Maana halisi ya siri za nchi ni nini na ni zipi?

MR KUO

JF-Expert Member
Jan 8, 2016
2,395
3,247
Kwa kuwa sijui Kama nimeamka vibaya au vizuri naomba niende moja kwa moja kwenye kilichonituma niulize swali hapo juu.

Kumekuwa utaratibu uliozoeleka hapa bongo unaoitwa Siri za nchi na kwanini kuwepo na usiri katika baadhi ya mambo yanayolihusu taifa?

Sasa Leo naomba wajuzi mniambie hizi Siri za nchi ni zipi ambazo Kama raia wa nchi husika hatutakiwi kuzijua na kwa nini?

Ipi faida na hasara Kama ikitokea raia wakazijua au wakaendelea kutozijua?

Na vipi hao watunza Siri husika huwa ni watu gani na wangapi kwa nchi nzima?

Msinitukane Wala kuniona mshamba tafadhari.

Asante.
 
Ndo nimeomba uniambie Sasa hizo Siri ni zipi??

Kumbuka Siri za nchi ni zetu sote Sasa Mimi sizijui ili nishiriki kuzilinda.
Siri za nchi zipo ndani ya serikali.
Serikali haijashare siri zake na yeyote, sasa unataka sisi tuseme siri zipi tena?

Njia rahisi nenda serikalini uwahoji watakupatia siri ambazo hawataki zitoke.

Parking at your own risk
 
In fact sio SIRI kana SIRI bali ni taarifa fulani kwa kundi fulani la watu na kwa wakati fulani.. Kiingereza inaelezeka vizuri zaidi kama CLASSIFIED INFORMATION kwakuwa hakuna SIRI ya watu wengi.

Wenzetu kwa kutambua binadamu hawezi kukaa na kitu rohoni milele basi huwa na utaratibu wa kuujulisha umma habari fulani muda unapopita na inapoonekana habari husika haina madhara tena.

1.Kuna 'siri' huwa wanazifahamu marais tuu(lakini kiuhalisia sio siri bali ni classified information
2. Kuna hizo siri wanazifahamu rais na mawaziri tuu
3. Kuna hizo siri wanazifahamu wabunge tuu..
Mambo huenda hivyo mpaka level ambayo hufikia isiwe siri tena kwakuwa jambo fulani kadiri linavyozidi kufahamika na wengi ndio 'usiri' wake hupungua

Kitengo cha usalama wa taifa ndio huwa kina dhima na jukumu la kutunza kinachoitwa siri za nchi..lakini nao si wote wanaweza kujua kila kitu kwa wakati fulani
 
Ndo nimeomba uniambie Sasa hizo Siri ni zipi??

Kumbuka Siri za nchi ni zetu sote Sasa Mimi sizijui ili nishiriki kuzilinda.
Unataka akuambie wakati ameshasema siri, sasa ikishakuwa siri maana yake hazijui.

Acha ushamba
 
Kwa kuwa sijui Kama nimeamka vibaya au vizuri naomba niende moja kwa moja kwenye kilichonituma niulize swali hapo juu.

Kumekuwa utaratibu uliozoeleka hapa bongo unaoitwa Siri za nchi na kwanini kuwepo na usiri katika baadhi ya mambo yanayolihusu taifa...

Siri za nchi/taifa maana yake ni mambo au mipango muhimu kwa taifa lolote lile duniani, ambayo mipango hiyo imewekwa kwa makusudi ya kulinufaisha taifa; mipango hiyo inaweza ikawa na madhara kwa taifa lingine, lakini jambo muhimu ni kuleta unafuu wa maisha na maendeleo kwa taifa husika lililoweka mipango hiyo.

Bila ya kujali kwamba kufanya hivyo ni kulidhuru au kuyadhuru mataifa mengine, na taifa hilo wakati wote linahakikisha kwamba mipango hiyo haijulikani kwa taifa lingine lolote zaidi ya taifa hilo na ndiyo maana mipango hiyo ikaitwa siri za taifa.

