Maana ya maendeleo ni nini? Mfano wa Mafia

bagamoyo

JF-Expert Member
Jan 14, 2010
21,283
24,155
MFANO WA MAFIA, TANZANIA
kwa Professor Patricia Caplan, BA, MA, Ph.D. Goldsmiths College, University of London

Hotuba hii imetolewa tarehe 11 Agosti 1994 Lizu Hotel, Kilindoni, Mafia
Imetayarishwa na Changia Maendeleo Mafia (Chamama).



MAANA YA MAENDELEO NI NINI? MFANO WA MAFIA
DIBAJI

Naona nimepewa heshima kubwa kuweza kupata nafasi ya kuw ahutubia watu wengi kama hivi wakiwa na nyadhifa tofauti, leo hii. Pamoja na kunipatia nafasi hii, mimi bado napata wasiwasi kidogo kuongelea maendeleo ya Mafia hasa mimi nikiwa si Mtanzania.

Isitoshe, watu wengi wa Mafia wameniita mara nyingi mimi mwenyeji. Nashukuru kwa heshima hiyo tukufu.

Heshima hiyo, pia, imenifanya mpaka mimi nione Mafia kama mji wangu wa pili, ambao imejaa wazazi wangu, ndugu zangu, dada zangu, kaka zangu, akina babu na bibi zangu, na marafiki zangu.

Miaka 29 iliyopita tangu nifike Mafia mwaka sitini na tano, nimeweza kujifunza mambo mengi, na watu wamekuwa
tayari kunifundisha mambo mengi, lakini kila mara, naona bado yapo mengi ya kujifunza na kwamba nahitaji
muda zaidi. Na huenda, kwa bahati mbaya, mengine sikuyajua vizuri, nadhani mtanisamehe.

Nimeamua kuzungumza kwa Kiswahili na nadhani mtakubaliana nami kuwa Kiswahili changu si kizuri sana lakini
mtakuwa radhi kunivumilia na kunisikiliza.

Baada ya hayo, machache, naomba sasa tuingie katika maada maalum nitakayoizungumzia leo hii.

MAANA YA MAENDELEO NI NINI ?​
Sifikiri kama tunaweza kuyapima maendeleo kwa wingi wa mahoteli makubwa au kwa wingi wa vyupa vya
soda, au wingi wa magari waliyonayo matajiri.

Maendeleo hasa maana yake ni kama yafuatavyo:
  • Kwanza ni afya na ustawi wa jamii ya watu.
  • Pili ni Elimu.
  • Tatu ni mishahara inayofaa
  • Nne kuinuka kwa hali ya maisha na upatikanaji rahisi w a mahitaji ya lazima.
Vipi tunaweza kupata maendeleo?
  • Yatubidi tufikirie mambo muhimu ambayo tunaweza kuyatumia katika kuipata maendeleo, kwani kila kitu ni
  • Nyenzo ya maendeleo kw a pale pahali kilipo.
  • Yatubidi kuheshimu na kutumia maamuzi walionao watu wetu, kwani wao ndio wataalamu zaidi wamaeneo wanayotoka.
  • Yatubidi kuwasikiliza wanayosema na kuzingatia wanayohitaji kwa maisha yao, iIi kuwepo na urahisi wa kuweza kufanya katika mendeleo. Kwa kifupi maendeleo huanza chini, na hayawezi kuletwa
kutoka juu. Hii haina maana ya kwamba katika maendeleo hakuhitajiki maelekezo kutoka juu, wataalamu kutoka nje, au ufundi kutoka mbali. Inawezekana lakini yatupasa tuwe waangalifu jinsi maendeleo haya yatakavyo saidia na jinsi yalivyokubalika, kwa wakati huo, mahali hapo kwa watu hao.

MAENDELEO KWA AJILI YA NANI ?​
Katika nchi nyingi za Kusini au nchi za ‘dunia ya tatu’, unaweza kuona majengo makubwa katika miji, mabenki, viwanda, na mahoteli. India yaweza ikawa mfano mzuri. Lakini watu wa Barahindi wamebaki maskini, wanalima lakini bila ya kujitosheleza kwa chakula. Hii si maana halisi ya maendeleo, haya ni maendeleo ya baadhi na baadhi ya watu tu.

Tangu Tanzania ipate Uhuru, serikali imejitahidi kulikwepa tatizo hiIi, na nafikiri kuendelea kulikwepa maradufu.
Vinginevyo, itajikuta imejenga nchi ya mataifa mawili, nchi moja kukaliwa na matajiri, na nchi nyingine kukaliwa na watu maskini sana.

MAFIA
Kila ninapokuja Mafia, watu huniuliza juu ya mabadiliko ya kimaendeleo ninayoyaona kama yapo. Wengi
hakuna maendeleo tangu kupatikana uhuru. Mimi nasema si kweli, hata kidogo. Naomba nianze na upande wa kwamba yapo maendeleo. Kwanza hebu tujaribu kuona jambo Ia muhimu Ia kuangaliwa katika Tanzania tangu uhuru. Tanzania imefaidika kwa amani na utulivu kuliko sehemu nyingi za Afrika, hivi sasa. Hakuna migogoro ya kidini, hakuna migogoro ya makabila, hakuna vita vya w enyewe kwa wenyewe, hakuna vita kati ya Tanzania na nchi za jirani.

Tukiangalia sehemu nyingine za Afrika, tutaona kuwa nchi ya Tanzania ninchi ya bahati. Angalia Somalia, Angola, Mozambique, Liberia, Sudan, Burundi na Rwanda, nchi ambazo zinatukumbusha na kutufundisha kuwa amani ni baraka, na lazima itunzwe na kuheshimiwa Hebu natuangalie mabadiliko yaliyokwishatokea kati ya miaka sitini na tisini.
a) Elimu
NiIipokuja hapa kwa mara ya kwanza mwaka sitini na tano, Mafia kulikuwa na shuIe chache sana za msingi,
na zilikuwa zinaishia darasa Ia nne tu. Ni vijana wachache waliokuwa wakienda kuendelea na masomo,walipelekwa kusoma bara. Hata hivyo, wengi wa vijana waliosoma wakati huo, walikuwa wavulana tu.

