Maana ya neno "CHAKACHUA"

Father Kianga

Member
Nov 1, 2010
6
0
NINAVYOFAHAMU MIMI

Neno "chakachua" tayari ni neno sanifu la kiswahili na lilianza kupata umaarufu baada ya EWURA kuanzisha kampeni kabambe ya kudhibiti vitendo vya kuchakachua mafuta hususani petroli.

Neno hilo linamaanisha kuchanganya kemikali (material) mbili tofauti au zaidi ili kupata kemikali nyingine tofauti, mara nyingi kwa lengo la kunguza ubora au ukali wa kemikali mojawapo au zaidi, branding kwa kiingereza.

Siyo kila unapochakachua unafanya kitendo hasi, unaweza kuchakachua kwa kufanya kitendo chanya.

Mifano chanya ya kuchakachua katika maana halisi:
(i)Ukipikia makaa ya mawe yasiyo chakachuliwa sufuria litatoboka kwani moto wake ni mkali mno lakini makaa ya mawe yanatumika kupikia kwa nchi zingine kama China baada ya kuchakachuliwa yaani kupunguza makali kwa kuchanganya na material zingine na kupata wanachoita coal briquettes, hapa kinachotoa nishati ni makaa ya mawe lakini material nyingine inapunguza nguvu ya nishata kwa kusharabu kiasi cha nishati ili chombo kama sufuria kisitoboke.

(ii)Kuchanganya kemikali yenge kutoa bio-fuel kama bio-gas (bi-ethanol) ilikupata brady itakayofaa kuendesha mitambo kama injini za magari yanayotumia gesi.

(iii)Kuchanganya maji ya matunda mabalimabali iil kupata radha inayokubalika zaidi au kemikali isiyo na madhara kwa matumizi ya binadamu, hapa tunda moja litakuwa maji yake yameondolewa ubora au makali yake ili mtu apate radha anayoipenda.

Mifano chanya ya kuchakachua katika maana halisi:
(i)Kuchanganya mafuta ya kuendesha mitambo kama petroli na kemikali zingine ili kuongeza ujazo na kupoteza ubora.

(ii)Kuchanganya dawa na chemikali nyingine ili kuongeza ujazo au tungamo, kama tunavyosikia kuhusu dawa badia za malaria kwa mfano, zile ambazo makali ya kemikali kiasili inayokua ghali yamepunguzwa kwa kuchanganya na kemikali zinazotibu lakini ni dhaifu na siyo aghali.

Ninaupungufu wa lugha lakini nadhani nimeeleweka vinginevyo tunaweza kulitumia neno hilo kama tupendavyo (hususani kwa mabo ya mzaha) kwani ni lugha yetu na lugha ina maanisha kusafilisha ujumbe, hivyo ikipidi tunaweza kukubaliana kubadilisha matumizi na kutumia maana inayokubalika zaidi kama ilivyo hivi sasa na mara nyingini ndiyo kukua kwa lugha.
 
Umenena vema na umeeleweka Father. Kuchakachua ni kitendo cha kuboresha au kudunisha kitu na kwa kufanya hivyo kuondoa uhalisia wa kitu husika. Neno hili limepokelewa na kukubalika na jamii ya kitanzania. Nadhani iliyobaki sasa ni kwa BAKITA kulipa ithibati.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom