Maana ya ndoto 12 kibiblia ambazo watu wengi huwa wanaota

kancher

JF-Expert Member
Dec 19, 2015
463
461
Ndoto ni muhimu sana katika ulimwengu wa roho. Tunapokuwa tumelala, miili yetu ndo inalala lakini roho zetu hazilali. Hivyo kunakuwa na mambo mengi ambayo yanakuwa yanatendeka katika ulimwengu wa roho.

Somo la ndoto ni somo pana sana na ni vigumu kuliandika nikagusia kila kipengele. Hivyo lengo la post hii ni kukupa mtaji ili uweze kuelewa maana ya baadhi ndoto chache ambazo umekuwa ukiota. Hii itakusaidia unapokuwa unaomba kwani unahitaji kuelewa unachoombea.

Kama nilivyosema mwanzo kuna ndoto za kutoka kwa Mungu (Matendo 2:17), ndoto za kutoka kwa shetani (Ayubu 7:14—15), na pia kuna ndoto ambazo ni matokeo ya shughuli nyingi. “Kwa maana ndoto huja kwa sababu ya shughuli nyingi” (Mhubiri 5:3).

Ndoto ambazo zinatokana na shughuli nyingi hazina madhara yoyote kwani ni akili tu ambayo inakuwa inarudia mambo yaliyotokea au yaliyokuwa yanaendelea katika fikra za mtu. Lakini ndoto za kutoka kwa Mungu au kwa shetani siyo ndoto ambazo ni za kupuuza. Lakini je utajuaje ndoto ya kutoka kwa Mungu au kwa shetani??

Ndoto huwa zimegawanyika katika makundi mbalimbali. Makundi makubwa mawili ni:

A. Ndoto ni mlango wa roho ya Mungu au ya shetani kuingia kwa mtu ambaye anaota. Tunasoma habari za Sulemani kuwa alipokea roho wa hekima ilikuwa kwenye ndoto (1 Wafalme 3:5—15). Mungu alimtokea Yakobo kwenye ndoto na kumwambia mataifa yote watabarikiwa kupitia yeye (Mwanzo 28:10—15).

Lakini pia tunasoma jinsi pepo alivyompitia Ayubu akiwa amelala (Ayubu 4). Hapa ndipo utapata lile kundi ambalo mtu anaona ndoto lakini kitu anaota kinakuwa kinaendelea katika ulimwengu wa roho.

B. Ndoto ni moja ya njia rahisi ambayo Mungu anatumia kuwasiliana na wanadamu. Zamani Mungu alikuwa anaongea na watu kupigia manabii lakini siku hizi Mungu anasema nasi kupitia Yesu Kristo (Waebrania 1:1—2). Mwandishi anaposema Mungu kusema nasi kupitia Yesu maana yake anasema nasi kupitia neno lake. Kumbuka “kusikia huja kwa neno la Kristo” (Warumi 10:17).

Kwa sababu watu wengi hawana neno, hawawezi kumsikia Mungu anaposema. Mungu anapotumia ndoto kuzungumza na mtu tafsiri yake ipo kwenye neno lake. Ndo maana hakuna ndoto ambayo unaweza kuota isiwe na jibu kwenye biblia. Iwe imetoka kwa Mungu au imetoka kwa shetani.

Njia pekee ya kuelewa ndoto zako zina maana gani, ni kuwa na neno la kutosha ili uweze kusikia sauti ya Mungu. Lakini pia kuwa unamuomba sana Mungu akupe karama ya kutafsiri ndoto. Mfano, unapoota ndoto juu ya mnyama fulani kama nyoka, inabidi uelewe nafasi ya nyoka katika ulimwengu wa roho baada ya Mungu kufanya uumbaji.

Ukiota ng’ombe anakukimbiza, inabidi uelewe ng’ombe anamaanisha nini kibiblia. Lakini pia kitendo kinachotokea kwenye ndoto nacho kinaweza kukuambia maana halisi ya ndoto. Mfano, ukiota unakimbizwa na nyoka na umeumwa na nyoka hizo ni maana mbili tofauti.

Zifuatazo ni ndoto ambazo huwa zinatokea kwa watu wengi. Tuangalie maana zake kibiblia.

