Maana ya neno"bwege"kwa mujibu wa kamusi ya kiswahili sanifu

Mwaliga

Member
Jan 11, 2016
59
47
292548828ede9c9082bf17d1f5c13e4b.jpg
 
Ingia kwny kamusi ya kiswahili angalia maana ya neno bwege utaona tafsiri yake ni. . . .

"mtu asiye na akili sawa sawa, hafundishiki, mpumbavu"

Ebu fikiri japo kidogo mwanajf, maneno kama haya uyasikie mtu anayatamka kumwambia mama yako tena mbele ya watu, utajisikiaje?!.

Tatizo letu vijana wa leo.

Vijana wa leo kinachotughalimu kiasi cha kuishi maisha magumu ama kuonekana wajinga na elimu zetu hazitusaidii ni kukosa nidhamu.

Utamkuta kijana mtanashati anaelimu yake ya juu lakn mambo anayoongea au kufanya ni ya kipuuzi kiasi cha kila mmoja kumuona hana akili hata kidogo.

Ukimkuta kijana wa namna hii ukamweleza angalia umri, elimu na mazingira ya hicho ufanyacho, atakwambia kila mtu na maisha yake so fuata yake.

Vijana tunatakiwa tutambue kwmb dunia hii tunaishi na jamii na tunapaswa kufanya mambo kwa kuangalia jamii na si kufuata tu mihemko yetu.

Malezi ni tatizo kwetu.

Hata hapa jf ukimuona mtu anapenda sana kutusi wenzake jaribu kuchunguza malezi yake utaona yanashida au kama hayana shida basi anafanya vitu kwa mihemko akijiamini yeye yuko sahihi kwa kila jambo coz anaelimu ya kutosha.

Kijana yeyote yule mwenye social status hawezi kuwa mtu wa kutusi tu wengine eti kisa yeye anajua sana au anaelimu kubwa au pesa.

Angalia baba na mama yako jinsi walivyoishi vizuri na watu hapo mtaani kwenu, kwanini usiige hiyo tabia kijana mwenzangu.

Kijana inafika hatua unajiona mjanja kutukana watu wazima tena wenye nyadhifa kubwa ama ktk kijiji chenu au hata serikali za mitaa.

Jf admin alishajua kwmb hata humu ndani kuna watu wabwege ambao wao badala ya kujadili hoja wanafikiria kuwatukana wengine huku wakidhani wapo sahihi ndio maana baadhi ya nyuzi hufutwa humu na wakati mwingine wahusika huonywa.

Vijana wenzangu tuwe na heshima kwa watu wakubwa na wale tunaowazidi umri ili tuwe na nafasi nzuri kwao ktk mambo kadha wa kadha.

Hata kama hukubaliani nami ktk uongozi wangu lakn niheshimu maana heshima haiangalii unampenda mtu au kumchukia.

Mchuma janga hula na wakwao.

Sasa hivi ndugu jamaa na marafiki bila kuisahau familia yake ndio wanaumia moyoni kwa tendo la kukosa uadilifu, kukosa nidhamu kwa mtu mzima tena kiongozi.

Tunajifunza nini hapa.

Kijana mwenzetu kafanya ujinga kwa kumtolea maneno machafu kiongozi wetu sote bila kujali unamkubali au kumkataa, ni vyema nasi tukajifunza ktk hili.

Tunapaswa kutambua ya kwamba heshima sio kwa viongozi tu bali hata kwa watu tunaoishinao. Kama unaweza kumsemea maneno machafu mtu mzima tena mwenye nafasi kubwa ndani ya taifa hili how comes kwa wanaokuzunguka?!.

Mwl nyerere alishamweka mzungu mmoja ndani baada ya kusema. . . . "serikali ya tanzania nimeiweka mfukoni."

Just think simply.. . . !! Neno kuiweka serikali mfukoni lilitosha kumuweka mzungu ndani na alipotolewa alifukuzwa asionekani ndani ya 24hrs, tena hiyo ni baada ya kuombewa msamaha na baadhi ya viongozi ugaibuni.

Tujifunze kuheshimu watu vijana wenzangu, tusiwe watu wakujikosea heshima kiasi cha kila kijana kuonekana hana nidhamu kwa ubwege wa mtu mmoja.

Nikuulize swali mwanajf mwenzangu.

1. Ukikaa na watu wazima hasa baba na mama yako, wataridhia na kuona huyu kijana alichokifanya ni sawa?!.

2. Kama wataona si sawa kivipi baadhi yetu tunatetea ujinga aloufanya kijanamwenzetu badala ya kujifunza?!.

3. Kijana alokuzwa kimaadili anaweza kumtusi mtu mzima?!.

4. Wewe unaeshabikia hili na kuona liko sawa, unajua maana ya maadili?!.

5. Wakat umtoto mpaka sasa ulifunzwa kuwaheshimu unaowapenda au wote wanaokuzunguka?!.

Mithali 10:1

Mwana mwenye hekima humfurahisha babaye bali mwana mpumbavu ni mzigo kwa mamaye

Hitimisho.

Tusiwe wajinga wakuiga ujinga tukajifunga na kuitwa wajinga.

Tusifanye ujinga tukijifananisha na watu wengine maana kila mmoja ananafasi yake ktk jamii na kinga yake.

Tuheshimu ili tupate heshima.
 
uploadfromtaptalk1460812192085-jpeg.339262


Hapa akipatikana wakili makini hamuoni kuwa kuna neno ambalo masikioni halipendezi lakini ambalo linaweza kuamriwa kuwa si tusi na kesi hii ikawa imelipa "promo"?Je,hamuoni kutakuwa na uwezekano wa wengine kundelea kulitumia?
 
uploadfromtaptalk1460812192085-jpeg.339262


Hapa akipatikana wakili makini hamuoni kuwa kuna neno ambalo masikioni halipendezi lakini ambalo linaweza kuamriwa kuwa si tusi na kesi hii ikawa imelipa "promo"?Je,hamuoni kutakuwa na uwezekano wa wengine kundelea kulitumia?
mbona hapo tayari tusi tayari, labda aseme alikuwa amezidiwa na pombe wakati anaandika,
 
Kwa hiyo huyo Bwana anasema tunaongozwa na mtu asiye na akili sawa sawa (chizi/kichaa) acha akanyee ndoo kwanza iwe fundisho kwa wengine wanaoleta hasira zao kwenye mitandao
 
Mlidhalilisha kikwete kwa kumuita DHAIFU sasa kaja ngangari mtaisoma namba
 
chuki zingine hazifai kukikua hakuna haja ya kutukana angetoa tu yake ya moyoni bila lugha ya kuudhi na ndo maana wananchi walimgeuzia kibao
 
chuki zingine hazifai kukikua hakuna haja ya kutukana angetoa tu yake ya moyoni bila lugha ya kuudhi na ndo maana wananchi walimgeuzia kibao
Nani alimgeuzia kibao? Sema nyie msio fanya analysis ya issues. Ukiambiwa Mungu hayupo unasema amekufuru bila kuuliza kwa nini mtu anasema hivyo
 
Mlidhalilisha kikwete kwa kumuita DHAIFU sasa kaja ngangari mtaisoma namba
hukumu ya kesi hiyo hata kama mtuhumiwa atakutwa alitukana unaijua ? hivi mlalamikaji hapa ni nani , Dr Magufuri mwenyewe au polisi ?
 
Kuna kila ya dalili ya kufunguliwa kesi dhidi ya Rais mstaafu aliyekawaita watu fulani wapumbavu wakati wa kampeni kama mahakama itaamua kuwa ni tusi.Kazi kwao wanasheria.
 
Back
Top Bottom