Maana ya mto ngono na eneo la katerelo hayana uhusiano na tabia ya uasherati

mechard Rwizile

JF-Expert Member
Sep 21, 2011
1,571
873
Wakati Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wakati akihutubia wakazi wa Mkoa Kagera, alionyesha kuhusisha janga la ukimwi na tabia ya uasherati na kuonyesha kama lilikuwa janga la kujitakia. Alionyesha maneno "mto ngono" na neno "Katerelo" kuyahusisha na tabia ya uasherati. Leo hii kwa faida ya kila mtu aliyesikia na anaye husisha neno mto ngono na uasherati kufuatia neno la kishwahili la ngono kama tendo la kujamiana, aelewe maana halisi na aachane na upotoshaji. Nimeshawika kuelezea maneno haya na yalivyotokea katika lugha ya kihaya na maana yake.

Nianze na neno mto ngono; Mto ngono uananzia eneo linalo itwa lwamilinga, eneo lililopo wilayani Muleba, Mkoa wa Kagera. Mto ngono humwaga maji yake katika mto Kagera, ambao nao humwaga maji yake ndani ya Ziwa Victoria. Ziwa nalo humwaga maji kwenye mto Nile kabla ya kuinufaisha bahari ya Mediterranean.

Katika mto ngono kuna aina fulani ya mimea inayotambaa, nayo inaitwa "omugono". Mimea hiyo hutumika kutengenezea aina fulani ya mitego ya samaki. Wingi wa "omugono" ni "engono". Hivyo ndivyo unavyoitwa mto ngono na watu wa eneo letu. Kwa maana hiyo neno ngono halina uhusiano na tendo la kujamiiana kama rais anavyotaka ifahamike. Hakika akutukanae hakuchagulii tusi.

Katerelo ni eneo lililopo katika wilaya ya Bukoba Vijijini karibu na bandari ya Kemondo. Hapo palikuwa makao makuu ya tarafa. Tarafa ya Katerrlo wakati wa utawala wa kikoloni ilikuwa ndio makao makuu wa chifu wa eneo linaloitwa Kianja. Utawala wa machifu ulikuwa unaendeshea shughuli za kiutawala hapo na hadi leo hii jengo lililokuwa likitumiwa na chifu bado lipo. Hukumu zilitoleewa hapo na adhabu halikadhalika. Moja ya adhabu hizo zilikuwa ni kuwachapa wahalifu viboko. Kwa maana hiyo kila aliyeshitakiwa na kuitwa, alijua eneo hilo ndipo wanapochapiwa. Kwa kihaya neno kupiga ni "kutela" na eneo wanapotolea adhabu ya kuchapa viboko ni "Katerelo". Kwa maana halisi neno hilo halina uhusiano na mtindo wa kufanya mapenzi kama ambavyo rais wa nchi anataka watu waamini.

Nihitimishe kwa kusema lugha ya kishwahili imeundwa na maneno ya kibantu na lugha ya kihaya ni lugha ya wabantu. Isishangaze maneno kuingiliana na hata kama yana maana tofauti. Kwa mfano; wanyakyusa wanatumia neno "mwagona" likiwa na maana ya salamu, wakati katika lugha ya kihaya neno wagona lina maana ya "kukoroma"
 
Asante sana mleta mada kwa kuwa tayari kutumia muda wako kwa kuelimisha jamii yetu. Safi sana.

Binadamu wanatofautiana sana, na aliyetuumba na kutupa uwezo wa kutofautiana alifanya hivyo akiwa na lengo jema.

JK anaweza kuongea katika hali ya utani na ikaeleweka kuwa anaongea utani. Mwalimu JKN alikuwa na uwezo huo kwa kiwango cha juu sana.

BWM na Mzee AHM hawakujaliwa utani, sio sehemu ya roho zao au silka walizozaliwa nazo. Huyu wa sasa pia hana silka ya utani ambayo ni ya asili kama walivyokuwa JKN na JMK. Analazimisha silka hiyo ili aonekane ni mtu mwenye uwezo wa kujichanganya na jamii ya kila kona ya nchi.

Ndio maana hukimbilia katika taratibu za maongezi za kusalimia kwa kutumia lugha za makabila, anajaribu kuonyesha a light side of him as a leader.

Sio dhambi kuchomekea maneno ya utani, hata kama mtu anaongea na waliofiwa. There is life even after some dark days of a certain society. Ndio maana utani na vichekesho huendelea kuwa sehemu ya maisha ya watu wa majimbo ya kusini ya Marekani, ambayo hushambuliwa sana na vimbunga vya hatari.