Nilipokuja mara ya pili mwaka 1976 kulikuwa na mafanikio kidogo: watoto walikuwa wakienda shule, wakike
na wakiume, na kulikuwa na ongezeko kubwa Ia shule za msingi, hadi darasa Ia saba. Kanga, kwa mfano,kulikuwa na darasa Ia sita kwa Kanga na Bweni Ia kufurahisha sasa ni kwamba kila kijiji kina shule yake hadi darasa Ia saba. Hali kadhalika, hivi sasa Mafia ina shule ya Sekondari.

Napenda kuchukua nafasi hii
kuwapongeza wananchi wote wa Mafia waliojenga shule hii kwa pamoja. Kitendo hiki ni cha maendeleo makubwa.

b) Afya
Nilipokuja mwaka 1965 kulikuwa na zahanati chache vijijini na hospitali ndogo mjini KiIindoni. Wakati huo, zahanati zilikuwa na watumishi wachache waliochukuwa mafunzo. Nilipokuja tena mwaka 1976, nilizikuta hospitali hizo na nyingine ziIikuwa zimepewa wakunga, na kwa mwaka 1985 (safari yangu ya tatu) kulikuwa na MCH Clinic zinapelekwa kwa kila kituo cha afya wilayani. Hali hii ni bora
sasa kuliko pale nyuma.

Leo, idadi ya zahanati imeongezeka, na pia idadi ya wahudumu wenye ujuzi imeongezeka, hata utoaji wa meno sasa unafanywa vijijini kama Kanga. Kwa upande wa huduma ya kinga, sasa watoto wengi wanachanjwa kuzuia kifua kikuu, polio, dondakoo, kifaduro na pepo punda.

Sasa maisha ya watoto wadogo yanaangaliwa, na kutunzwa vizuri zaidi kuliko pale nyuma. La kufurahisha zaidi, hata mama waja wazito wanaangaliwa vizuri kwa kupatiwa kinga, matibabu na chanjo, hata pia huduma bora za kujifungua. Haya ni maendeleo ya aina yake, natumaini si kwa Kanga peke yake bali kwa Mafia nzima.

c) Maji
Nilipokuja mwaka 1965, Mafia.kulikuwa na ukame mkubwa. Kw a mfano, pale Kanga, maji yalikuwa hakuna, na mara nyingine watu walikuwa wakienda kufuata maji mpaka Kirongwe. Hata mimi
nilifuata maji Kirongwe, wakati huo. Visima vilikuwa katika hali mbaya sana. Mwaka huu, nimeona visima vingi vizuri vimechimbwa, na wananchi wanapata huduma ya maji kwa urahisi zaidi na maji
safi zaidi kuliko pale mwanzo. Kwa hali hii, wananchi wamepunguza kidogo kazi kubwa ya kuchota
maji.

VIZUIZI VYA MAENDELEO HAYA​
Ingawaje hakuna kati yetu hata mmoja hivi sasa anayeweza kusema kuwa hali yetu ni nzuri, na hatuna matatizo ya elimu wala afya, kwa sababu bado kuna matatizo mengi ya vifaa vya mashuleni,
waalimu, vitabu, madawati ya kutosha, vifaa vya mahospitali pia madawa, pamoja na hatua hiyo kubwa ya kimaendeleo iliyofikiwa.

Ingawaje kuna shule ya sekondari ni jambo zuri, lakini gharama ya kuwasomesha watoto katika shule iIe ingali na matatizo, kwa kuwa watoto inawabidi wajitegemee kwa malezi, kwa chakula, na mahitaji mengine.

Hii ina maana si watoto wote wenye
kupasi kuingia katika shule hii, wanafanikiwa kumaliza masomo yao, kama nilivyokwisha sema. Vivyo hivyo, kuna matatizo katika maswala ya afya, katika kutumia kw a mipango: kupatikana kwa dawa za kutosha, na kupatikana dawa za kinga, na wakati mwingine hata kushindwa kutekeleza kabisa kwa mipango yenyewe kwa ukosefu wa fedha.

Kwani, wakati mwingine hata mafuta ya taa ya kuwashia jokofu yanakosekana. Hali kadhalika, kama inavyofahamika, watu wengi wanakaa mbali kidogo na vituo vya afya. Kwa hiyo hata wengine hushindwa kutembea kwa miguu kuja
mahospitalinl. Vivyo hivyo, hata watumlshl huondoka kila mwisho wa mwezi kwenye hospitali zao kuja wilayani kwa ajili ya kupata mishahara.

Baadhi ya matatizo haya, si rahisi kuyazuia, upatikanaji wa dawa unategemea na serikali, kama vile
illvyo kwa walimu, vitabu, na vifaa vingine. Lakini kama illvyoonyeshwa, na jinsi ilivyofunguliwa shule ya Sekondari, wananchi pia wanaweza kusaidia katika nyanja mbalimball, kuongeza juhudi
maarifa na hata michango kidogo ili kutatua matatizo kidogo kutokana na uwezo wao.

MATATIZO YA MAENDELEO: MAFIA NA SEHEMU NYINGINE
Sehemu nyingine mathalan, katika Mafia zimepata maendeleo kidogo tu, kwa maana kuna wengi wamekuwa maskini zaidi kuliko walivyokuwa pale nyuma. Je, hii ni kwa sababu gani? IIi kufahamu
hali hii, inatubidi tuangalie mambo tofauti.
  • Hali ya uchuml wa dunia
  • Hali ya uchumi wa nchi
  • Hali ya uchumi wa wilaya na mkoa
  • Hali ya uchumi wa kijiji na nyumba

Ninajitahidi kulitupia macho kila moja kati ya haya, lakini itabidi ielew eke kw amba vyote hivi vinahusiana kwa karibu mno na kwamba vinaweza pia kuleta tofauti kwa kila kimoja.

a) Hali ya uchumu duniani
Tanzania, na hata klsiwa cha Mafia, ni sehemu ya uchuml wa ulimwengu. Tanzania inaagiza bidhaa kutoka nje, na kusafirisha vitu kama korosho, chai, kahawa, katani, pamba, mafuta, na kadhalika.

