Maana halisi ya nguvu ya umma! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Maana halisi ya nguvu ya umma!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by MwanaFalsafa1, Jan 30, 2011.

 1. MwanaFalsafa1

  MwanaFalsafa1 JF-Expert Member

  #1
  Jan 30, 2011
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 135
  Tokea mapinduzi ya Tunisia yatokee na sasa yanayo elekea kutokea Misri nimekua nikisoma maoni ya wanaJF mbali mbali ambao baadhi wao (sina uhakika kama ni wengi wao) wana hoji kwa nini hayo haya tokei Tanzania?

  Kwanza niseme tu kwamba lazima tuambiane ukweli. Mapinduzi si jambo jema hata kama saa nyingine ni lazima. Pia mapinduzi si lazima yalete demokrasia au mabadiliko. Kwa maana ukiangalia Mapinduzi ya kwanza ya Ufaransa wananchi waliondoa ufalme lakini wakaishia kurudi huko huko. Kwa maana kwenye mapinduzi unaweza kuondoa mfumo uliopo kwa kukaribisha mfumo bora zaidi au hata mbaya zaidi. Yaweza kwenda upande wowote.

  Sasa tuje kwenye maana ya "nguvu ya umma" au "people's power". Ni kweli wananchi wana nguvu sana kwani "There is more power in numbers than anything else". Lakini kwa sababu nguvu ya wananchi ipo kwenye idadi yao basi mabadiliko yoyote lazima yatokane na wananchi walio wengi kutaka mabadiliko hayo.

  Kwa hiyo kwenye mabadiliko yoyote tunaona kwamba lazima kuwe na mambo mawili:
  a) Wachache wenye ujasiri wa kuanzisha mapambano ya mabadiliko (Tunisia yalianzishwa na mtu mmoja tu kuji choma moto)
  b) Support ya wananchi walio wengi. (Tunisia baada ya jamaa kuji choma moto watu wakainukwa na msisimko wa kimageuzi).

  Kwa hiyo jamani kama leo mnaoshabikia mapinduzi Tanzania mnaona hayaja tokea mjue basi hapo kuna sababu mbili
  a) Wote mnaoshabikia ni waoga kwa maana hamna hata mmoja wenu ambae mpaka sasa hivi kajitolea kuwa muanzishaji.
  b) Kama wapo waliojitolea kuanzisha (na kama wamesha anzisha) basi ina maana mageuzi hayo hayana support ya umma (watu wengi)

  Amini usiamini wenzangu kama kweli Tanzania ingekua nchi ya mapinduzi basi yaliyo jiri Mwanza na Arusha yangesha anzisha mageuzi hayo. People's power is only as strong as it's people.

  Tusi shabikie mapinduzi. Kama hayaja tokea jua ina maana wengi wenu mnaogopa mapinduzi na wengi hawaya support. Tuna hitaji mapinduzi ya kifikira na mageuzi yatokee kwenye boxi la kupigia kura. Na tusi singizie wizi kwa maana Ivory Coast tumeona serikali iki chakachua lakini kutokana na wingi wa kura wa mpinzani hazi kuchakachulika.
   
 2. G

  Gad ONEYA JF-Expert Member

  #2
  Jan 30, 2011
  Joined: Oct 26, 2010
  Messages: 2,641
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  So?
   
 3. M

  Mwan mpambanaji JF-Expert Member

  #3
  Jan 30, 2011
  Joined: Apr 3, 2008
  Messages: 468
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  Wewe ni mmoja wa waoga maana hata hujataja what to do,zaidi ya kujifanya wajua maana ya peoples power,hujui chochote maana hakuna asiyejua kuwa mapinduzi ya ufaransa yameleta maendeleo si tu ufaransa bali ulaya,ndio yalikuwa mwanzo wa mapinduzi ya viwanda barani ulaya,jambo lolote lina gharam na lazima zilipwe hivyo hatuogopi wala hatutaogopa gharama za mapinduzi,kwa Tanzania ni swala la muda,na kamwe kipimo cha arusha na mwanza haviwezi kuwa sababu,the move is on and the time will determine our victory
   
 4. Mzalendo80

  Mzalendo80 JF-Expert Member

  #4
  Jan 30, 2011
  Joined: Oct 30, 2010
  Messages: 2,385
  Likes Received: 122
  Trophy Points: 160
  :sick:Baba yako ni fisadi? mbona unaiyogopa sana nguvu ya umma kama wewe ni mtoto wa fisadi basi isubirie nguvu ya umma ikiingia mitaani ndio utaielewa vizuri. inavyoelekea umeshaingiwa au mmeshaingiwa na hofu juu ya nguvu ya umma:roll:
   
Loading...