbertgoodluck

  Gosbertgoodluck JF-Expert Member

  #15
  Oct 15, 2011
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 2,867
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Umemaliza. Nilitaka nimjibu hivi hivi. Inawezekana hata shule ya msingi hakumaliza.
   
 16. L

  Luluka JF-Expert Member

  #16
  Oct 15, 2011
  Joined: Oct 6, 2011
  Messages: 628
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Afadhali mmenisaidia coz alishanitia hasira huyo anayedoubt elimu ya doct lwaitama!ana phd na amenifundisha commctn skills nikiwa first year UDSM. Ni m2 mwenye uchungu na hii nchi.
   
 17. kapotolo

  kapotolo JF-Expert Member

  #17
  Oct 15, 2011
  Joined: Sep 19, 2010
  Messages: 3,713
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 145
  Sio wewe ndio unamuonea wivu kwa kuwa ni Dr wa ukweli na ni timamu kuliko JK.

  Dr Lwaitama is a senior lecturer, Philosophy Programme (Unit), University of Dar es Salaam
   
 18. N

  NALO LITAPITA JF-Expert Member

  #18
  Oct 15, 2011
  Joined: Aug 25, 2011
  Messages: 255
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Aliwahi kunifundisha pl 111 ambayo ni argumentation criticalthinking
   
 19. N

  NewOrder JF-Expert Member

  #19
  Oct 15, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 463
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 45
  Umaarufu hautafutwi kwa kutumia akili vizuri. Hutafutwa na mtu anayejidhania kwanza anastahili kuwa juu lakini akikiri moyoni kuwa hapaswi kuwa juu. Hii ndio uleta msemo wa "desperate times call for desperate measures". Jiulize Dr. Juma Kapuya, Dr. Kigwangala, Dr. Mrema kwanini hawajaalikwa katika midahalo ya kichambuzi. Dr. Lwaitama anatofauti moja na wengine wote - ni jasiri na msema kweli hadharani. Huenda wengine hao ni wasema kweli lakini si jasiri wala hawawezi kusema vitu katika hadhara.
   
 20. Kimbunga

  Kimbunga Platinum Member

  #20
  Oct 15, 2011
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 12,489
  Likes Received: 1,228
  Trophy Points: 280
  Nilimkubali mwaka 1995 baada ya kutangazwa matokeo ya uchaguzi huko Zanzibar. Dr. Lwaitama alitoa uchambuzi pole Nkrumah hadi watu wakainua mikono juu na kuipiga piga kwa pamoja (makofi) mengi tuuuu. Mwenyekiti wa UDSM Philosophical Club!!
   
Loading...