Lakini uchumi wa dunia kwa sasa ni chini. Hata kwa zile nchi zilizoendelea, uchumi wao upo katika sura mbaya, kwani kuna hali mbaya ya watu w engi wasiokuwa na kazi. Ingawaje, utaratibu ambao uchumi wa dunia umepungua kuendeleza, nchi kama vile USA, Ulaya na Japan, kuw a na njia za kibiashara kuendeleza Asia, Latin Amerika na Afrika. Mpango huu upo kw a sababu mbili zaidi.

Kwanza kupanga bei kwa bidhaa ambazo zinasafirishwa na Tanzania, na vile vile kupanga bei ya vitu ambavyo Tanzania inavihitaji kutoka nje, kama vile mafuta, mitambo na vipuli, vitu ambavyo bei
zake huongezeka mara kw a mara, wakati mazao ambayo Tanzania inauza hushuka mara kwa mara.

Kwa maneno mengine, kununua tractor moja mwaka huu Tanzania ingehitaji gharama mara tatu au nne zaidi ya kiwango cha nyuma pia, nchi zinazoendelea za magharibi zinaweza kuziwekea vikwazo nchi za kusini, na kusababisha usafirishaji kuw a na matatizo.

b) Hali ya uchui wa Tanzania
Kutokana na mambo kadhaa muhimu ya kiuchumi, Tanzania inaw eza kulazimika kuingia katika hali ya kukopa madeni makubwa ya pesa hasa kutoka kwenye Mashirika ya Fedha ya Kimataifa yaanl IMF.

Wakati huo, fedha hlzo zililazimika kulipwa, kwa riba kubwa. Tanzania si nchi peke yake inayokumbwa na janga kama hili. Nchi zote za Afrika zinakabiliwa na madeni makubwa na mizigo hiyo mara nyingi hukwamisha maendeleo papo hapo.

Wakati mwingine inabidi ikubaliane na masharti ya IMF iIi kurekebisha hall yake ya uchuml.
- Kuangalia kwa thamani ya fedha (kunafanya biashara kuwa na gharama zaidi)
- Vivyo hivyo kuanguka kwa mishahara (kunasababishwa na kupanda kwa hali ngumu ya maisha ya wafanya kazi)
- Kutokuw a na bei maalum ya vitu mbalimbali (kumesababisha kupanda kwa bei, na hivyo kuathiri gharama za maisha ya watu)
- Kuongezeka kwa riba (kumefanya gharama za mikopo kuwa kubwa)
- Kuharibu utaratibu wa uingizaji wa bidhaa kutoka nje (kumeipunguzia serikali gharama kama vile kutoa fedha kidogo kwa ajili ya huduma za elimu na afya).

c) Hali ya uchumu wa wilaya
Nini matokeo ya mambo haya ya kiuchumi katika ngazi za wilaya hasa kwa wilaya yetu ya Mafia?
- Vitu vingi vinapatikana sasa lakini gharama kubwa.
- Mishahara kwa wafanya kazi haikupanda sawa na kupanda kwa maisha.
- Bei za vyakula zimekuwa juu mno.
- Gharama za afya na elimu hazikwenda sambamba na kuongezeka kwa idadi ya watu na mahitaji yao.

Watu wamekuwa na wajibu wa kulipia gharama za masomo kw a watoto wao, na sasa wanaanza kulazimishwa kulipia gharama za afya.

Kwa jumla watu wengi wa Mafia ni wakulima wadogo wadogo wanategemea hasa vitu viwili:
- Chakula kidogo akilimacho kama vile mpunga, muhogo, viazi vitamu.
- Mazao kidogo ya biashara, hasa nazi na korosho.Kama bei ya mazao kwa wakulima ingeongezeka kulingana na kupanda kwa maisha, basi wasingeona ugumu kupanda kwa bei ya mahitaji yao ya kila siku. Ukweli wa mambo ni kwamba
bei za nazi bado hazijaongezeka isipokuwa mkulima anaweza kupata mwaka huu bei nusu kulinganisha na bei ya mwaka jana. Siku hizi wale wanaosafirisha nazi kutoka Mafia kwenda
Dar es Salaam, wakisha lipia gharama za usafirishaji, wanabakiwa na kiasi kidogo tu, ambacho hata hicho huw ezi kusema kw amba w amepata faida.

Lakini kuna mambo mengine ya hapa ndani yanayozuia ongezeko Ia uchumi wa Mafia. Baadhi yake yapo katika ngazi za kijiji, na mengine katika ngazi za kaya, nayo nitayaoorodhesha hapo
baadaye. Kwanza tuangalie hali ya wilaya kwa jumla.

Njia kuu za uchumi kuwa duni Mafia:
i) Wilaya ina barabara mbili tu, na hizo zote ziko kwenye hali mabaya sana, na kusababisha usafirishaji wa watu na bidhaa kuwa na matatizo makubwa. Pia hata vyombo vya kusafirishia
huchakaa haraka, hali hii inafanya wasafiri wa ndani wabaki wamekwama.

Papo hapo, usafiri kwenda nje ya Mafia ni tatizo jingine. Watu husafiri kwa mashua ambazo si hatari tu, lakini pia hazina starehe yoyote na kama tunavyoelewa, mashua inasafiri kwa kutegemea upepo na kujaa na kupwa kwa maji.
ii) Njia nyingine ya usafiri ni ya ndege ambayo ni ghali, na hivo haina maalum. Ndege tulizonazo ni ndogo na uwezo wake pia ni mdogo. Nimeambiwa kulikuwa na stima ikisafiri kati ya Mafia na
Dar es Salaam, lakini sasa haionekani. Kwa hiyo Mafia kwa hali zote haina usafiri maalum kutoka hapa kwenda bara, na matatizo wanayoyapata watanzania wote wakiwa hapa kuongezeka kutokana na hali ya Mafia kuwa kisiwa. Kwa hiyo mawasiliano kati ya Mafia na sehemu nyingine za Tanzania, hasa Dar es Salaam, ni magumu na mazito. Hata ndani ya kisiwa, njia kuu ya usafirishaji ni kutembea kwa miguu. Magari mara kwa mara yanaharibika na upatikanaji wa vipuli ni wa matatizo, mgumu, na wa gharama sana. Hata kwa watumishi wa serikali utendaji wao wa kazi umekuwa mgumu pia kw a sababu hata kutembelea maeneo yao ya kazi na kukutana na wananchi wameshindwa.

