Maana halisi na lengo la "diaspora" nini? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Maana halisi na lengo la "diaspora" nini?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Technician, May 3, 2011.

 1. Technician

  Technician JF-Expert Member

  #1
  May 3, 2011
  Joined: Mar 30, 2010
  Messages: 843
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  WanaJF,
  Naomba ufafanuzi kwa yeyote anayejua maana ya DIASPORA na malengo yake kwa uhakika.
  Naomba kuwakilisha.
   
 2. The Prophet

  The Prophet JF-Expert Member

  #2
  May 3, 2011
  Joined: Mar 17, 2011
  Messages: 682
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  diaspora (sina hakika na spelingi).

  ni jamii ya waafrika (si lazima waafrika tu) waliotawanyika katika nchi mbalimbali za ughaibuni. hawa ni watu ambao kikwete wetu huwa anawalilia walete ukwasi wao (in case wanao) katika nchi walikozaliwa ili kujenga maendeleo kwa nchi zao. hakuna hotuba yoyote kikwete anaweza kuitoa mbele ya wazungu asitamke neno 'dayaspora'.
   
 3. Technician

  Technician JF-Expert Member

  #3
  May 3, 2011
  Joined: Mar 30, 2010
  Messages: 843
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Thanks for your comments.
   
 4. U

  Ulimakafu JF-Expert Member

  #4
  May 3, 2011
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 18,005
  Likes Received: 741
  Trophy Points: 280
  Asante sana mkuu kwa ufafanuzi,nami nilikuwa nikitatizwa.
   
 5. M

  Mkeshaji JF-Expert Member

  #5
  May 3, 2011
  Joined: Jan 7, 2011
  Messages: 4,264
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Ingia google. Tafuta meaning ya diaspora, utapata maelezo mazuri sana. Lakini kwa jinsi ninavyoelewa mimi ilianzia na Jews.
   
 6. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #6
  Aug 15, 2017
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,576
  Likes Received: 18,550
  Trophy Points: 280
  View attachment 566354

  [​IMG]
  Katibu Mkuu Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Salum Maulid Salum, akitoa taarifa kwa waandishi wa habari juu ya kongamano la nne la kitaifa la Watanzania wanaoishi nje litakalofanyika tarehe 23 na 24 Agosti hapa Zanzibar. Hafla hiyo imefanyika Ikulu mjini Zanzibar.
  [​IMG]
  Katibu Mkuu Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Salum Maulid Salum, akitoa taarifa kwa waandishi wa habari juu ya kongamano la nne la kitaifa la Watanzania wanaoishi nje litakalofanyika tarehe 23 na 24 Agosti hapa Zanzibar. Hafla hiyo imefanyika Ikulu mjini Zanzibar.
  [​IMG]
  Mkurugenzi wa PPR Pascal Mayalla akiuliza suali katika mkutano na waandishi wa habari uliozungumzia Kongamano la kitaifa la Watanzania wanaoishi nje uliofanyika Ikulu mjini Zanzibar.
  [​IMG]
  Mkurugenzi Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa na Uratibu wa Wazanzibari wanaoishi nje ya nchi Bi. Adila Hilali Vuai akijibu masuali yaliyoulizwa na wandishi wa habari kuhusu maandalizi ya kongamano la kitafa litalofanyika tarehe 23 na 24 Agosti hapa Zanzibar. (kushoto) Muandishi wa habari Rahma Suleiman wa Chuchu Fm Redio.
  Picha na Makame Mshenga.
  Wanabodi.

  Declaration of interest. Japo mimi Paskali Mayalla sio mwana Diaspora, bali nimewahi kuishi nje kwa muda mfupi mfupi katika nchi mbalimbali, na nimewahi kufanya kazi tena sio kubeba box, bali kubeba zege ndani ya jiji la London, hivyo nina mwanga kidogo kuhusu diaspora, ila kwenye hili
  Kongamano la Nne la Diaspora, litakalo fanyika Zanzibar, tarehe 23 na 24 Agosti, I have a role to play.

  Hivyo hili ni bandiko la kuomba ushirikiano wenu, kwa ushiriki wako kwenye kongamano hili, physically or by proxy, ili kutoa mawazo yako Tanzania ikusaidiaje ili kukuwezesha wewe kuisaidia nchi yako.

  Tanzania itajengwa na Watanzania wote wakiwemo wana diaspora. Kitu cha kwanza ni kuomba ushiriki wako physically kwa wale wenye nafasi to make it home, wajisajili kupitia
  DIASPORA: Home Page
  or
  4TH Tanzania Diaspora Conference 2017 - Diaspora and SMEs ...

  Kwa wale ambao hawatapata nafasi ya kuwepo physically, wanaweza kushiriki by proxy, kwa vile dunia sasa ni kijiji kimoja, wanaweza kushiriki by proxy.

  Kwanza The Official Opening ya Kongamano lenyewe litatangazwa live za TV za Tanzania. Pili tutatangaza live kupitia video streaming kwenye youtube hivyo wana diaspora wote wenye nafasi wanaweza kufuatilia kupitia youtube, facebook, tweeter na mitandao ya kijamii.

  Hapa naomba ushirikiano wako tujadiliane how to reach you out ili tupate maoni na mawazo yako, Tanzania ikusaidiaje wewe mwana Diaspora ili uweze kuisaidia nchi yako?.

  Uzalendo sio kujiuliza "Tanzania Ikusaidie nini, bali ni wewe kujiuliza jee nimeisaidia nini nchi yangu Tanzania?". Kwa vile wana diaspora wengi wako nchi za nje na wamepata bahati ya kupata exposure kubwa, tunaomba mawazo yenu, Tanzania iwasaidieje ili muweze kuisaidia nchi yako Tanzania.

  Natanguliza Shukrani.

  Pascal Mayalla
  +255 784 270403
  pascomayalla@gmail.com
   
Loading...