Maana halisi ya siri za nchi ni nini na ni zipi?

Nimekwambia Google Sheria ya Utunzaji wa Siri.
Ni Sheria namba 4 ya mwaka 1970.
Mfano mitihani ya Taifa inayoandaliwa na NECTA ni miongoni mwa Siri za nchi ingawa Siri hii ni ya muda mfupi, mitihani hiyo ikisha fanyika siyo Siri tena. Ila Kuna zile wanaita top secret hizi Huwa ni hiri Hadi ukamilifu wa dahari.
 
mf; jpm aliwahi nusulika kufa kwa sumu zaman sana enz za uwazili ila hakuwahi sema;;amekuja sema hiv majuz koz haikuwa siri tena,coz ilikuwa kitambo,, nimeongeza ili aelewe mleta mada
Hii ishu ya viongozi kupewa sumu ni SIRI kwa wengi wanaohusika na wachache wanaofahamu kwa undani wake.. Lakini nyakati zikitimia moja moja itadondoshewa jamii
 
Umeziita SIRI halafu unataka kuzijua! Anyways, utajua tu kile unachopaswa kujua. Kuna vitu anajua Rais tu na wanaompa hizo taarifa, hata Makamu wa Rais havijui.
 
Sio lazima
Taifa ililiendeshwe ni lazima kuwepo siri nzito za kiutawala , kiuchumi, kijamaa, kisiasa, ili kulinda usalama wa Taifa...

Ukitaka kujua siri nzito..za nchi mkuu jiunge na idara ya usalama wa Taifa.. na wewe ujifunze hizo siri ila out of that you can't know.
 
Kuna mambo lazima yawe siri tu hata chumbani kwako.

Udhaifu wako
Mipango yako
Utegemezi wako
Itikadi zako
Tabia yako
Asili yako

Igeuze kwenda kwenye swali la muulizaji.

JamiiForums mobile app
Sawa ila hayo ya mtu mmoja mmoja hayana shida.

Mimi nataka kujua Siri za kitaifa ambazo Mimi na wewe lazima/inabidi,/tunatakiwa/ kuzijua ili tushiriki kikamilifu kulilinda na kulijenga taifa letu.

Kwa mfano umeambiwa nchi yako kwa Sasa Ina upungufu wa wanajeshi idadi Fulani na wewe kwa kutambua wajibu wako katika ulinzi unajitolea kumpeleka mwanao,ndugu yako, au hata wewe mwenyewe.

Sent from my Infinix X5515 using JamiiForums mobile app
 
In fact sio SIRI kana SIRI bali ni taarifa fulani kwa kundi fulani la watu na kwa wakati fulani.. Kiingereza inaelezeka vizuri zaidi kama CLASSIFIED INFORMATION kwakuwa hakuna SIRI ya watu wengi
Wenzetu kwa kutambua binadamu hawezi kukaa na kitu rohoni milele basi huwa na utaratibu wa kuujulisha umma habari fulani muda unapopita na inapoonekana habari husika haina madhara tena
1.Kuna 'siri' huwa wanazifahamu marais tuu(lakini kiuhalisia sio siri bali ni classified information
2. Kuna hizo siri wanazifahamu rais na mawaziri tuu
3. Kuna hizo siri wanazifahamu wabunge tuu..
Mambo huenda hivyo mpaka level ambayo hufikia isiwe siri tena kwakuwa jambo fulani kadiri linavyozidi kufahamika na wengi ndio 'usiri' wake hupungua

Kitengo cha usalama wa taifa ndio huwa kina dhima na jukumu la kutunza kinachoitwa siri za nchi..lakini nao si wote wanaweza kujua kila kitu kwa wakati fulani
Good
 
Noo simaanishi ziandikwe hapa.

Nilimaanisha niambiwe Siri gani sitakiwi kuzijua Kama raia wa kawaidana faida yake ni ipi nikizijua aunikiendelea kutozijua.
Ambazo zipo nje ya mamlaka yako.
Hata ukizijua huna amri yakuzisema.
Subiri tukuteue halafu tukutegeshe hizo siri uzione kama utatoa nje.
 
Mkuu usitake kuzijua!ukizijua hutokua Salama!!!Kuna mambo hufanyika kwa siri kwa usalama wetu!kuna watu huuawa,hufungwa hata hutiwa vilema ili nchi iwe salama!!!Mf. majuzi tu hapa tumempoteza Waziri fulani kwa kosa la kutotunza siri za nchi yetu!!!RIP E.K!!!
Yule msukuma wa Ushetu Kahama Elias Kwandikwa? Alikuwa chini chini na kaanzia jeshini kumbe alikosea akatapika siri wakaamua kudeal naye???!!!
 
Maana halisi ya SIRI za nchi yeyote ni Usalama wa Nchi, watu wake,mipaka yake, mipango ya muda mfupi na mrefu, mahitaji muhimu kwa wakati uliopo na ujao/takwimu n. k.

Hivyo sio sawa kwa mwenye dhamana ya mifano iliyopo hapo juu kujifanya ama kwa kujua au kutokujua kusambaza kwa namna yeyote details /nyaraka ambazo hazitakiwi kujulikana kwa wengine wasio na mamlaka nazo na pengine usambazaji wake haukufuata utaratibu yakinifu hivyo kuleta taaruki, njama/nia ovu, uchochezi au namna yeyote ya kuhujumu Nchi na watu wake.

SIRI ndio msingi wa uajibikaji,uadilifu,uaminifu,unyenyekevu,kuwa na hofu ya Mungu, hekima, busara, uvumilivu na upendo (AMANI na UTULIVU).

SIRI ndio kipimo number 1 cha UADILIFU na UAMINIFU.
 
Kwa kuwa sijui Kama nimeamka vibaya au vizuri naomba niende moja kwa moja kwenye kilichonituma niulize swali hapo juu.

Kumekuwa utaratibu uliozoeleka hapa bongo unaoitwa Siri za nchi na kwanini kuwepo na usiri katika baadhi ya mambo yanayolihusu taifa...
maana halisi ya siri za serikali ni mfano pale makomandoo wanaomlinda mbowe ambao wameshitakiwa naye, wanapokuwa walikula kiapo cha kufa na kupona kulinda siri za serikali, halafu mbowe na chadema wanaamini ni wenzao hadi wanawatetea, bila kujua kuwa wale walikula kiapo cha kufa na kupona na maisha yao yote watakuwa loyal kwa serikali kuliko kwa mbowe na chadema. hivi huwa wanafikiria hili?
 
14 Reactions
Reply
Back
Top Bottom