Tunajaribu kukuza sana maneno ambayo kwa wenzetu ni just a part of a light mood. Tunajaribu kujifanya kama tunao uchungu sana wa maisha kuliko binadamu wenye maendeleo ya kweli kuliko sisi!.

Katerero, Mto Ngono, Ruterangoma ni maneno yaliyotamkwa katika hali ya masikhara, na hakuna mwanadamu mwenye kuweza kuishi bila ya kuwa na dakika za utani na masikhara. Watanzania, hii tabia ya kulalamika hovyo, zaidi ya kutuzeesha na kutufanya tuonekane ni watu wenye nongwa, haina faida nyingine za ziada.
 
Ila ktk tafsiri ya pili kuna kitu kinashabiana kabisa na uzushi huu wa pwani
 
utani gani huo ambao anauelewa yeye tu na ummy mwalimu? anyamazege tu!
 
Kwa kijana , kupiga au kuchapa, kupigiwa au kuchapiwa yanaenda huko huko sawa na kutela
 
Kusema ukweli aliwakosea mno watu Wa bukoba na wanakijiji cha katerero kyetema
 
Wakati Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wakati akihutubia wakazi wa Mkoa Kagera, alionyesha kuhusisha janga la ukimwi na tabia ya uasherati na kuonyesha kama lilikuwa janga la kujitakia. Alionyesha maneno "mto ngono" na neno "Katerelo" kuyahusisha na tabia ya uasherati. Leo hii kwa faida ya kila mtu aliyesikia na anaye husisha neno mto ngono na uasherati kufuatia neno la kishwahili la ngono kama tendo la kujamiana, aelewe maana halisi na aachane na upotoshaji. Nimeshawika kuelezea maneno haya na yalivyotokea katika lugha ya kihaya na maana yake.

Nianze na neno mto ngono; Mto ngono uananzia eneo linalo itwa lwamilinga, eneo lililopo wilayani Muleba, Mkoa wa Kagera. Mto ngono humwaga maji yake katika mto Kagera, ambao nao humwaga maji yake ndani ya Ziwa Victoria. Ziwa nalo humwaga maji kwenye mto Nile kabla ya kuinufaisha bahari ya Mediterranean.

Katika mto ngono kuna aina fulani ya mimea inayotambaa, nayo inaitwa "omugono". Mimea hiyo hutumika kutengenezea aina fulani ya mitego ya samaki. Wingi wa "omugono" ni "engono". Hivyo ndivyo unavyoitwa mto ngono na watu wa eneo letu. Kwa maana hiyo neno ngono halina uhusiano na tendo la kujamiiana kama rais anavyotaka ifahamike. Hakika akutukanae hakuchagulii tusi.

Katerelo ni eneo lililopo katika wilaya ya Bukoba Vijijini karibu na bandari ya Kemondo. Hapo palikuwa makao makuu ya tarafa. Tarafa ya Katerrlo wakati wa utawala wa kikoloni ilikuwa ndio makao makuu wa chifu wa eneo linaloitwa Kianja. Utawala wa machifu ulikuwa unaendeshea shughuli za kiutawala hapo na hadi leo hii jengo lililokuwa likitumiwa na chifu bado lipo. Hukumu zilitoleewa hapo na adhabu halikadhalika. Moja ya adhabu hizo zilikuwa ni kuwachapa wahalifu viboko. Kwa maana hiyo kila aliyeshitakiwa na kuitwa, alijua eneo hilo ndipo wanapochapiwa. Kwa kihaya neno kupiga ni "kutela" na eneo wanapotolea adhabu ya kuchapa viboko ni "Katerelo". Kwa maana halisi neno hilo halina uhusiano na mtindo wa kufanya mapenzi kama ambavyo rais wa nchi anataka watu waamini.

Nihitimishe kwa kusema lugha ya kishwahili imeundwa na maneno ya kibantu na lugha ya kihaya ni lugha ya wabantu. Isishangaze maneno kuingiliana na hata kama yana maana tofauti. Kwa mfano; wanyakyusa wanatumia neno "mwagona" likiwa na maana ya salamu, wakati katika lugha ya kihaya neno wagona lina maana ya "kukoroma"

Baada ya ile kauli ya raisi kuhusu mto ngono na Katerero niliwaza sana wakaazi wa maeneo hayo wanajisikiaje. Nadhani watakuwa hawana tena hata uhuru wa kusema "mimi natokea Katerero au kando kando ya mto ngono". Ingekuwa burasa huyu raisi awaombe radhi wakaazi wa maeneo hayo kwa kuwafanyia udhalilishaji kwa kauli zake. Asipo fanya hivyo historia itamhukumu
 
Back
Top Bottom