Baada ya Januari 20 kupita, TCRA yasema itakuwa inazima laini za simu zisizosajiliwa kwa alama za vidole kwa awamu

Influenza

JF-Expert Member
Jul 1, 2018
1,445
3,403
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), James Kilaba amesema uzimaji wa laini za simu ambazo hazijasajiliwa kwa alama za vidole unafanyika kwa awamu kuanzia jana Jumatatu Januari 20, 2020 ili kuondoa usumbufu.

Amesema hadi jana saa nne usiku walikuwa wamezima laini 975,041.

Amesema kundi la kwanza waliozimiwa laini ni watu 656,091 ambao wana vitambulisho vya Taifa au namba lakini hawajasajili laini zao.

Kilaba amesema kundi la pili ni watu 318,950 waliosajili laini zao kwa kitambulisho cha Taifa kabla ya kuanza mfumo wa kusajili kwa alama za kidole.

“Hawa wote hawana sababu ya kutozimiwa laini zao leo, uzimaji huu hatutaki kumnyang’anya mtu laini yake ambayo ameizoea ila tutaisitisha kutoa na kupokea huduma. Hivyo simu yake itapokea ujumbe mfupi tu ambao utakuwa unamkumbusha usajili” amesema Kilaba akibainisha kuwa usajili wa laini za simu hauna kikomo.

Ameongeza, “tunazima kidogo kwa sababu ya mambo ya kitaalamu, hauwezi ukazima laini milioni tano au 10 kwa mara moja.”

“Tunahitaji warudi, tukiwazimia tunategemea kesho watarudi kwenye foleni za kuhuisha laini zao kwa hiyo wakienda wengi zaidi hawatapata huduma kama ambavyo walijaa juzi na jana na leo mpaka mifumo ya Nida inaelemewa.”

Amesisitiza kuwa watafanya kistaarabu na kiufundi uzimaji laini ili mifumo isielemewe kwenye usajili.
 
Kila jambo lina faida na hasara lak

Hii ni miradi ya uswahili sana, nakumbuka tumeanzia kwenye Imei za cm feki zinafungiwa lakin bado tatizo liko palepale, leo hii kusitishwa huduma za mawasiliano kwa kutosajili alama za vidole, wakati swala la kupata kitambulisho tu cha taifa, inachukua miezi mitatu.hii inaboa sana kufuatilia kadi moja kila cku mlango wa Nida kama omba omba.
 
Dah
IMG-20200121-WA0008.jpeg

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom