Maana ya maendeleo ya nchi yaanzia kwa mtu mmoja mmoja

Sky Eclat

JF-Expert Member
Oct 17, 2012
57,597
215,272
Maendeleo ya nchi yanaanzia kwa mtu mmoja mmoja. Elimu, afya, dini, mila, ajira, mazingira anayoishi, na upatikanaji wa habari. Elimu ina beba mwongozo mzito katika haya mengine kwani elimu nzuri itamsaidia mtu kupata ajira nzuri, kuwa na uwelewa wa kutunza afya yake, kuboresha mazingira anayoishi, na kupata habari itakayo msaidia kuelewa dunia inakwendaje na pia ubongo wake kuendelea kuchangamka.

Serikali ni jukumu lake kuimarisha miundo mbinu. Kama jamii itakosa maji safi na salama ni rahisi kupata magonjwa mlipuko. Gharama za kutibu magonjwa hayo ni mzigo wa ziada kwa serikali. Hata mazingira unayoishi yakiwa mabovu yanarudisha nyuma maendeleo. Ukilima mazao ukose barabara ya kupeleka mazao sokoni kunakuletea umasikini.

Dini na mila vinachangia kwa kiasi kikubwa maendeleo ya watu. Dini na Mila vinaleta umoja na mshikamano.

Ukitaka kudumaza akili ya mtu, chagua habari ya kumpa. Ukimfahamisha maisha ni ujamaa, ataamini hivyo kuwa hakuna maisha mengine tena.

Ukitaka kujua kama taifa lina maendeleo angalia
Idadi ya vifo kwa mwaka, idadi ya wasio na ajira, Aina ya nyumba wanazoishi na barabara zao. Hizi ndiyo alama kubwa za maendeleo.
 
Back
Top Bottom