iii) Huduma za umeme hakuna isipokuwa Kilindoni, na huduma kubwa ya kazi hutengemea nguvu za jambo ambalo nitachukua muda kuziongelea kidogo. Hata mashine ya kutegemea nguvu ya
watu - baiskeli kwa mfano - zinapatikana kwa uchache na ghali sana. Papo hapo hakuna mashine za kulimia, na kama zipo ni chache mno, na hazitoshelezi kutokana na gharama za uendeshaji; Ia kustaajabisha hata mashine ndogo ndogo za mikono kama troli, inikokoteni, na
inashine za inikono za kusagia hazipatikani.

iv) Vifaa duni vya kuliinia kaina vile jembe la mkono, nundu na panga. Kilimo tunachotumia hapa
Mafia kinategeinea nguvu za watu, yaani nguvu kubwa hutuimika kwa muda mrefu kwa kupata kiasi kidogo kwa matumizi madogo ya mbolea na umwagiliaji, na mategemeo makubwa bado yapo
kwa ajili ya mvua. Tangu utaratibu wa kuweka kumbukumbu ya kilimo uanzishwe hapa, Mafia bado yaonyesha haijitoshelezi kwa chakula.

v) Gulio Ia mazao ya biashara yapo mbali na maeneo ya wananchi. Mara nyingi watu husafirisha inazao yao kwa mfano nazi, kupelekea Dar es Salaam, shughuli ambayo hufanywa na mkulima mwenyewe.
Ubunifu wa hali ya maisha ya Mafia
Pamoja na hali ngumu ya maisha, watu wa Mafia mnamudu kuishi hivyo hivyo. Wanaweza kutembea mwendo mrefu kwa ajili ya kuona ndugu na jamaa, kuhudhuria shughuli, kwenda mahakamani, kwenda katika ofisi mbalimbali, na kwenda hospitali ya wilaya na kadhalika. Pia
katika misafara kwenda Bara wanatumia ngalawa, mashua na majahazi. Baadhi ya vijiji wameweza kununua magari, matrekta, na kadhalika. Watu wengine wanafanya kazi kwa bidii, wakitumia nguvu zao kulima mazao ya chakula na biashara. Pia kama nitakavyoendelea
kusema hapo baadaye, watu wengine wanafanya kazi kupindukia. Watu wengine pia hujaribu kazi nyingine kw a ajili ⋅ya kujipatia maisha. Kwa mfano, kwa vijiji vya kaskazini, baadhi ya vijana sasa wanavua kamba ambao wanawapeleka Dar es Salaam na nje, na kupata bei nzuri kuliko samaki.

Kwa hiyo, watu wanaweza kubadilika, hawakosi ufumbuzi, wanatafuta shughuli nyingine.

Tunapotafuta vipi tunaweza tukaendelea, ni rahisi kupata majibu kwa ndoto, na kuweza kupata msululu wa vitu, na kusema kwamba kama tukipata vitu hivi, tutafurahi, na kwamba tutakuwa
tumepata maendeleo.

Vitu hivyo ni kama:-
- Barabara nzuri,
- Magari ya kutosha kusafirisha watu na mizigo yao.
- Umeme kw a vijiji vyote
- Huduma za simu na posta kwa Mafia nzima. Lakini kaina tunavyojua, vitu vyote hivi haviw ezi kupatikana kw a pamoja, au kwa siku moja, vingine kati yake vinahitaji fedha nyingi ambazo si kw a wilaya na hata serikali yenyewe haiwezi
ikazipata kw a mara moja.

Kwa hiyo, inatubidi tufikiri jinsi tutavyoweza kutumia tulivyonavyo kuweza kupunguza matatizo yetu na kuleta maendeleo na kuboresha hali ya maisha ya watu wetu wilayani?

Tunayo ardhi ya kutosha, na tunayo bahari pia. Tunaweza kupata chakula chetu na tuna mazao ya biashara. Mwisho wa hotuba yangu, nitajaribu kutaja mambo ambayotunaweza kuyafikiria jinsi tunavyow eza kutumia rasilimali tuliyonayo.

Tumejaribu kuzungumzia uchumi wa ulimwengu, uchumi wa taifa, na uchumi wa wilaya. Sasa hebu tuzumgumzie uchumi w a kijiji na kaya.

d) Hali ya uchumi kijijini
Kijiji ni sehemu ndogo ya wilaya ambayo inahitaji shule, kliniki, na utaw ala, lakini wanakijiji wanaweza wakaungana katika kuendesha miradi kama vile kununua lori au kujenga zahanati.
Kwa maana hii vijiji havikai peke yao bila ya kuungana, vijiji vinafaa viungane pamoja na wanavijiji pia wanaungana kijamaa wilaya nzima hata ukanda wa pwani ikiwemo Zanzibar na Pemba.

Papo hapo kuna tofauti baina ya vijiji vya kaskazini, vijiji vimejikusanya pamoja, kila kimoja kimezungukwa na msitu wake. Lakini kusini, kwa upande mwingine, eneo lake lote liinepandwa minazi. Kwa hiyo vijiji hivyo kuna nafasi ndogo ya kulima. Kwa hiyo, kila ki jiji kina utaratibu wake
maalum wa maisha.

Ni swala Ia msingi kuona kwamba maendeleo ya kila kijiji hutegemea kijiji kilivyo. Hakuna mtumishi yeyote wa serikali, au mtaalam wa kilimo, uvuvi au ufugaji anayeweza kujua habari za
kijiji fulani kupitia w anakijiji wenyewe.

