Maana ya Jina la Rais wa Tanzania, Samia Suluhu

FaizaFoxy

Platinum Member
Apr 13, 2011
92,881
109,188
Jina la Rais wetu Bi Samia Suluhu limeundwa kutokana na maneno ya Kiarabu.

1) Samia: Maana yake ni msikivu. Neno hili hupatikana hata katika salat za kila siku kwa Waislaam, pale Muislam anaposali, akinyanyuka kwenye rukuu husema "Samia Llahu liman Hamida". maana yake, Ni "Allah humsikia mwenye kumhimidi".

2) Suluhu: Ingawa neno hili linatokana na neno la Kiarabu "Sulh" lakini Kiswahili tunalitumia sana, suluhu kwa maana ya kukubaliana yaishe kwa amani na si kwa ugomvi.

Mfanya Suluhu mara nyingi huwa ni anaeheshimika na pande zote mbili, msikivu, mwenye hekima na asiependelea.

Tutegemee mema sana kutoka Kwa bi Samia Suluhu.

Ma Shaa Allah.

Ndugu yetu kaongezea maana ya jina la tatu: Maana ya Jina la Rais wa Tanzania, Samia Suluhu.
 
Karibu tena na sana mkuu hapa jukwaani.

Ulipotea na baadhi yetu tunaokujali na tunothamini mchango wako tukaanza patwa na wasiwasi.

Shukran kwa kutufafanulia maana ya jina la rais wetu mpya. Tutegemeeni makubwa kutoka kwake na Allah amuongoze!
 
Wewe Ustadhati Faiza na Mzee Mohamed Said hapa JF forum nawapongeza sana kwa Propaganda za kidini na kutaka kuligawa Taifa

Naona mmetoka mafichoni sasa mnaanza kuhubiri udini kama kawaida yenu

Ahaaa nilijua tu sasa utakuja kwa kasi baada ya miaka mitano kujificha chini ya utawala wa JPM, Sasa umekuja kueneza Propaganda na itikadi kali za kidini kama kawaida yako

Huu ni mwanzo tu Mama Faiza naona mvua yenyewe tunasubiri

Ni wakati mtaanza tena kushinikiza mahakama ya kadhi kama wakati wa JK

Ni wakati Mama asipokuwa makini Nyaraka kali na za onyo zitaanza kutembezwa toka CCT, Tec na Vatican

Ndio maana JK aliamua kuziba masikio na kusafiri tu kila siku maana nyumbani ilikuwa Wengine Nyaraka Wengine Tunataka Mahakama ya kadhi

Tutashuhudia mengi
 
Hata kwa sura tu unaona kabisa huyu ni mtu mwema. Tofauti na yule katili dikiteta, nitamkubali huyu mama, iwapo atawaonea huruma wafanyakazi wa chini kwa kuongeza mishahara.
Wafanyakazi kuweni wabunifu kipato chenu kiongezeke. Msitegemee kila kitu kufanyiwa na serikali, anzeni kufikiria nyinyi mnaifanyia nini serikali.

Tazama hawa wazee wa Madrassa wamewaletea fursa za kuwawezesha kujiongezea kipato hamzioni, mmekalia mnangoja huruma za serikali tu. Anzeni kwa kujihurumia wenyewe, Soma: "Social Economic Empowerment Program,." Madrassa Yabuni Mpango wa Kijamii wa Kuwezeshanana kiuchumi. Haujawahi kutokea, duniani.
 
Jina la Rais wetu Bi Samia Suluhu limeundwa kutokana na maneno ya Kiarabu.

1) Samia: Maana yake ni msikivu. Neno hili hupatikana hata katika salat za kila siku kwa Waislaam, pale Muislam anaposali, akinyanyuka kwenye rukuu husema "Samia Llahu liman Hamida". maana yake, Ni humsikia mwenye kumhimidi.

2) Suluhu: Ingawa nen hili linatokana na neno la Kiarabu "Sulh" lakini Kiswahili tunalitumia sana, suluhu kwa maana ya kukubaliana yaishe kwa amani na si kwa ugomvi.

Mfanya Suluhu mara nyingi huwa ni anaeheshimika na pande zote mbili, msikivu, mwenye hekima na asiependelea.

Tutegemee mema sana kutoka Kwa bi Samia Suluhu.

Ma Shaa Allah.
Jina halina maana yoyote katika uongozi wa nchi bali sifa za mtu binafsi,weledi, uadilifu, ubunifu, uaminifu, uchapakazi na mengine kama hayo. Sijui majina ya Magufuli yalikuwa na uhusiano gani na utendaji wake. Nadhani mleta mada anataka kupromoti imani yake ya kiarabu.
 
Wewe jina lako ulilopewa na wazazi lako ni nani tukupe maana yake.
 
Jina la Rais wetu Bi Samia Suluhu limeundwa kutokana na maneno ya Kiarabu.

1) Samia: Maana yake ni msikivu. Neno hili hupatikana hata katika salat za kila siku kwa Waislaam, pale Muislam anaposali, akinyanyuka kwenye rukuu husema "Samia Llahu liman Hamida". maana yake, Ni "Allah humsikia mwenye kumhimidi".

2) Suluhu: Ingawa neno hili linatokana na neno la Kiarabu "Sulh" lakini Kiswahili tunalitumia sana, suluhu kwa maana ya kukubaliana yaishe kwa amani na si kwa ugomvi.

Mfanya Suluhu mara nyingi huwa ni anaeheshimika na pande zote mbili, msikivu, mwenye hekima na asiependelea.

Tutegemee mema sana kutoka Kwa bi Samia Suluhu.

Ma Shaa Allah.

Hassan mbona hujaliletea maana yake?

Kuna mtu mmoja aliwahi Nipa maana ya majina..

Zinedine yazid Zidane...
It was so beautiful ukipewa maana ya majina yote..
 
Muda mrefu mpenzi sijakusoma. Nilikuita kwenye uzi fulani ukaita. Karibu tuyajenge
 
Jina halina maana yoyote katika uongozi wa nchi bali sifa za mtu binafsi,weledi, uadilifu, ubunifu, uaminifu, uchapakazi na mengine kama hayo. Sijui majina ya Magufuli yalikuwa na uhusiano gani na utendaji wake. Nadhani mleta mada anataka kupromoti imani yake ya kiarabu.

Hujui halafu unasema havina maana?Wakati unakiri hujui??
 
Wewe Ustadhati Faiza na Mzee Mohamed Said hapa JF forum nawapongeza sana kwa Propaganda za kidini na kutaka kuligawa Taifa

Naona mmetoka mafichoni sasa mnaanza kuhubiri udini kama kawaida yenu

Ahaaa nilijua tu sasa utakuja kwa kasi baada ya miaka mitano kujificha chini ya utawala wa JPM, Sasa umekuja kueneza Propaganda na itikadi kali za kidini kama kawaida yako

Huu ni mwanzo tu Mama Faiza naona mvua yenyewe tunasubiri

Ni wakati mtaanza tena kushinikiza mahakama ya kadhi kama wakati wa JK

Ni wakati Mama asipokuwa makini Nyaraka kali na za onyo zitaanza kutembezwa toka CCT, Tec na Vatican

Ndio maana JK aliamua kuziba masikio na kusafiri tu kila siku maana nyumbani ilikuwa Wengine Nyaraka Wengine Tunataka Mahakama ya kadhi

Tutashuhudia mengi
Kila mtu na muono wake na uupo huru na maoni yake.

Soma mada kisha uijibu, achana na sisi binafsi.
 
Back
Top Bottom