1. NYOKA: Nyoka ni mnyama aliyelaaniwa kuliko wanyama wote (Mwanzo 3:14). Mungu alimwambia nyoka “nitaweka uadui kati yako na mwanamke, na kati ya uzao wako na uzao wake; huo utakuponda kichwa, na wewe utamponda kisigino” (Mwanzo 3:15). Hivyo kitu kikubwa nyoka anawinda kwako ni kisigino.

Nilishafundisha nafasi ya miguu katika ulimwengu wa roho. Kwa hiyo unaweza kuelewa kwa nini nyoka anawinda miguu. Hivyo nyoka anapokuwa anakukimbiza, lengo lake ni kukuponda kisigino ili apitishe roho fulani ya shetani. Kuna roho mbalimbali ambazo zinaweza kupita kupitia nyoka.

Roho Mtakatifu pekee ndiye anayeweza kukuambia ni roho ipi ilikuwa inapitishwa. Lakini ukiota nyoka amekuuma kabisa, maana yake ile sumu imeingia tayari katika mwili wako na tayari kuna roho fulani imepita kupitia ndoto.

Lakini pia ukubwa wa nyoka una maana. Mfano unapokimbizwa na nyoka mmoja wa kawaida tunaongea pepo. Lakini unapokimbizwa na nyoka wengi au uko mazingira ya nyoka wengi, tunaongelea jeshi la mapepo (Angalia Waefeso 6:12). Unapoota nyoka mkubwa kama Cobra au Python inasimama badala ya mfumo fulani wa kipepo.

Ukiota nyoka mmoja mkubwa mwenye vichwa 7 vita yako ni dhidi ya Lucipher mwenyewe, malaika aliyetupwa. “ikaonekana ishara nyingine mbinguni; na tazama, joka kubwa jekundu, alikuwa na vichwa saba na pembe kumi, na juu ya vichwa vhake vilemba saba” (Ufunuo 12:3). Ukiendelea kusoma utagundua huyu joka anayeongelewa ni shetani.

Hivyo kama unafatiliwa na nyoka usiku, katika maombi yako uwe unatamka pepo maneno kama “pepo nyoka ambaye...” Nakumbuka nilikuwa namuombea mtu fulani siku moja na Mungu akaonesha nyoka ameketi tumboni mwa mwanamke katika ulimwengu wa roho.

Sasa Mungu anapokuonesha, lazima umtoe huyo pepo specific. Wengi huwa wanasema tu “kwa jina la Yesu pepo toka.” Pepo yupi unamwambia atoke?? Mtu anaweza kuwa na pepo waliomfunga kihalali.

2. KUTUMBUKIA SHIMONI: “Rubeni akwaambia, Msimwage damu; mtupeni katika birika hii iliyopo nyikani, wala msimguse; ilia pate kumwokoa katika mikono yao, akamrudishe kwa baba yake” (Mwanzo 37:22).

“Basi wakamtwaa Yeremia, wakamtupa katika shimo na Malkiya, mwana wa mfalme, lililo katika uwanda wa walinzi; wakamshusha kwa kamba. Na mle shimoni hamkuwa na maji, ila matope tu; naye Yeremia akazama katika matope hayo” (Yeremia 38:6). “Na kwa habari zako wewe, kwa sababu ya damu ya agano lako, nimewatoa wafungwa wako katika shimo lile lisilo maji” (Zekaria 9:11).

Nimekupa mistari hiyo makusudi ile ikupe picha nini maana ya kuwa shimoni. Shimo inasimama badala ya kifungo ambacho wewe mwenyewe huwezi kujitoa mpaka msaada kutoka nje. Unapoota upo shimoni, inategemea nani alikutupa shimoni.

Kama umetumbukia mwenyewe, chimbuko la kifungo chako ni wewe mwenyewe. Kama rafiki zako au ndugu zako wamekutupa shimoni, maana yake wao ndo chanzo cha kukwama kwako. Kuna utofauti kuwa katika shimo lisilo na maji na shimo lililo na maji au matope.

3. CHAKULA: “Tena itakuwa kama mwenye njaa aotapo, kumbe anakua, lakini aamkapo, nafsi yake haina kitu” (Isaya 29:8). Siyo kila ndoto ya kula ni mbaya ila kuota ndoto unakula na watu huwafahamu au na wafu.

Chakula kina maana kubwa sana katika ulimwengu wa roho. Ndo maana kuna kiwango fulani ukifikia Mungu hawezi kukuruhusu ule chakula sehemu yoyote. Katika ulimwengu wa roho, unapokuwa unakula chakula unakuwa unafanya ushirika pamoja na wale unaokula nao. Wana wa Israel walipotengeneza mungu wa ndama walifanya nini?