Kwa maana hiyo, maendeleo hutegemea ujuzi wa wanavijiji, pamoja na elimu ya w ataalamu kutoka nje ya kijiji kile. Maendeleo hupatikana kutoka
chini kwenda juu. Lakini utaalamu wa mbinu mpya unapasw a kuletw a kutoka sehemu nyingine na kuenezw a vijijini kwa kupitia mikutano, semina na mafunzo mbalimbali.

e) Hali ya uchumi wa kaya
Kaya ni sehemu muhimu ya uzalishaji w a mazao ya chakula na biashara, ya uzalishaji na malezi ya watoto, na utunzaji wa w atoto na jamii. Kwa maelezo mengine, kaya ni sehemu maalum
ambayo kila mtu anaweza akapatiwa matunzo. Watu wote wa kaya wana haki ya kugawana pato Ia kazi yao. Je, hiyo ndivyo ukweli ulivyo? Si mara nyingi mapato ya watu wote katika kaya
moja kulingana. Hebu tuangalie kw a ndani kidogo mambo yanayo husika hapa.

i) Mgawano wa kazi
Hapa tunaona wanaume na wanawake wanafanya kazi tofauti. Kw a mfano, wanaume kazi yao ni kufyeka misitu, kuchoma moto na kujenga korti kuzunguka shamba, kuzuia wanyama waharibifu kama vile nguruwe. Kazi ya wanawake kuanzia upandaji, upaliliaji, ulindaji na uvunaji; labda pengine wanaume na wanawake husaidiana kulima viazi na mihogo.
Wanaume hufanya kazi zote zinazohusu upandaji wa minazi, na kwa hiyo, wanaume ndio wenye minazi kuliko wanawake.

Hii vilevile kutokana na urithi na desturi tangu huko nyuma na kadhalika. Hali kadhalika wanaume wana muda mwingi wanaweza kufanya shughuli nyingine za kujipatia mapato kama vile uvuvi wa samaki, kufanya vibarua, au kwenda mijini kutafuta kazi. Kwa wanaume kwa hali hii wana kila sababu ya kupata pesa zaidi, na kuonekana matajiri kuliko wanawake katika kaya, na hatakuw a na mali nyingi kama minazi, mikorosho, ng' ombe, .kuhodhi fedha yote, ndio huwa w anao
uw ezo w a kuamua jinsi ya kuitumia, kama kununua chakula, chakula gani, kununua nguo, sigara, hata kuoa wake w engine.

Lakini wanawake wana njia chache sana za kujipatia fedha. Wanaweza kuwa na kiasi kidogo cha minazi, lakini hata hivyo shughuli zote za sokoni ni za wanaume. Kwa hiyo, kazi za ziada wanabaki nazo, iii kuwapatia fedha na ukusanyaji wa mikeka mizuri, shughuli ambayo wanawake wa Mafia inawapatia heshima na umaarufu mkubwa. Lakini kutokana na kazi nyingi
walizonazo, wanawake wa Mafia humudu kwa mwaka mzima kutengeneza mikeka kati ya sita mpaka minane ambayo huiuza kwa T. Sh. 1,000/= tu kwa kila mkeka wakati mchuuzi ambaye ni mwanaume, huuuza mkeka huo kw a Sh. 2,000/= au zaidi huko Dar es Salaam. Ingawa huwa ni pesa chache, wanawake wengi sheria ya mgawanyo wa kazi kati ya mwanamume na mwanamke hapa Mafia ni kama ifuatavyo:
Mwanamume hushughulukia utafutaji wa chakula, mavazi, ada za shule, gharama za kila siku; wakati shughuli za mwanamke ni pamoja na kazi za nyumbani kuanzia kufikicha mpunga,
kupepeta, kutwanga, kupika, kwenda maji na kuni, na kuosha vyombo, kuangalia watoto kwa kuwanyonyesha, kuwalisha, na kuwaogesha, pamoja na kusafisha nyumba.

Lakini tukitazama ukweli wa mambo, tunaona kwamba wanawake wanashughulikia sana uzalishaji wa
chakula, yaani wa kilimo kuliko wanaume. Huwa pia na jukumu Ia kutafuta pesa kwa ajili ya matumizi ya nyumbani au nguo, jambo ambalo ni kazi za wanaume, isipokuwa wengi waohukwepa kwa visingizio vya kutokuwa na fedha, au kuamua kutumia pesa zao kwa vitu vingine.

Kwa hiyo tutaona kw amba kazi ya mw anamke ni kama ifuatavyo:
- Kulima mazao ya chakula
- Kufanya kazi za nyumbani, pamoja na kutengeneza chakula, na kulea w atoto.
- Kutafuta fedha, kw a mfano kw a kusuka mikeka.
Katika utafiti w angu nilioufanya hivi karibuni, saa za kazi za wanaume na wanaw ake ni tofauti sana. Wanawake wengi wanafanya kazi kutwa mashambani wakati w a kulima, lakini wanaume si sana kufanya kazi kutwa. Wanawake wanafanya karibu kazi zote za nyumbani,
labda w akipata misaada ya w atoto wakubwa wakati ambapo hawapo shuleni. Kazi hizo za nyumbani lazima zifanywe kila siku.

ii) Uzazi
Baada ya kazi zote hizo, wanawake ndio w anaobeba ujauzito, wanaozaa watoto,
wanaonyonyesha kwa miaka miwili. Hapa Tanzania wanawake wanazaa watoto wengi; hesabu ya watoto wastani kwa kila mwanamke ni saba, lakini wanaw ake wengi wa Mafia wameshika mimba mara kumi au zaidi. Wengi wanaanza kuzaa baada ya kuolew a mapema, kwa umri wa miaka 16, w akaendelea kuw a katika hali ya kuwa waja wazito au kunyonyesha mpaka umri wa miaka arobaini. Mambo haya yana maana gani kwa wanawake,
hali yao, na hali ya kaya yao?
- Wanawake wengi wana hali mbaya kiafya, hasa wengi wao wanapata upungufu wa damu.
- Wengi wao wanazaa watoto wadogo mno, ambao wengi wanakufa mapema.
- Wanawake ambao ni wajawazito, au wamezaa hivi karibu, haw awezi kulima kama kawaida, kwa hiyo kila wakati ambapo mw anamke anazaa w akati w a kulima, kaya inapata mavuno machache. Kwa hiyo, lazima w atu w ake w alime chakula zaidi. Kwa maneno mengine, kiwango cha malishaji, hasa cha mazao ya chakula, kinaathiriwa na swala Ia
uzazi. Uzazi unaathiriw a pia na sw aIi Ia uIishiaji. Mwanamke mja mzito akifanya kazi mno anaweza kuharibu mimba yake, au kupata mtoto dhaifu ambaye hatimaye hufa.
iii) Chakula
Sasa natuingie katika swaIa Iingine IinaIohusu kaya sehemu ambaye chakula hugawanywa.
Katika utafiti wangu, nimeweza kugundua kwamba wanawake wanapokuIa chakuIa,
w anaw apa chakuIa kingi na kizuri wanaume kuIiko wenyewe. Hivi kw a nini? Wanawake wanasema kama ifuatavyo:-
- Wanaume hukasirika sana kama haw akupewa chakuIa kizuri na kingi.
- Wanaume huhitaji chakuIa kingi zaidi kuIiko wanawake kwa sababu kutokana na kazi wazifanyazo ni muhimu zaidi.
- Wanawake wanoa uwezo wa kustahimiIi njaa zaidi kuIiko wanaume hii ni haIi ya
maumbiIe

