Unaleta siasa sio sheria.Leo habari iliyo juu ni uamuzi wa spika Tulia Ackson wa kuwaruhusu Halima na wenzake kuendelea kuwa wabunge licha ya kutokuwa wanachama wa chama chochote cha siasa, jambo ambalo ni kinyume na matakwa ya katiba yetu.
Spika Tulia anasema, hawezi kuwaondolea ubunge wabunge waliovuliwa uwanachama wa chama cha siasa kwa sababu wabunge waliovuliwa uwanachama wa CHADEMA, wamefungua kesi mahakamani kupinga kufutwa kwao uwanachama! Ni sababu ya kushangaza, ni sababu ya kipuuzi na kinafiki kwa sababu mfumo wa sheria haufanyi kazi namna hiyo.
Leo hii, hata ukifukuzwa kazi na muajiri wako kimakosa, huwezi kuendelea kuwa mfanyakazi eti kwa sababu tu umefungua kesi. Kama anayoyasema Tulia, ndiyo mifumo ya kesi ingekuwa inafanya kazi namna hiyo, basi mambo yangekuwa hovyo sana.
Siku zote, hukumu ya mwanzo huendelea kusimama mpaka siku kitakapopatikana chombo cha juu zaidi chenye mamlaka ya kisheria au kikatiba kuweza kutengua uamuzi wa awali.
Anachosema Tulia, ni dhihirisho la unafiki mkubwa uliopo nchini mwetu. Sheria hazina maana, bali zinapindishwa ili kutekeleza matakwa ya watu fulani.
Utawala wa awamu ya 5 haukutaka demokrasia, lakini baadaye baada ya kuona kuwa utakosa pesa ya Jumuia ya Madola, wakalazimisha, kwa kutengeneza upinzani bandia Bungeni.
Lakini tuwe wakweli, ndani ya Bunge hili bandia, nani ana ujasiru wa kumwadhibu mwingine? Karibia wabunge wote, pamoja na spika, waliopo huko Bungeni, ni zao la uovu mkubwa, uchafu, na takataka za kila aina zilizotendwa mwaka 2020 wakati wa utawala dhalimu wa kipindi cha giza.
Ubunge wa kupewa wa akina Halima una tofauti gani na ule wa kupewa wa Spika, na wengine wengi ambao wapo Bungeni? Hawa wabunge pamoja na huyu Spika, ambao wote walipachikwa na marehemu bila ya ridhaa ya wananchi, wana uhalali gani wa kuwaondoa akina Halima kwenye Bunge hili fake wakati nao wamefika hapo kwa namna ile ile ambayo akina Halima walifika?
Akina Halima walipelekwa pale na jiwe, huyo spika, naye kapelekwa pale na jiwe, ni nini kinachowafanya akina Halima wawe batili, halafu akina Katambi waliopata kura 3 kwenye kura za maoni dhidi ya Masele aliyepata kura 360 za wajumbe, lakini Jiwe likamviringisha mpaka kwenye unaibu Waziri?
Tufahamu tu kuwa akina Halima, ni waovu kama wenzao wengi waliojazana kwenye hilo jumba. Tunasubiria embe chini ya mchongoma.
Sheria za kazi sio sawa na siasa. Kule kazini wanaangalia uwezekano muajiri kuathirika ikiwa muajiriwa atamhujumu..
Lakini wameweka fidia kubwa sana ikithibitika kuwa kulikuwa na makosa ktk kumfukuza pia wameweka fidia pesa aliyostahili kuwa amelipwa na atakayolipwa mpaka mwisho wa mkataba au kurudishwa kazini pia kuna fidia ya defamation ambayo kiwango chake ni kikubwa sana
Defamation kwa mwanasiasa hailipiki atakuambia mimi nilikuwa nataka niwe Raisi ningepata pension ya Urais wewe umeharibu carrier yangu nilipe fidia. Je chama kitaweza kuwalipa?