Na Musa aliwafanyia nini? (Angaalia maandiko). Unadhani kwa nini Mungu anasema “Wala usingie ndani katika nyumba yenye karamu, kuketi pamoja nao, na kula na kunywa” (Yeremia 16:8). Sehemu zingine utaona Mungu anakataza “Usiingie ndani ya nyumba yenye matanga, wala usiende kuwaombolezea, wala kuwalilia” (Jeremia 16:5).

Kumbuka katika kitabu cha Jeremiah hii sura ilikuwa inalenga kundi fulani la watu. Hivyo haina maana usiende kwenye sherehe yoyote na kula. Ndo maana siyo kila ndoto ambayo unakula ni mbaya. Kinachofanya iwe nzuri au mbaya ni “je unakula nini na akina nani?” au “nani kaandaa chakula?” Kama unaota unakula na watu waliokufa, maana yake unafanya ushirika na wafu na maandiko yanakataza.

Kwenye suala la kula kwa ujumla siyo kila sehemu unatakiwa ule. Kuna watu ambao wana tabia ya kula kila sehemu. Kwenye misiba, kwenye sherehe, kwenye harusi, hata kwenye sherehe ambazo hawajaalikwa wao wanakula tu. Kabla hujala, hakikisha umepata kibali kutoka kwa Roho Mtakatifu juu ya chakula unataka kula.

Wengi wanaokula kwenye sherehe wakidhani wanakula chakula cha sherehe lakini hawajui maana yake katika ulimwengu wa roho. Ukiwa na neno, mambo haya yote biblia imeongelea. Mbaya ni wale ambao wanakula au wanalishwa nyama za watu au za nyoka katika ndoto. Hakikisha unaelewa maana yake.

Maana yake hicho ni kitu unafanya katika ulimwengu wa roho. Hakikisha unayajua madhara yake (Angalia maandiko yanasemaje juu ya nyama – Walawi, Romans, Mithali, 1 Timothy, Kumbukumbu na vingine vingi vimeongelea juu ya nyama). “Utakula, lakini hautashiba; na fedheha yako itakuwa kati yako nawe utahama, lakini hutachukua kitu salama; na hicho utakachochukua nitakitoa kwa upanga” (Mika 6:14). Pia angalia Hagai 1:6; Hosea 4:6. Je huwa unaota sana unakula??

4. SHULENI: Ukisoma kitabu cha Daniel utaona mfalme alitoa amri ili waletwe vijana wenye sifa fulani na kisha wapelekwe shule kwa muda wa miaka mitatu. Lengo la kuwapeleka shule ni ili kuwaandaa ili waje kusimama mbele ya mfalme (Daniel 1). Kwa hiyo shule inakuandaa kwa ajili ya ya hatua ijayo ya maisha. Mfano, ukiwa chuo, unakuwa unaandaliwa ili uweze kuwa na maarifa fulani. Kuna uhusiano mkubwa sana kati ya elimu na ndoto za shule.

Wengi huwa wanaota wapo madarasani au mazingira wa shule ambazo zipo kwenye level ambazo walishavuka. Mfano, wewe una familia yako unaota upo shule ya msingi. Unapoota upo darasani au mazingira ya shule ambayo ulishavuka, maana yake katika maisha yako, kuna eneo bado hujaivuka kimaisha. Mahali ulipo sipo unapotakiwa uwepo.

Ndo maana kama huwa unaota ndoto za namna hii, lazima kuna mambo fulani katika maisha yako ambayo hayaendi vizuri. Hivyo unapokuwa unaomba, unatakiwa uwe specific katika maombi na kujitoa huko katika ulimwengu wa roho. Kumbuka chanzo cha mafanikio yako ni ulimwengu wa roho, hivyo kama unaota upo level ya chini, maana yake huko ndipo ulipo.

5. KURUDISHWA NYUMBANI: Pia watu wengine huwa wanaota wanarudi nyumbani kwao. Mfano mtu anaota yupo kijiji ambacho baba au mama anatokea. Unapoota ndoto upo kwenye kijiji, hiyo inakuambia kuwa vita yako ya kiroho chimbuko lake ni huko. Mfano ukiota umeenda kijiji cha babu mzaa mama, maana yake chanzo cha kukwama kwako katika ulimwengu wa roho ni kwenye kizazi cha mama yako.