Lakini haIi ya chakuIa ambacho mwanadamu anahitaji, ⋅hutegemea mambo mengi kama umri, uzito na urefu, kazi w azifanyazo (w aIe w anaofanya kazi za nguvu huIa zaidi) na haIi yao (mwanamke ⋅mja mzito au anayenyonyesha, huhitaji chakuIa zaidi kuIiko mwanamke wa kawaida).
Sehemu kubwa ya chakuIa katika nyumba hapa Mafia hununuIiwa kwa sababu nyumba chache hupata chakuIa wanachohitaji kwa mw aka. Kwa hiyo hununua sana unga wa dona. Zaidi ya
hayo, hununua kitoweo kama maharage au samaki, na mara chache kuku au nyama. Hii ni njia muhimu ya kujipatia protini nani ambayo ni muhimu hasa kwa ukuw aji w a wototo, kuwasaidia
kujenga miili yao na akili zao.

Moja kati ya matatizo tunayoona hapa na sehemu nyingine ni kwamba kila serikaIi au mtaaIamu anapozungumzia swala Ia chakula bora, hasa kw a w atoto, husema wanawake wanahitaji kuelemishwa. Lakini si hivyo, mara nyingi wanawake wanafahamu juu ya kinachohitajika
Iakini kinacho kosekana ni nguvu ya kuamua kipi kinunuliwe au uwezo w a kifedha.

Wanaume, kwa upande mwingine, wanaweza wakawa na yote haya; uwezo wa kuamua nini anunue, na
fedha, Iakini hukosa ujuzi juu ya chakula kipi ni muhimu kw a w atoto w ake na mw anamke mja mzito au anayenyonyesha. Vile vile, mw anamume anaweza asitambue kiasi gani cha kazi mwanamke anafanya, na kutolipa swala hili uzito unaostahili, au wanaweza hata kupuuzia kazi wanazozifanya wanawake huwa hazina umuhimu au si nzito kulingana na kazi wanazozifanya wao. Kwa hiyo, kazi ya wanawake haionekani umuhimu wake na kukosa kuthaminiwa au kwa
kifedha hata kw a chakula.

Je, sasa tufanye nini iIi kusaidia kuinua hali hii katika kila nyumba?

Mabadiliko yanyohitajika nyumbani
Kw anza kuw apunguzia kazi w anaw ake, hasa w aja w azito na wanaonyonyesha.

Je, kw a kufanyaje?
- Msaada mkubw a unahitajika kw a w atu waliobaki katika nyumba, kama vile watoto wakubwa na wanaume kuwasaidia wanawake. Kwani hakuna ubaya wowote
utakaotokea kwa mwanamume katika kuisadia kazi za nyumbani. Lakini ni vibaya sana mtu mwingine kukaa tu akiwatazama wenzio wanapata taabu na kuumia kw a kazi nzito za kila siku, ambazo kuwafaidia wote.

- Njia nyingine ya kugawana rasilimali ya ⋅nyumba kwa usawa kuanzia chakula na hata fedha. Si jambo Ia kushangaza kwa watu wa Mafia kwamba wanaume ndio mara nyingi hula mahotelini na mitaani kuliko w anavyofanya wanawake. Nadhani swala kubwa hapa ni uwezo wa kifedha.

- La tatu, kuongeza kiwango cha chakula na Iishe katika nyumba zetu, sababu
tumekwishaona kwamba wanawake na watoto hawana sehemu nyingine ya kupata vitu hivi.

- La nne, ni kufikiria kuwa pamoja mwanamke na mwaname katika nyumba jinsi gani wataweza kupata pato zaidi Ia fedha kwa maisha yao, iIi waweze hata kutoa matunzo ya ziada kwa w atoto w ao kama zile kuweza kulipia ada za shule na uanzishaji wa miradi mingine midogo midogo kwa maisha yao.

- La tano njia nyingine ni kupunguza uzazi wa mara kwa mara, ambao unampa
mw anamke nafasi ya kupumzika kati ya mtoto na mtoto; swala hili ni muhimu sana kwa afya zao. Zaidi ya yote ni muhimu pia kw a mtoto kupata kunyonya kipindi cha miaka miwili na kumpatia afya bora. Nadhani tunakubaliana kuwa hata mafundisho ya dini yanatueleza hivyo. Kwa hiyo ni vizuri akina mama wachukue uja uzito baada ya miaka miwili au zaidi.

- La sita si vyema watoto wakiwa bado wadogo kuzaa, sababu watakuwa hajakomaa kiakili na kimwili. Vile vile, si vizuri kabisa kwa akina mama wenye umri zaidi ya miaka 35 kuzaa sababu watakuwa wamechoka na kuweza kusababisha kushindwa kutunza
mtoto, na pia kuweza kusababisha kuwazaa w atoto tofauti tahira au wasiojiweza.

Hali hii ni hasara kwa ulimwengu, taifa, mkoa, wilaya, kijiji, mtaa, hadi nyumba.
Katika utafiti w angu, nimepata kusikia kutoka kwa wanawake wengi wa hapa Mafia wakisema kuwa wangependa zaidi kutumia uzazi wa mpangilio iIi wapate kupumzika, lakini waume zao hawapendi mpango huu, na wengi hawataki hata kusikia hatimaye sisi mwenyewe kama
w azazi kwa hiyo, uamuzi mkubwa wa utaratibu gani nyumba au kaya ichukue katika maswali ya uzazi, yanamtegemea zaidi mw anamume. Kwani kwa wao watoto ni utajiri , na kwamba utajiri wa mtu maskini ni watoto. Watu wote duniani wanakubaliana na ukweli huo, Iakini kuna
utaratibu wake, na tunavyosema hivyo, tunashaw ishika kw amba kuwa na watoto wengi pamoja ni mzigo tunaokubebesha.