Taifa lolote lenye watu wenye akili timamu na linaloongozwa kwa taratibu za sheria na utawala bora ni lazima liwe na siri za taifa; siri ambazo hazitakiwi kujulikana na taifa lingine lolote.

Siri hizo zinalindwa na sheria ya usalama wa taifa!
 
Taifa ililiendeshwe ni lazima kuwepo siri nzito za kiutawala , kiuchumi, kijamaa, kisiasa, ili kulinda usalama wa Taifa...

Ukitaka kujua siri nzito..za nchi mkuu jiunge na idara ya usalama wa Taifa.. na wewe ujifunze hizo siri ila out of that you can't know.
 
Siri za nchi/taifa maana yake ni mambo au mipango muhimu kwa taifa lolote lile duniani, ambayo mipango hiyo imewekwa kwa makusudi ya kulinufaisha taifa; mipango hiyo inaweza ikawa na madhara kwa taifa lingine, lakini jambo muhimu ni kuleta unafuu wa maisha na maendeleo kwa taifa husika lililoweka mipango hiyo, bila ya kujali kwamba kufanya hivyo ni kulidhuru au kuyadhuru mataifa mengine, na taifa hilo wakati wote linahakikisha kwamba mipango hiyo haijulikani kwa taifa lingine lolote zaidi ya taifa hilo, na ndiyo maana mipango hiyo ikaitwa siri za taifa. Taifa lolote lenye watu wenye akili timamu na linaloongozwa kwa taratibu za sheria na utawala bora ni lazima liwe na siri za taifa; siri ambazo hazitakiwi kujulikana na taifa lingine lolote.
Siri hizo zinalindwa na sheria ya usalama wa taifa!
Asanteeeeeeeeeeeeee sana
 
Siri ni nyingi sana, mifano michache ni hii:

1. Ni namna gani watawazunguka wafadhiri wa nchi ili waendelee kukamuliwa;
2. Namna watatumia misaada au kuisambaza misaada hiyo nchini bila kelele toka sehemu mbalimbali;
3. Ukweli katika taarifa Halisi za mambo ya uviko; hali ya chakula nchini; hali ya nchi kiuchumi, kisiasa , kijamii bila kuleta taharuki nchini;
4. Hali halisi na utayari ktk vyombo vya usalama nchini..
5. Na mengineyo mengi ya namna gani nchi inaongozwa- ni kama vile kuna Job descriptions za kuiongoza nchi, yaani Raisi na serikali ni lazima wafanye mambo Fulani ili nchi itule au itawalike watake au wasitake...ikiwemo kubambikizia watu kesi Ili watu hao waache kelele zao na wajipambanie mahakamani huko na mwisho wa siku attention inakwenda kwingine na mambo ya nchi yanaenda kama chain of custody inavyotaka...
Ya sirini ni mengi kwa kweli -utayajua tu ukiwamo ndani si huku nje...na ukiyachunguza sana utajua si Siri Bali ni uongo na uoga wa serikali wa kufanya matendo maovu... wewe tathmini kesi nyingi za jamuhuri uone ni kitu gani jamuhuri wanalalamika...mfano
1. Watu kuandamana
2. Nchi kutotawalika
3. Mikataba feki
4. Madeal ya kuwanufaisha watawala
5. Mgao wa umeme
6. Wa maji
7. Etc
Mifano ya Siri ni mingi sana... ni headache tupu huko serikalini sijui watu wanakimbilia nini kungangani madarakani Kama Akina CCM...ni kama vile. wanaogopa kuchomolewa maana undondocha wao wanaouita Siri za nchi au za chama na serikali utajulikana tu Mara wakitolewa kwa namna yeyote ile... piga ua, ni lazima watatumia kila njia kuzilinda siri zao zikiwemo mbinu za kubakia madarakani...
Ni maoni yangu- ruksa kuyapinga
 
Back
Top Bottom