Hivyo yamkini kuna maagano ya kizazi cha mama ambayo utakuwa umeunganishwa kihalali au pasipo kihalali. Mungu anajaribu kusema na wewe ili uweze kutoka lakini wengi hawajui cha kufanya kwa sababu hawana neno. Ukiota ndoto ya namna hii, jiombee na kujitoa kwenye maagano na watu wa nyumbani kwenu.

6. KUFANYA TENDO LA NDOA AU KUFUNGA NDOA: Hizi ni ndoto mbaya haijalishi mazingira. Kuna watu wanaota wapo wanafanya mapenzi na wakiamka sehemu zao za siri zinakuwa kama walikuwa wanafanya tendo hilo. Maana yake hiyo haikuwa tu ndoto ila ni kitu ambacho kilikuwa kinafanyika kiuhalisia. Moja ya madhara ni kuleta matatizo sana katika ndoa. Tuchukulie katika hali ya kawaida. Mume akiwa na wanawake wengine wengi, hiyo ndoa lazima itakuwa ya shida sana.

Vivyo hivyo unapokuwa unaota ndoto za hivi, maana yake unakuwa unashiriki tendo la ndoa na mapepo katika ulimwengu wa roho. Mwingine anaota amefunga au amefungishwa ndoa na watu asiowajua. Maana yake katika ulimwengu wa roho, huyu mtu tayari yupo katika ndoa za kipepo.

Kama tayari uko katika ndoa na unaota ndoto za namna hii, lazima utakuwa na matatizo katika ndoa yako. Kama huwa unaota hizi ndoto, angalia jinsi ndoa yako ilivyo. Lakini kama hujafunga ndoa na unaota unafungishwa ndoa na watu huwajui, maana yake katika ulimwengu wa roho, tayari wewe una ndoa ya kipepo.

Moja ya madhara utayoyapata ni tatizo la kuoa/kuolewa au kuzaa. Haijalishi wewe ni mzuri kiasi gani lazima wanaume watakuwa wanakuja na kukuacha au wengine hawaji kabisa. Sababu ni kwamba unataka ufunge ndoa ya pili: ya Mungu huko uko kwenye ndoa ya miungu. Lazima kwanza uvunje ndoa ya miungu.

Hivyo katika maombi yako, tumia damu ya Yesu kuvunja ndoa, kufuta sahihi zote za kipepoe, unguza vyeti vya ndoa za kipepo kwa moto wa mbinguni, vua pete na utumie damu ya Yesu kusafisha kidole chako.

7. NDOTO ZA KUFA: Ndoto za kufa ni moja ya ndoto mbaya kuliko ndoto zote kwani zinakuambia kuwa roho ya mauti inakutafuta wewe au mtu fulani. Kwa wasomaji wa biblia mnajua kuwa mauti na kuzimu zinafanya kazi pamoja katika ulimwengu wa roho.

Hivyo roho ya mauti inapokuwa inakujia, kuzimu inakuwa tayari kukupokea katika ulimwengu wa roho. Ukiwa unaota ndoto hizi, kuna kipindi unakuta mawazo yako yote unawaza kifo.

Kuna watu ambao waliwahi kuota ndoto hizo na hawakuamka tena. Hujawahi kusikia mtu amekufa ghafla? Maana yake roho ya mauti imechukua maisha ya mtu huyo. Lakini kama unaota ndoto za aina hiyo haina maana itatokea kama kwenye ndoto, hapana. Inakuambia tu kuwa hiyo roho ya mauti inakutafuta.

Hiyo nimeeleza zaidi juu ya ndoto ya mauti kwa jinsi ya mwili. Ukisoma biblia pia mauti ya roho na mauti ya nafsi. Mauti ya nafsi maana yake kila unachoamua kinakufa na mauti ya roho maana mtu anaishi ila kibiblia amekufa (Ufunuo 3:1).

8. KUKIMBIZWA NA NGO’MBE: Tulishajifunza maana ya ndoto ya kukimbizwa na mbwa. Ngo’mbe ni tofauti na mbwa. Ukitaka kuelewa ndoto zinazohusu ng’ombe, soma habari za ndoto ya Farao katika kitabu cha Mwanzo 41 au muelewe ng’ombe katika maisha yetu ya kawaida. Unapoota ndoto ya ng’ombe, maumbile ya ng’ombe yana maana tofauti.