MWISHO ( SHINIKIZO)
Mapendekezo:
Mapema katika hotuba yangu nimesema tunapozungumzia swala Ia maendeleo yatupasa tujiulize maswali yafuatayo:

Kwanza , nini tunataka?

Pili, ni vipi vitakavyo tusaidia kupata mahitaji yetu?

Tatu, nini matokeo kutokana na maendeleo hayo? Ni maendeleo kwa watu wote au ni maendeleo kwa watu wachache? Pia nilisema Mafia inayo rasilimali:
- Watu wake na elimu yao
- Utaratibu walionao; ardhi nzuri; na bahari.
Kutokana na babadiliko mafupi, tunaweza kupiga hatua kubwa ya maendeleo.

I. Kuzidisha uzalishaji wa chakula.
Kama watu wengi wataalam sana, wataweza kujipatia chakula cha kutosha, wataweza kutumia baadhi ya fedha wanazozipata kununua vitu vingine
kama nguo nzuri, watasomesha watoto wao vizuri, na watanunua vitu vingine kama vile redio na baiskeli. Je, tutayapataje haya?
- Tutayapata haya kwa kuwashawishi wakulima kulima zaidi na kupanua mashamba ya chakula
- Kumfundisha kila mkulima, wanawake kwa wanaume, kulima kwa kutumia njia bora za kilimo.
- Kumsaidia kila mkulima kupata vifaa bora vya kulimia na kuvuna.
- Kumshauri mkulima jinsi ya kuhifadhi chakula chake.
- Ni bora ieleweke kuwa kuvuna vizuri maana yake ni kupata chakula cha kutosha na kukihifadhi kwa matumizi ya baadaye.
- Njia nyingine ya kuongeza pato Ia mkulima ni kuongeza ulimaji wa mboga za aina mbalimbali kama vile mchicha, nyanya, bamia, matango, matikiti, maboga, fivi, kunde,- na kadhalika.

2. Utuimiaji wa mbinu bora na za kisasa
Utumiaji w a njia rahisi za kilimo kwa kutumia rasilimali tulizonazo unaw eza ukafanya kilimo chetu kiwe na matatizo makubwa, kw a mf ano kupanda mazao kwa mistari au kwa hatua zinazopendekezwa na kilimo bora zinaweza kumzidishia mkulima mapato. Nadhani mnakubaliana na mimi kwamba si kila mtu kati yetu anaweza kununua trekta kwa ajili ya kulimia, na wala siyo uwezo wa serikali yetu. Kwa nini tupoteze wakati wetu kufikiria upatikanaji wa matrekta ya kutosha kwa ajili ya kulimia wakati tunaweza tukazalisha vizuri na
kwa urahisi kwa kutumia ujuzi na vifaa tulivyonavyo? Kwa hiyo, si bora wataalam wetu wa kilimo watuelezee zaidi mbinu za kilimo rahisi ambacho kila mkulima w etu anaweza kazitumia?

3. Ufugaji bora
Ufugaji bora w a ng'ombe maana yake ni kupata nyama kwa wingi na maziwa kwa wingi kwa ajili ya Iishe, na vilevile kuweza kupata mifugo yenye uwezo wa kutusaidia katika kilimo na kubebea mizigo yetu, pia na upatikanaji w a mboleo wa kutosha. Si vibaya hapa tulipo tukifikiria upatikanaji wa biogas kwa ajili ya kujipatia umeme kwa urahisi kuliko kufikiria umeme kama huu tulionao hapa Kilindoni ambao hutegemea mafuta ghali.

Ni vizuri vile vile tuwahimize wakulima wetu na wananchi kwa ujumla ufugaji wa wanyama wanaostawi vizuri hapa kwa gharama nafuu kama vile kuku, bata, punda na mbuzi: kuku na bata kwa ajili ya mayai na fedha, mbuzi kwa ajili ya maziwa na nyama, punda kw a ajili ya
kubebea mizigo.

4. Uendelezaji wa kilimo cha biashara
Ndugu zangu nionavyo mimi, ninyi w atu w a Mafia mna bahati kubwa kuwa na ardhi nzuri kwa maisha yenu kama mngeitumia vizuri kw a ulimaji w a mazao ya biashara, badala ya minazi na mikorosho peke ⋅yake mngeweza kupata fedha nyingi. Sehemu mlizopanda minazi na mikorosho bado zinatoa nafasi kw a kupanda mazao mengine ya muda mfupi ya biashara kama vile kokoa, pilipili, mapapai, ndizi, machungwa, na mboga mboga. Je, kw a nini hatufanyi hivi?
kuna sheria ⋅yeyote ndogo iliyow ekw a na serikali inayowazuia msifanye hivyo?

5. Soko lingine la minazi
Hivi sasa, soko Ietu Ia nazi Ia Dar es Salaam limezidiwa na hivyo kusababisha nazi zetu zikose bei nzuri. Yatubudi hivi sasa tutafute njia zingine. Kw a mfano nimesikia kw amba Mafia Coconuts Limited (MCL) sasa hivi ina mpango mpya w a kuboresha mashamba yake na kusindika upatikanaji wa mazao ya minazi kama vile mafuta , sumba, vifuu, na unja
w a vifuu, na kuuza nje. MCL pia ingeweza Iabda kununua nazi kutoka kwa wakulima
wengine, na kusaidia kw a upatikanaji w a soko kw a urahisi kuliko ulivyo sasa.

