Maana halisi ya siri za nchi ni nini na ni zipi?

In fact sio SIRI kana SIRI bali ni taarifa fulani kwa kundi fulani la watu na kwa wakati fulani.. Kiingereza inaelezeka vizuri zaidi kama CLASSIFIED INFORMATION kwakuwa hakuna SIRI ya watu wengi
Wenzetu kwa kutambua binadamu hawezi kukaa na kitu rohoni milele basi huwa na utaratibu wa kuujulisha umma habari fulani muda unapopita na inapoonekana habari husika haina madhara tena
1.Kuna 'siri' huwa wanazifahamu marais tuu(lakini kiuhalisia sio siri bali ni classified information
2. Kuna hizo siri wanazifahamu rais na mawaziri tuu
3. Kuna hizo siri wanazifahamu wabunge tuu..
Mambo huenda hivyo mpaka level ambayo hufikia isiwe siri tena kwakuwa jambo fulani kadiri linavyozidi kufahamika na wengi ndio 'usiri' wake hupungua

Kitengo cha usalama wa taifa ndio huwa kina dhima na jukumu la kutunza kinachoitwa siri za nchi..lakini nao si wote wanaweza kujua kila kitu kwa wakati fulani
Duh!
 
Taifa ililiendeshwe ni lazima kuwepo siri nzito za kiutawala , kiuchumi, kijamaa, kisiasa, ili kulinda usalama wa Taifa...

Ukitaka kujua siri nzito..za nchi mkuu jiunge na idara ya usalama wa Taifa.. na wewe ujifunze hizo siri ila out of that you can't know.

Ni nani kakuambia ukijunga na idara ya usalama wa taifa utajua siri za nchi/taifa...!?
Siyo kila aliyeko kwenye idara hiyo anafahamu kila kitu kuhusu siri za nchi!
Acha kuleta stori za vijiweni wewe...
 
Uovu wote unaofanywa na serikali ndio huitwa siri za serekali/nchi.
simaanishi ziandikwe hapa.

Nilimaanisha niambiwe Siri gani sitakiwi kuzijua Kama raia wa kawaidana faida yake ni ipi nikizijua aunikiendelea kutozijua.
 
Siri ni nyingi sana, mifano michache ni hii:

1. Ni namna gani watawazunguka wafadhiri wa nchi ili waendelee kukamuliwa;
2. Namna watatumia misaada au kuisambaza misaada hiyo nchini bila kelele toka sehemu mbalimbali;
3. Ukweli katika taarifa Halisi za mambo ya uviko; hali ya chakula nchini; hali ya nchi kiuchumi, kisiasa , kijamii bila kuleta taharuki nchini;
4. Hali halisi na utayari ktk vyombo vya usalama nchini..
5. Na mengineyo mengi ya namna gani nchi inaongozwa- ni kama vile kuna Job descriptions za kuiongoza nchi, yaani Raisi na serikali ni lazima wafanye mambo Fulani ili nchi itule au itawalike watake au wasitake...ikiwemo kubambikizia watu kesi Ili watu hao waache kelele zao na wajipambanie mahakamani huko na mwisho wa siku attention inakwenda kwingine na mambo ya nchi yanaenda kama chain of custody inavyotaka...
Ya sirini ni mengi kwa kweli -utayajua tu ukiwamo ndani si huku nje...na ukiyachunguza sana utajua si Siri Bali ni uongo na uoga wa serikali wa kufanya matendo maovu... wewe tathmini kesi nyingi za jamuhuri uone ni kitu gani jamuhuri wanalalamika...mfano
1. Watu kuandamana
2. Nchi kutotawalika
3. Mikataba feki
4. Madeal ya kuwanufaisha watawala
5. Mgao wa umeme
6. Wa maji
7. Etc
Mifano ya Siri ni mingi sana... ni headache tupu huko serikalini sijui watu wanakimbilia nini kungangani madarakani Kama Akina CCM...ni kama vile. wanaogopa kuchomolewa maana undondocha wao wanaouita Siri za nchi au za chama na serikali utajulikana tu Mara wakitolewa kwa namna yeyote ile... piga ua, ni lazima watatumia kila njia kuzilinda siri zao zikiwemo mbinu za kubakia madarakani...
Ni maoni yangu- ruksa kuyapinga
Kama no huvi basi mwenda zake alikuwa dahihi urais ni mzigo mzito.

Kwenye hiyo watake wasitake nimejikuta naogopa sana
 
Ndani ya nchi za kidikteta ambazo hazina demokrasia ya kweli, serikali wanafanya kila kitu kwa siri ili waweke wananchi gizani. Mikataba siri, takwimu za ugonjwa wa corona siri, kila kitu siri. Wananchi wanabaki gizani.
 
Huyo Mshana Jr ndio kakuingiza chaka kabisa! Google Sheria ya Utunzaji Siri u siri uone.
Hebu lete ya kwako tulinganishe.

Yule kajibu kitaalamu na kiuhalisia zaidi

Wewe lete hata hayo yaliyobase kwenye chuki na kuisimanga serikal nitapokea tu.
 
Ila wabongo sijui ni ubishi au ignorance.
Asa siri za serikali utaziwekaje kwenye mitandao?
 
In fact sio SIRI kana SIRI bali ni taarifa fulani kwa kundi fulani la watu na kwa wakati fulani.. Kiingereza inaelezeka vizuri zaidi kama CLASSIFIED INFORMATION kwakuwa hakuna SIRI ya watu wengi
Wenzetu kwa kutambua binadamu hawezi kukaa na kitu rohoni milele basi huwa na utaratibu wa kuujulisha umma habari fulani muda unapopita na inapoonekana habari husika haina madhara tena
1.Kuna 'siri' huwa wanazifahamu marais tuu(lakini kiuhalisia sio siri bali ni classified information
2. Kuna hizo siri wanazifahamu rais na mawaziri tuu
3. Kuna hizo siri wanazifahamu wabunge tuu..
Mambo huenda hivyo mpaka level ambayo hufikia isiwe siri tena kwakuwa jambo fulani kadiri linavyozidi kufahamika na wengi ndio 'usiri' wake hupungua

Kitengo cha usalama wa taifa ndio huwa kina dhima na jukumu la kutunza kinachoitwa siri za nchi..lakini nao si wote wanaweza kujua kila kitu kwa wakati fulani
mf; jpm aliwahi nusulika kufa kwa sumu zaman sana enz za uwazili ila hakuwahi sema;;amekuja sema hiv majuz koz haikuwa siri tena,coz ilikuwa kitambo,, nimeongeza ili aelewe mleta mada
 
Ulimchangia Mello chochote katika kuanzisha hii forum hadi uandike huo ujinga ulioandika?
Mjomba wangu huyo kwa hiyo hebu potea hapa nenda kwa waandika (ASA), (xaxa) wenzako.
 
Sawa natulia. Nawe endelea kula matango pori toka kwa kina Mshana Jr.
Kuna vitu Kama raia lazima uvijue ili ushiriki kikamilifu katika kilinda na kuijenga nchi yako sio mtu uende ende tu Kama kopo linalosukumwa na upepo.
 
Back
Top Bottom