Tuchukulie katika uhalisia. Ng’ombe dume akikukimbiza akakumata atakufanya nini? Atakujeruhi kwa kukupiga kwa pembe au kichwa. Kumbuka biblia inapoongelea kujeruhiwa inaongelewa moyo au nafsi kujeruhiwa baada ya kubeba mambo fulani ambayo yanaumiza.

Hivyo ukijeruhiwa na ng’ombe kwenye ndoto, jeraha linaloongelewa ni la nafsi. “” Lakini pia unaweza kuota ndoto ya ng’ombe na ikawa na maana nyingine kutokana kile ng’ombe anataka kufanya.

Nakumbuka niliwahi kuota ndoto kuwa natakiwa nikate majani kwa ajili ya ng’ombe niwalishe. Kulikuwa na majani mengi sana halafu nikaona joka mkubwa sana mweusi akiingia kwenye yale majani ambayo natakiwa niende kukata kwa ajili ya kulisha ng’ombe.

Katika ndoto hii, majani ni neno chakula au neno la Mungu, ng’ombe ni watu na joka ni shetani. Joka alipoenda kwenye majani maana yake ni vita ambayo shetani ataileta wakati mimi naifanya kazi hii.

Lakini pia ukiota kwa mfano ng’ombe amezaa, au unakamua maziwa na mambo mengine, hizi ndoto zina maana tofauti kabisa. Hivyo ndoto za ng’ombe zinategemea na jinsi ndoto ilivyokuja kwani zipo ambazo zina maana baraka na zingine siyo za baraka.

Ila kwa ujumla ndoto za mafahari hao ni maadui. “Mafahali wengi wamenizunguka, Walio hodari wa Bashani wamenisonga. Wananifumbulia vinywa vyao, Kama simba apapuraye na kuunguruma” (Zaburi 22:12—13).

9. KUKIMBIZWA NA WATU: “Tazama, umenifukuza leo katika uso wa ardhi, nitasitirika mbali na uso wako, nami nitakuwa mtoro na mtu asiye na makao duniani; hata ikiwa itakuwa kila anionaye ataniua” (Mwanzo 4:14).

“Nanyi mtawafukuza adui zenu, nao wataanguka mbele zenu kwa upanga” (Walawi 26:7). “Matisho yatamtia hofu pande zote, na kumfukuza karibu na visigino vyake” (Ayubu 18:11).

Saul alipotaka kumuua Daudi, tunasoma kuwa “Hivyo Daudi akakimbia, akajiponya, akamwende Samweli huko Rama, akamwambia hayo yote Saul aliyomtenda” (1 Samuel 19:18).

Nimekupitisha kwenye hiyo mistari ili uone kuwa unapoota unakimbizwa na watu hii inakuambia juu ya maadui zako wa kimwili ambao unawaona katika ulimwengu wa roho.

Mara nyingi watakukimbiza lakini hawatakukamata. Wanaweza kuwa watu unaowafahamu wakati mwingine usiowafaham. Utaona katika maandiko, mtu aliyekuwa anakimbizwa, alikimbia ili kuikoa nafsi yake kutoka kwa adui wa mwili, siyo adui wa roho kama mapepo.

10. KUOGELEA: Siku moja niliota rafiki yangu mmoja yupo anaogelea kwenye mto na anaenda opposite na mkondo wa maji. Nilipoota hiyo ndoto, nilielewa kabisa kuwa ana mambo mengi sana yanamsonga na anahangaika. Kesho yake mimi nilichomwambia ni kwamba “naona una mambo mengi sana kwa sasa.”

Ndipo akaanza kuniambia mlolongo wa mambo yote anatakiwa kufanya. Lakini kwa sababu Mungu alishanionesha, nilichofanya ni kumuombea ili Mungu ampe nguvu aweze kufanya mambo yote. Watu hatukuumbiwa kuishi majini hivyo ukiota upo majini maana yake kuna mambo fulani katika maisha ambayo unapitia na unahangaika.

Lakini pia inategemea kama unaogelea kwenye swimming pool, baharini, au mto. Lakini pia kuna utofauti kati ya kuogelea kwa kutaka na kuogelea kwa kutotaka. Unapojipeleka mwenyewe kuogelea, chanzo cha mahangaiko ni wewe mwenyewe. Watu wengine wakikutupa majini ukaanza kuogelea, watu wengine ndiyo chimbuko la kile unahangaika.

