Maana na aina za sentensi katika lugha ya Kiswahili

Suley2019

JF-Expert Member
Oct 7, 2019
1,812
4,533
1 Sentensi Shurutia.
ni sentensi inayohuundwa kwa viambishii kama -ngeli-, -nge-, na -ngali-.
kwa mfano:
(1) ningelikutana naye angelinisaidia sana.
vilevile aina hii ya sentensi hutumia kiambishi -ki-;
kwa mfano:
(1) ni kimwona tu nitakwambia.​

2 Sentesi-Sahili​
Sentesi sahili ni kifungu cha maneno chenye kiima na kiarifu na chenye kuleta maana kamili iliyokusudiwa. Isitoshe, hii ni sentesi ambayo haifungamani na sentesi nyingine yo yote.

Mifano:
(i) Huu si ugonjwa wa kutisha.
(ii) Mama anapanda mahindi.
(iii) Mbunge wetu anahutubia.
Katika sentesi-sahili (i) – (iii), zote ni sentesi sahili ambazo kila moja ina kiima kimoja na kiarifu kimoja.Aidha, zote huleta maana kamili.

3 Sentesi Ambatani
Sentesi ambatani ni sentesi iliyoundwa ama kwa kuambatanisha au kuunganish

Mifano:
(a) Sentesi-sahili na Sentesi sahili;
(i) Khamisi alifika na Asha akaimba sana.
(ii) Mgonjwa hali wala haendi choo.
(iii) Mama analima shambani lakini Baba yeye halimi.
(iv) Yosefu anakunywa sana pombe ila sigara havuti.
au

(b) Sentesi sahili na Sentesi changamani;
(i) Khamisi alifika ukumbini na Binti aliyemwimbia akachoka.
(ii) Mkewe hampelekei mumewe chakula sipitalini wala waliopenda hawamletei cho chote.
(iii) Mama mdhaifu anafanya kazi kila siku lakini Baba aliye na afya nzuri hafanyi kazi.
(iv) Watu wanene hawali sana ila wembamba hula sana.

au
(c) Sentesi-changamani na Sentesi-changamani;
(i) Khamisi alipofika ukumbini akaketi na binti aliyemwimbia akachoka baada ya saa moja.
(ii) Wasanii walipoingia ukumbini hawakuimba wala hawakucheza walipotakiwa kufanya hivyo.
(iii) Mama asipofanya kazi husemwa lakini baba asipofanya kazi hasemwi.
(iv) Watu walio wembamba hula sana ila wasio wembamba hawali sana.

4 Sentesi Changamani​
Sentesi-changamani ni sentesi iliyoundwa kwa sentesi sahili na tungo tegemezi. Kwa kuwa maana ya tungo tegemezi hukamilishwa na maana ya sentesi sahili, sentesi changamani hujitokeza kama sentesi mchanganyiko, yaani maana za sentesi-mbili sahili zilizochanganyishwa.
Mifano:
(i) Binti ambaye hakufika jana, asimame.
(ii) Viti ambavyo vimevunjika, tutavitengeneza.
(iii) Wanaojidai shupavu, mkamfunge paka kengele). nk.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom