Wakuu Kwema!

Mara kwa mara nimekuwa nikihamasisha vijana humu kuwa wasioe wanawake wasio na bikra kwani hao sio wake zao. Pia mwanamke usikubali kuolewa na mwanaume ambaye hajaitoa bikra yako, huyo sio mumeo.

Huyo sio mkeo kama hukukuta bikra na wala hukuitoa. Huyo ni mke wa uzinzi, na lazima upate matokeo ya uzinzi,

Mwanamke uliyemkuta bikra na ukaitoa ndiye mkeo, huyo ndio mliwekeana agano la kuwa mwili mmoja na roho moja na yeye na sio mwanamke ambaye hukuikuta bikra yake.
Mwanamke kama hukuitoa bikra yake ni lazima akumbuke wanaume wake wa zamani, ni lazima awe mzinzi na malaya. Usioe! Usikubali kujidharau wewe kama mwanaume kwa kuoa mtu ambaye sio mke wako, huko ni kufanya uzinzi.

Leo nitanukuu aya za mke wa ujana wako ambaye sharti awe na bikra, bikra ndio ujana au usichana wa mwanamke, bila bikra mwanamke ni mtu mzima, hawi tena msichana(kijana wa kike) yaani ni kusema umeoa mzee wakati wasichana wapo.

Katika nukuu hii nimekoleza sehemu muhimu
Malaki 2:14- 16
14Mnauliza, “Mbona sasa hazikubali?” Mwenyezi-Mungu hazikubali kwa sababu anajua wazi kuwa umeivunja ahadi yako kwa mke wa ujana wako. Umekosa uaminifu kwake ingawa uliahidi mbele ya Mungu kwamba ungekuwa mwaminifu kwake.
15Je, Mungu hakuwafanya nyote wawili muwe mwili mmoja na roho moja? Je, alikusudia nini alipofanya hayo? Yamkini alikusudia tuzae watoto ambao watamcha yeye. Kwa hiyo, hakikisheni kuwa hakuna hata mmoja wenu anayekosa uaminifu kwa mkewe.
16Mwenyezi-Mungu, Mungu wa Israeli asema: “Ninachukia talaka. Ninachukia mmoja wenu anapomtendea mkewe ukatili huo. Hakikisheni kwamba hakuna hata mmoja wenu anayekosa uaminifu kwa mkewe.”

Mambo ya msingi
1. Usipooa mwanamke asiye na bikra Mungu hasikii maombi yako, na ukitoa bikra usimuoe mwanamke uliyembikiri pia hasikii maombi yako.
2. Mwanaume ukimtoa bikra mwanamke mnakuwa mwili mmoja na roho moja. Lakini usipotoa bikra hamuwi wamoja na ndio maana ndoa za siku hizi zinaumiza pande zote mbili
3. Mungu anachukia talaka kwa mke uliyemtoa bikra.

Kiufupi ni kuwa Mungu hamtambui mkeo kama hukumkuta na bikra, anaona mnafanya zinaa.

Usioe mwanamke asiye na Bikra, usiolewe na mwanaume ambaye hakukutoa bikra.

Jokajeusi
Huu ni ukweli mtupu na unatakiwa kuungwa mkono na kila mwenye akili,vijana tunakosea sana linapokuja suala la kuoa.Unamkuta mtu humjui hata kwao akikwambia jina lake tu inatosha na unataka ule tu,aidha uondoke au ndio hivyo tena unaoa.Mkianza kupishana unaanza kumlaumu Mungu,kama tu kwenye mambo ya kwaida tunatumia muda kuulizia kwanini tuwe na papara kwenye kuoa na kuolewa?Tumwombe sana Mungu atusamehe na kuturehemu kwa tulioa,na wale ambao bado jifunzeni kwenye hili.Kusema ukweli mimi nimeoa,lakini kuukubali ukweli kuwa kuna mtu alimtoa bikra mke wangu inakera na kudhalilisha sana,yaani hata ukitaka kuona hilo mwulize tu mwanaume aliyemtoa bikra yupo wapi uone hasira zake.
 
kuna siku hapa nilisema....''mwanamke/msichana asie na BIKRA hapasi kutolewa mahari" , ni aibu iliyojificha katika tamaa zetu wanadamu.....but.....hao wenye bikra wako wapi.........????....
 
Huoni umuhimu wa bikra zama hizi wakati huo huo unaona ndoa nyingi zikipumulia mashine kisa na mkasa wengi wamechukua wake na waume wasio wao?