Lakini kumbuka kuwa Mungu yupo pamoja nawe katika mahangaiko yoyote. “Upitapo katika maji mengi nitakuwa pamoja nawe; na katika mito haitakugharikisha; uendapo katika moto, hutatekea; wala mwali wa moto hautakuunguza” (Isaya 43:2).

Wakati mwingine unakuwa tu unavuka mto, au bahari, au dimbwi la maji. Maana yake kuna changamoto ambazo upo unazipitia lakini zinatofautiana. Ukiwa unaogelea na unataka kuzama, hapo maana ni tofauti. Kama miguu yako imezama kwenye dimbi la maji maana ni tofauti.

11. PESA: Tuchukulie katika hali ya kawaida. Je ukiwa unatembea ukaona hera njia, kwa mfano 10,000 Tshs utaichukua au utaicha? Jibu ni INATEGEMEA. Kabla hujaichukua lazima uhakikishe Roho Mtakatifu amekuruhusu uichukue. Unaweza kuchukua pesa kumbe ni sadaka ilitolewa kwenye kafara au ni sadaka imewekwa kwa ajili ya mapepo. Hivyo ukiichukua kuna kitu kitakupata.

Hivyo hata kwenye suala la ndoto za pesa ni hivyo hivyo. Ndoto ya pesa inategemea. Kwa mfano: watu wengine wanaenda kwa waganga wakienyeji halafu wanatoa sadaka. Halafu mganga anaweza kuchimba na kuzika zile pesa kama ishara ya kuzitoa kwa miungu.

Katika ulimwengu wa roho, zile pesa zinakuwepo kule. Sasa wewe kwenye ndoto unaota unachimba hera then unazichukua halafu zinakuwa haziishi. Je unapoamka nafsi yako inakuwaje?

Lakini pia kuna ndoto zingine ambazo Mungu anakuonesha mafanikio ambayo unaenda kuyapata kama ukiwa mtii Wa neno lake.

12. NDOTO ZINAZOJIRUDIA: Hizi ni ndoto ambazo mtu unakuwa unakumbusha kitu fulani kinachoendelea au kitachotokea katika maisha yako. Kuna ujumbe ambao Mungu anaweza kuwa anakuambia kwa kurudia.

Wengi huwa hawajali hata kama Mungu akiwaambia zaidi ya mara moja. “Kwa kuwa Mungu hunena mara moja, Naam, hata mara ya pili, ajapokuwa mtu hajali. Katika ndoto, katika maono ya usiku, Usingizi mzito uwajiliapo watu, Katika usingizi kitanani” (Ayubu 33:14—15).

Ndoto za kujirudia usizipuuzie kwani kuna ujumbe muhimu. Farao aliota ndoto mbili ila zenye ujumbe mmoja. Yusufu alimwambia “Na ndoto ya Farao kwa vile ilivyokuja mara mbili, ni kwa sababu neno hilo Mungu amelithibitisha, na Mungu atalitimiza upesi.

Hakikisha una tabia ya kuandika ndoto kama inawezekana kwani maono yanapokuja, lazima yatatokea kwa wakati ulioamuriwa (Habakkuk 2:2—3). Tutazidi kujifunza katika kundi letu la WhatsApp na kuangalia maandiko yanasema nini juu ya ndoto unazoota.

Ubarikiwe
 
Ndoto ya kushambuliwa na mbwa wa mtu mwingine ila nikawapiga wakaanguka chini wote na kuinuka wote ina maana gani?

Ndoto ya kusafiri kwa basi ila ulipofika njiani na kushuka kufanya jambo fulani ukajikuta basi imekuacha, ukaikimbilia bila mafanikio ina maana gani?
 
Mkuu mimi niliota naogelea mtoni (ruaha) na ikaonekana yale maji yamenizidi nguvu na kila kitu kifupi nlkw siwez kujitetea lakini kwa namna ya ajabu kabisa nilijiokoa mwenyewe baada ya kukuta sehemu pana udongo nikavukia hapo mpaka upande wa pili wa mto nikatokomea mtaani
 
Imebidi nisome pote kabisa na kwa umakini wa hali ya juu. Imeniongezea kitu, asante sana mkuu. Naona hapa karibia kila ndoto imenigusa.
 
Niliota doto nikiwa naaguka kwenye Simo kumbwa mara kidogo akatokea mhesimiwa rahisi watu akanishika mkono nisiaguke nadoto ikaishia hapo
 
Back
Top Bottom