6. Njia zingine za kupatia mapato
a) Bahari nzuri tuliyonayo tungeweza kuitumia kuanzisha mashamba ya mw ani kuliko kuishia na kuvua samaki peke yake. Hali kadhalika hata uvuvi wenyewe ungebalidishwa kidogo kwa kuwasaidia wavuvi wetu kupata msaada au mikopo ya kuw apatia vifaa bora na vya kisasa vya uvuvi. Kwani kufanya hivyo kutasaidia upatikanaji wa samaki wengi na wazuri na
kwa hali hiyo wavuvi wetu wapate fedha na kuweza kumudu maisha yao vema zaidi. Ni vizuri tunapozungumza ugumu wa maisha tuonyeshe jinsi gani tunajitahidi kukabiliana nayo sisi
wenyewe kwa njia nafuu tulizonazo.

b) Ufugaji wa nyuki. lnavyoonekana, hali ya hewa ya Mafia inaruhusu ufugaji wa nyuki. Je, isingekuw a bora tukaanzisha mashamba ya nyuki kw a ajili ya asali na nta? kwa mfano pale Kanga chupa moja ya asali inauzw a kati ya sh.400/= mpaka 700/=. Je, hii isingesaidia?

7. Uanzishaji wa ushirika wa watenegengezaji wa mikeka vijijini

Kisiwa cha Mafia kina bahati ya kuwa na wasukaji wazuri wa mikeka, lakini wanakosa namna ya kuendeleza kazi hiyo na kuitegemea. Hivi sasa wasukaji w engi vijijini wanakabiliwa na matatizo mawili: kwanza upatikanaji wa rangi za mikeka, na pili, soko Ia mikeka. Kwa nini ufundi
huu tusingetumia kuwapatia wananchi wetu pato kwa maisha yao? Kuna haja gani kuanzisha miradi mikubwa na migeni wakati tunaiacha mizuri na ya gharama nafuu inayoweza kutupatia pato kubwa kwa wananchi wetu? Ingefaa tutupie macho vitu kama hivi iIi kuinua hali ya maisha yetu kwa urahisi na haraka zaidi, natubidi tutilie mkazo mambo muhimu mawili: kuboresha njia ya usafirishaji ndani ya Mafia na nje ya Mafia. Tunahitaji barabara nzuri, na usafari w a stima
wakati wote. Nimepata habari karibuni kwamba barabara zetu zinatengenezwa. Ukweli ni kwamba kama hali za barabara zote zitakuwa nzuri naamini itaamsha maendeleo kwa wilaya nzima.

Haya ni mapendekezo yangu tu - mengine yanawezekana, mengine hayawezekani, kama tungeongeza uzalishaji wa kila mtu, tungew eza kuinua hali ya maisha na hali ya kinga ya miili yetu kwa magonjwa.

Kufanya hivyo , ndio kuishi vizuri. Na kama tungeweza kuinua pato letu la kila siku, tungewawezasha watu wetu kuwa na vitu vingi. Kwa ufupi, tungemfanya kila mtu
kuw a na maisha bora.

Mwisho zaidi, nimefurahia sana na safari ya mw aka huu kw ani nimekuja Mafia mara tatu bila ya kupata bahati ya kukaribishwa nizungumze chochote wilayani, lakini mwaka huu

kutokana na kuanzishwa kwa Chama Cha Maendeleo ya Mafia (Chamama) kumenifanya mimi niwe hapa leo na kuweza kuongea na nyi hapa. Na viIi vile nimefurahi sana kuona kwamba
NGO kama Chamama imeanzishw a hapa Mafia. Natumaini mtanivumilia na kunisamehe kwa yote yale ambayo Iabda hayakuwafurahisha. Yawezekana yote hayo ni kutokana na mchanjo wangu mdogo wa lugha ya Kiswahili. Nawashukuru wote kwa kuja kunisikiliza.

ASANTENI SANA, NA KWAKERINI
Yalichapishwa 25th May 2014
 
Nyerere na Maana halisi ya Maendeleo
 
Nikisoma mfano wa wilaya hii ya Mafia na kuhusu dhana ya maendeleo naona wilaya nyingi zina vipaumbele vinavyofanana na mahitaji ya wilaya ya Mafia na pia tafsiri yao ya maenedeleo vinashabiana.

Turudi kwa vipau mbele vya uongozi wa awamu ya tano ya CCM ambavyo ni kuhamia Makao Makuu Dodoma, ndege za Bombadier, Dreamliner, SGR reli, barabara za Flyovers, madaraja ya baharini, magari ya kifahari ya gharama ya viongozi wa serikali ......n.k

Maendeleo ya vitu vyote hivi ambavyo CCM ya awamu ya 5 inadai ndiyo maendeleo na vipaumbele vya wananchi, lakini ukweli wananchi wengi ktk wilaya nyingi vipaumbele vyao ni vingine kabisa.

Si bure wananchi walia maisha ni magumu pamoja na kufanya kazi kwa bidii na nguvu nyingi lakini serikali kuu iliyohodhi madaraka yote vipau-mbele vyao havilengi kuwasaidia wananchi walio wengi wanaoishi ktk wilaya nyingi mbalimbali wenye vipau-mbele visivyofanana na vya serikali kuu yenye makao Dar-es-Salaam na Dodoma.
 
26 July 2019

Wananchi wapiga yowe wakipanda chombo ktk mazingira yenye changamoto kubwa

Kisiwa cha Mafia kilichopo bahari ya Hindi nchini Tanzania kimekuwa hakina usafiri wa hakika kwa miaka 58. Usafiri huo wa kukiunganisha kisiwa hicho na maeneo ya Tanzania Bara na Zanzibar ili kuchochea uchumi wa wakazi wa kisiwa cha Mafia.



Source: MwanaHALISI TV
 
PROF LWAITAMA ASHANGAA DHANA YA MAENDELEO KWA KUWACHUKUA WANANCHI KWENDA KUSHANGAA NDEGE
Akiongea kwenye Mdahalo ulioandaliwa na Chama cha wanasheria Tanzania (TLS) kujadili na kupata maoni ya wadau mbalimbali ikiwemo wananchi, Prof Lwaitama ameshangaa dhana ya Serikali kuwachukua wananchi kwenda kupokea ndege ili hali Uhuru wao umetoweka.​

Source: CHADEMA MEDIA TV
 
Naombeni msaada juu ya kilimo cha maindi matatizo yake yaani magonjwa kwa heka mbili mpaka kukamilika itaniharimu bei gani?
 
Ahsante kwa bandiko.....Kumbe hotuba imetolewa 1994, nilianza kusema mbona jamaa anasema amekaa miaka 29 alafu anazungumzia 1965, akili yangu ilikuwa inanituma kwa kuwa kiswahili ni shida labda alimaanisha 1995
 
Back
Top Bottom