Hapa ndio utajua vijana wa siku hizi uwezo wao wa kufikiri upo chini, wanazidiwa hata na wanyama wa porini
@Jokajeusi hakuna kuimbe cha kuielew hii kitu bikra haiimarishi ndoa broo ni mtu mwenyew

utamtoa bikra akion huelewki anagawa kwingine
utamtoa bikla lkn usipo muelew unapiga chini

kuna matendo kabla ya tend na pia baada ya tendo kuna matendo


nimekuuliza je kwa walio tolewa bikla kwa misukosuko kam vile kubakwa huyu nae tunamuwek wapi!?
 
Joka mimi huwa nakuelewa sana, sema tu kuna viumbe humu wamegeuza mioyo yao kuwa migumu kama jiwe.

Bikra ni kila kitu katika ulimwengu wa Roho.
 
Joka kama joka hujazingatia ile note
Kipimo cha mwanamke mcha Mungu ni lazima awe na bikra, awe msafi,
Mwanamke akishakuwa ameitoa bikra yake kisha akaolewa na mwaname mwingine tayari yupo kwenye kundi la wanawake wachafu na najisi.

Kama angekuwa anamcha Mungu asingeitoa bikra kwa kuwapa wanaume ambao hawajamuoa
 
Wapi uliona kutongoza ikawa ni uzinzi?

Hakuna sheria inayomzuia mwanaume kutongoza, lakini ipo sheria inayomzuia asizini.

Mwanamke ndio hujitunza kwa ajili ya mwanaume na sio mwanaume ajitunze kwa ajili ya mwanamke
Safi kabisa. Tuje hapa.

Mithali 6:32 "Mtu aziniye na mwanamke hana akili kabisa, afanya jambo litakalomwangamiza nafsi yake." (Obviously anayeongelewa hapo ni mwanaume)

Andiko hilo hapo lakini cha ajabu wanaume wengi wanazini je kwanini wanazini? Na je unakubaliana na maandiko kuwa mwanaume anayezini na mwanamke hana akili kabisa?

Kwa maana hiyo basi ni kwamba mwanaume naye anatakiwa asizini! Which brings us back to my point kuwa kama ndiyo hivyo basi hata mwanaume anatakiwa ajitunze hadi ndoa!
 
Sasa wewe embu toa maana ya Neno Bikra na utupe mfano wowote kwenye dini yako kwa kunukuu maandiko ya kitabu chako unachokiamini, uonyeshe hata mtu mmoja wa kiume alishawahi kuitwa Bikra.

Wewe kama unaona tunajadili kwa mihemko, tupe hoja zako ili watu wazione na wakuelewe.

Kuhusu utafiti wa ndoa zenye amani, nimeshajitolea mimi mfano na ukoo wetu.

Nilitegemea utaleta hata maana ya bikra naona unatoa maelezo matupu.

Mwanamke mwema, mke bora ni lazima aolewe akiwa na bikra zaidi ya hapo ni majanga
Kwa kifupi tu ni kwamba virginity means purity. Kitu chochote ambacho hakijawahi kuguswa au kutumika na chochote basi hicho ni bikira hivyo kwa muktadha huu hapa mtu bikira ni mtu yeyote yule ambaye hajawahi kushiriki tendo la ndoa.

Mnachokosea ni kudhani kuwa mwanamke tu ndiyo bikira eti kwa sababu yeye amewekewa alama ya kile kimlango ambacho hufunguka anapokutana na mwanaume kwa mara ya kwanza na wengi kutokwa na damu! Bikira ni zaidi ya hicho kimlango na zile damu!

Hicho kimlango kinaweza kutolewa kwa sababu lukuki ambazo zinajulikana mfano mwanamke kuendesha baiskeli kupita kiasi nk! Je unataka kuniambia hicho kimlango kikitoka ndiyo tayari mwanamke anakuwa ameshapoteza bikira yake hata kama hajawahi kukutana na mwanaume?

Kwa mantiki hiyo unataka kuniambia mwanamke wa aina hiyo akikutana na mwanaume kwa mara ya kwanza asipoona kile kimlango au damu zisipomtoka basi yule mwanamke siyo bikira? Halafu kuhusu takwimu hauwezi kukurupuka tu kuja kusema umejitolea mfano wa wewe na ukoo wako wakati hii dunia ina watu zaidi ya billion 7!
 
Back
Top Bottom