Maana ya kampeni - kwa nini nichaguliwe mimi na si mpinzani wangu ? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Maana ya kampeni - kwa nini nichaguliwe mimi na si mpinzani wangu ?

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Mag3, Aug 31, 2010.

 1. Mag3

  Mag3 JF-Expert Member

  #1
  Aug 31, 2010
  Joined: May 31, 2008
  Messages: 9,094
  Likes Received: 6,188
  Trophy Points: 280
  Inaonekana Tume ya Uchaguzi kwa sababu wanazozifahamu wameamua kutoa tafsiri mpya kwa maana ya kampeni ya Uchaguzi. Ninavyoelewa mimi kufanya kampeni ni kujinadi kwa wapiga kura kwa nini wakuchague wewe na si mpinzani wako.

  • Kujinadi kunajumuisha kutaja sifa zako na uwezo wako kwa nini utakuwa kiongozi bora kuliko mpinzani wako na hivyo unastahili kura zao.
  • Kujinadi pia kunajumuisha kutaja mapungufu ya mpinzani wako kwa nini hana sifa ya kuwa kiongozi bora na hivyo hastahili kura yao.
  Tume ya Uchaguzi kupitia sheria ya uchaguzi inamtaka mgombea asiongelee mapungufu ya mpinzani wake - ni wapi duniani sheria hii inatambulika na kutumika kwaniinazua maswali mawili;

  • Kwa mtu anayeutafuta uongozi kampeni itafanyika vipi kama sheria inamzuia kutaja kwa nini yeye anafaa zaidi kuliko kiongozi aliyeko madarakani ?
  • Ataelezeaje atakavyotekeleza mambo tofauti kama hakuonyesha mapungufu ya kiutekelezaji na uwezo mdogo wa kiongozi anayetaka kumwondoa ?
  Je kuna mambo Tume ya Uchaguzi isingependa wananchi wapiga kura wayafahamu kuhusu utawala wa sasa ? wanachojaribu kuficha ni kitu gani na kwa maslahi ya nani ? Jaji Lewis Makame, huwatendei haki wazalendo wa nchi hii. Je ni dhambi kuwatahadharisha wananchi kuwa mgombea fulani asipewe kura kwa sababu kadhaa ?
   
Loading...